Captain Edward Lowassa.....Tido Mhando Rudisha Kipande Cha Interview Yangu Kuhusu Richmond na Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Captain Edward Lowassa.....Tido Mhando Rudisha Kipande Cha Interview Yangu Kuhusu Richmond na Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kipanga mlakuku, Oct 31, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. k

  kipanga mlakuku Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mambo yanazidi kukolea kuhusu sakata la Ricmond na Dowans mara baada ya waziri mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond Bw Edward Lowassa kumtaka aliwahi kuwa Mkurugenzi wa TBC1 Bw Tido Mhando kuachia kipande cha mahojiano kinachodaiwa kunyofolewa makusudi kwa amri ya wakubwa ambacho kilifanyika katikati ya mwaka 2008 kati ya Tido Mhando na Edward Lowassa.

  Hatua hii ya Lowassa inadaiwa kuchochewa zaidi na pressure ya waandishi kumtaka aeleze kuhusu kashfa hizo...................
   
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  What is your source? kama kipo ina maana kwa hali ya sasa hata wanaharakati wameshindwa kweli kukipata na kukirusha hata youtube? i doubt it;
   
 3. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kipande gani mbona hatuelewi
   
 4. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowasa ni mwizi !!!!!!!!!!
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Sasa umesema nini hapa?
   
 6. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  ina maana lowasa hajui kuwa tido walishamtoa tbc?au anaamini hicho kipande cha interview tido aliondoka nacho?
   
 7. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haha ndio kazi uliyokuwa unaifanya kwenye lowasa great tour
   
 8. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  jamii forum tunaanza poteza imani na moderator, ukitoa post imayoeleza ukweli na uovu wa lowasa wanaichomoa hata haijasomwa, hadi sasa naona juhudi ni kumsafisha lowasa kupitia jamiiforums. ukitafakari hata thread hii unaona inalenga kuonyesha kuwa lowasa ni mzuri na dowans haimuhusu bali kuna watu wengine, lowasa kama anataka kutubu sisi hatuwezi kumzuia, ajifunze toba ya kweli toka kwa zakayo, sio suala la kusadikika kuwa lowasa ni fisadi na mwizi, atubu, arejeshe mali zetu na atakuwa mtu safi, si maneno ya kujitakasa, kujitakasa vitendo, hata uende kwa TB Joshua, Ben Hinn bila toba kama ya Zakayo imekula kwako, ilikuwaje uibe wakati una ndoto za kuwa prezoo, huoni mwizi mwenzio rostam kaamua bizness tuuuuuuuuuuuu. kuwa na Rais kama wewe ni laana, kwa nchi yetu, 1995 tu ulishaiba hadi mwalimu akakukataa. moderator hata hii ukipenda ifute maana naona kawanunua media zote, imagine mwizi magazeti yote hata ya wadau wa chadema yanaweka lead story yake kana kwamba ni shujaaa, hivi hata walioua Gadafi si waje wachukue hili jizi waende nalo!!!!!!!!!!!! kichefuchefu tu, ndo maana hata nywele nyeusi zimemkataa maana ni kinyaaa tu.
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Hebu tupe source ya haya maneno kwanza kabla hatujaanza kuchangia.
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Mwizi ni mwizi tu_hata akifanyaje hawezi kujisafisha kamwe.period
   
 11. F

  Fareed JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Lowassa fisadi tu, PCCB wangekuwa mashujaa wangempeleka mahakamani kwa tuhuma za rushwa za kuwa na utajiri usioweza kujieleza. Hii kesi kama kumsukuma mlevi tu mamvi Lowassa angetupwa jela kutokana na ufisadi wake uliokubuhu. Mafisadi wote kama kina Andrew Chenge, Rostam Aziz, Nazir Karamagi, nk wangeweza kukamatwa na sheria hii.
   
 12. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Mi sijui bana, lakini nakumbuka, nikiwa na akili zangu timamu na wala si kwa kusimuliwa-bali kwa kuona kwa macho yangu mawili. Nakumbuka vizuri kwamba, mara baada ya Lowasa kujiuzuru kufuatia kashfa ya Richmond; siku chache baadae Tirdo Mhando kweli akafanya mahojiano nae. nakumbuka vizuri wote walikuwa wamekaa kwenye viti wakitazamana uso kwa uso. Lakini katika hali ya kushangaza, mahojiano yalikatizwa ghafla na wala sio kwamba kuna kipande kiliondolewa!!!! Binafsi, nikahisi labda kuna tatizo la mawasiliano na huenda wangerudisha hewani mahojiano yale; lakin wapi na badala yake kikaja kipindi kingine kabisa!!! Sasa ni kwanini mahojiano yale yalikatizwa ghafla bila shaka ni Tirdo Mhando pekee ndie anayeweza kuelezea mkasa mzima. hata hivyo, Lowasa hana sababu ya kulilia mahojiano ambayo aliyafanya yeye mwenyewe na wala si kwa kuandikiwa. Alichokisema, anaweza hata leo kukisema na si lazima aseme kupitia Tido. Labda kama kuna drama ili ionekane Lowassa alitaka kuongea ukweli lakini ghafla akakatishwa na TBC1, manake kumbukumbu zangu zinaonesha kwamba hata Rostam Azizi nae alilalamika kutopewa nafasi ya kujieleza bungeni kuhusu kashfa hiyo. Na ni kweli, RA aliomba nafasi ya kujibu mapigo lakini Sitta akamnyima nafasi hiyo na hadi leo RA hajaongea alichotaka kuongea bungeni kana kwamba aliambiwa akiongea nje ya bunge angeuawa! Mazungumzo ya EL yalikatizwa ghafla na TBC na aliyotaka kuongea RA yalinyimwa nafasi na Spika Sitta.....sijui ni kweli walizuiwa ili wasiseme ukweli au ni usanii wa serikali wa kutaka kutonesha kwamba walitaka kuongea ukweli lakini wakanyimwa nafasi.
   
 13. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #13
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hii thread itabakia imefungwa hadi mhusika atakapotuthibitishia aunthetic source ya;
  • Lowasa alitoa demand hiyo lini?
  • Wapi?
  Pia tunawaasa members wetu kwamba tuwe na uhakika wa kile tunachotolea taarifa hapa jukwaani. Ifahamike kwamba jukwaa hili siyo sehemu ya hadithi za udakuzi na kufikirika zenye kusheheni ukiukwaji wa upashanaji habari.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...