Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,797
- 11,959
Cape Town: Mitambo ya kusukuma maji na kuyapeleka kwa watumaji itazimwa Aprili 29, mwaka huu na kuweka historia ya jiji hilo kukosa huduma hiyo muhimu.
Kuzimwa kwa mitambo hiyo kunakuja baada ya Cape Town na maeneo mengine Afrika Kusini kukabiliwa na ukame.
Takwimu zinaonesha ukame wa aina hii ulilikukba jiji hilo miaka 100 iliyopita.
Akizungumza jana, meya wa jiji hilo, Patricia de Lille alisema mitambo ya kusambaza maji itazimwa kuanzia tarehe hiyo, kwani haitakiwa na uwezo wa kuyasukuma kutokana na mabwaya kukosa maji.
Amewahimiza wakazi na wageni kujiandaa kuikabili hali hiyo mbaya kuwahi kutokea hivi karibuni.
Kila kona Cape Town kumesambaa mabango yenye matangazo ya kuhimiza matumizi mazuri, yenye kubana matumizi ya maji yasiyokuwa ya lazima.
Matangazo hayo yanahimiza kila mtu kutumia maji kidogo kadri imavyowezekana.
Jamiiforums jana ilishuhudia wamiliki wa hoteli na nyumba za wageni "wakihaha" kunusuru hali hiyo kwenye biashara zao.
Wamiliki hao walikuwa na kikao wakijadili namna bora ya kuhakikisha wanapata maji ya kutosha kwa wateja wao.
Moja ya maazimio waliyofikia ni kuagiza maji kwa wingi kutoka miji mingine na hata nje ya nchi, endapo hali itakuwa mbaya zaidi