Canada yaungana na Marekani na Uingereza kuelezea wasiwasi wao juu ya kuzorota kwa Haki za raia Nchini

Ubalozi wa Canada umesema unaungana na ubalozi wa Marekani na Uingereza katika kutilia wasiwasi wa uzorotaji wa utoaji haki nchini Tanzania.

Hawa wazungu sitaki kuwasikia
FB_IMG_1565760099253.jpeg
 
Kwani Erick Kabendera na wote wanaotetewa wanahusika vipi na acacia au barrick? Yaani nyie mtese na kunyanyasa watu, mkiambiwa mnakosea, mnakuja na mashairi yasiyokuwa na vina. Hacha ujinga chukua huo ushauri na mkome kuwanyanyasa watu kwa mambo yenu ya kijinga ya kutafuta sifa.
Yes,tutapata sifa kwa kuwa tunawatumikia wananchi na hatutacheka na nyani ng'o.Manyani yote yakae chonjo.
 
Pichani ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Tinde, Josephine Otieno (AMO) ambaye ameshurutishwa kupiga magoti na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, ili kumuomba msamaha Mbunge wa jimbo la Solwa, Ahmed Salim kwa niaba ya watumishi wa kituo chake ambao wanatuhumiwa kutoa lugha chafu za kashfa na matusi kwa wagonjwa.

KWA NINI NASEMA HUU NI UDHALILISHAJI?

DHAMBI moja haihalalilishi DHAMBI nyingine na wala kosa moja halihalalishi kosa lingine. Binafsi napinga na kulaani vitendo vya baadhi ya Watumishi wa afya kuwakashifu, kuwatukana na kuwadhalilisha wagonjwa. Vitendo hivi vinafaa kushughulikiwa na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria.

Watumishi wa afya wana mwajiri na mamlaka ya kinidhamu ya kuwashughulikia. Alichofanya huyu Mwenyekiti wa CCM ni udhalilishaji. Ameidhalilisha taaluma ya udaktari, amewadhalilisha Watumishi wa idara ya Afya, amemdhalilisha huyu mwanamke. Hii sio sawa hata kidogo.

Wanasiasa wa nchi hii wamejawa na kasumba ya ulimbukeni, kibri na dharau dhidi ya Watumishi wa umma. Hii si mara ya kwanza udhalilishaji kama huu kufanyika hadharani.

Nani hakumbuki tukio la Mkuu wa Wilaya kuamuru Walimu wacharazwe viboko hadharani na kweli Walimu kwa HOFU na UOGA wakasalimu amri na kucharazwa bakora tena mbele ya wanafunzi. Yule DC alifanywa nini? Hakuna!

Nani hakumbuki kitendo cha yule Diwani kule Tanga alivyomdhalilisha Mwalimu. Mwalimu kasaini kitabu cha mahudhurio saa 6.45 A.M. Diwani anamuuliza Mwalimu umeripoti kazini saa ngapi, Mwalimu kamjibu saa moja kasorobo. Diwani anamwambia Mwalimu wewe nakuona una kiburi na jeuri kwa nini unanidanganya wakati kwenye kitabu umesaini saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano. Anaanza kumtisha Mwalimu na kumuambia atatoa amri aondolewe kwenye halmashauri yake.

Nani hakumbuki sakata la udhalilishaji Ali Hapi aliomfanyia yule mama wa idara ya Ardhi, akimtisha tena mbele ya umma kwamba yeye ni mtu hatari sana. Hivi unategemea nini mfanyakazi anapotishwa na Mkuu wa mkoa?

Nani hakumbuki Bashite akiwatisha Walimu kuwa kama wangedhubutu kunyanyua mabango ya kudai nyongeza ya mshahara, kupandishwa madaraja na malimbikizo ya madeni yao angewacharaza viboko Walimu hadharani pale pale uwanjani. Yani mtu mwenye tuhuma za kufoji vyeti anapata ujasiri wa kuwatisha na kuwanyamazisha Walimu kwa sababu tu yeye ni mwana CCM mwenye madaraka ya uongozi. Kwake anaona taaluma za watu si chochote wala lolote.

Mambo mengi ya kitaaluma kwa sasa yanakabiliwa na shinikizo la wanasiasa wa CCM wanaotaka kumfurahisha mwenyekiti wao wa CCM.

Wafanyakazi wamebaki kama mayatima hakuna wa kuwasemea. Wamejawa HOFU na UOGA, kila mwanasiasa anayezuru eneo lao la kazi anakuja na vitisho na maagizo ya kipuuzi. Udhalilishwaji umekuwa sehemu ya maisha ya Wafanyakazi.

Hata kama tuhuma zilizotolewa ni za kweli. Tujiulize je Mwenyekiti wa CCM ndizo mamlaka za kinidhamu za kuwawajibisha Watumishi wa idara ya Afya?

Je adhabu ile ndio iliyoainisha kwenye kanuni za utumishi wa umma? Kwamba washurutishwe kupiga magoti kwenye mkutano wa hadhara wa CCM na kuomba msamaha?

Hivi Wafanyakazi wa nchi hii wameikosea nini serikali hii ya CCM? Kuwapandisha mishahara na madaraja imeshindikana wamekaa kimya wameamua kufa kwa njaa kimya kimya kama wafuasi wa Kibwetere. Hiyo haitoshi bado mnaamua kuwadhalilisha kwa nini?

Maeneo mengine Walimu wanashurutishwa kufundisha hadi weekend, hakuna likizo. Naibu Waziri anasema amesitisha uhamisho mwalimu asijisumbue kuomba uhamisho. Hii maana yake nini?

NANI WA KULAUMIWA?

Wa kwanza anayestahili kidole cha lawama ni hivi vyama vya Wafanyakazi. Tuna vyama vya Wafanyakazi vya hovyo haijawahi kutokea Duniani. Madaktari na wauguzi wanadhalilishwa chama cha Madaktari na kile cha Watumishi wa afya kipo kipo tu. Walimu wanacharazwa bakora hadharani, chama cha Walimu (CWT) kipo tu kinakula asilimia za mishahara ya Walimu kila mwezi.

Pili ni serikali ya CCM. Wanasiasa wa CCM Mpya wanadharau na kupuuza taaluma za watu. Yani Diwani au Mwenyekiti wa CCM ambaye anajua tu kusoma na kuandika kwa tabu ana ujasiri, dharau na kiburi cha kudhubutu kumdhalilisha Mwalimu, Daktari, Muuguzi, Injinia au Muhasibu mwenye vyeti vyake. Huu ni upuuzi ambao ukifumbiwa macho siasa itazidi kuangamiza elimu, idara ya afya n.k. Tujifunze kuheshimu taaluma za watu. Penye makosa watu wawajibishwe na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria, taratibu na kanuni. Acheni mizuka, nchi hii mnaipeleka korongoni kwa sababu mnaendesha nchi kwa mizuka. Lazima kuwe na clear line inayotenganisha mpaka wa siasa na taaluma.

Mwisho nimnyooshee kidole cha lawama huyu Daktari na Watumishi wengine wengi wanaokubali kuweka kando taaluma zao na kudhalilishwa na wanasiasa hawa uchwara. Wafanyakazi mna haki zenu, zipo Sheria za kuwalinda acheni kujidhalilisha, kataeni kudhalilishwa. Hivi kwani huyu Daktari angedinda kupiga magoti hapo huyo Mwenyekiti wa CCM angemfanya nini? Ana jeuri ya kumfuta kazi kwa Sheria ipi na kwa mamlaka gani?

Aidha nanyi ndugu zetu baadhi ya Madaktari, wauguzi n.k. Chonde chonde kazi hii ni wito tunapokuja hospitalini hebu kuweni na UTU, hekima, adabu na busara. Wapo Watumishi wa afya wanaofanya kazi hii kwa weledi, wito, hekima na upendo mkubwa. Lakini baadhi yenu hata mgonjwa usipokuwa na uvumilivu unaweza ukamchapa nesi makofi, mnakuwa na kiburi na dharau utadhani mmelazimishiwa kazi. Badilikeni hii kazi ni zaidi ya utume.

Nanyi wanasiasa kama mwanataaluma anatuhumiwa, mpelekeni kwenye mamlaka za kinidhamu kwa kuzingatia taratibu, Sheria na kanuni akawajibishwe kwa mujibu wa Sheria pasipo kudhalilishwa.
Mkuu huko vizuri. Tanzania inaharibiwa na wanasiasa. Niliona bashiru, katibu ccm akibwabwaja siku moja pale udsm, eti anawaambia endapo hata lecturer yeyote atakuwa na tatizo katika ufundishaji basi wamwambie yeye waone kama ataendelea kuwepo pale kama mwalimu wa chuo. Nikajiuliza sasa katibu wa ccm, na uwajibishwaji wa mtaaluma wa chuo kikuu wapi na wapi? Inamaana kila kitu kwa sasa hapa nchini ni siasa tu.
Hilo la wauguzi na ma-medical Drs, siyo kwamba nawatetea ila kiujumla, sehemu nyingi Tanzania huduma siyo nzuri lakini huko kwenye afya malalamiko yanakuwa mengi kwa sababu ya unyeti wa kazi yenyewe. Ila tukumbuke, manesi na madokta ni watu walewale sawa na wale wanasumbua kule mfano nida kwenye vitamburisho vya taifa au uhamiji kwenye utoaji wa passport. Na pia hawana hata amasa ya kazi, kama mwajili anaona hamna haja ya kupandisha vyeo na kuongeza mshahara hivyo hivyo na mfanyakazi haoni umuhimu wa kupandisha ubora na ufanisi wa huduma anayotoa, tusilaumiane pasipo sababu za msingi.
 
Yes,tutapata sifa kwa kuwa tunawatumikia wananchi na hatutacheka na nyani ng'o.Manyani yote yakae chonjo.
Wewe ndiyo nyani nambar one. Uliishia darasa la ngapi? Rudi shule elimu haina mwisho maana hujui hata kuandika, unajikanyaga. Utakuwa mlamba viatu wewe.
 
Wewe ndiyo nyani nambar one. Uliishia darasa la ngapi? Rudi shule elimu haina mwisho maana hujui hata kuandika, unajikanyaga. Utakuwa mlamba viatu wewe.
Ndo wasomi wa nchi hii hao kaka;kwa staili hii ndo watu wanamsingizia mzungu matatizo ya bongo?nimeanza kumwelewa Trump kwa nn anatudharau waafrika sababu Mambo yetu ni ya hovyohovyo
 
Ndo wasomi wa nchi hii hao kaka;kwa staili hii ndo watu wanamsingizia mzungu matatizo ya bongo?nimeanza kumwelewa Trump kwa nn anatudharau waafrika sababu Mambo yetu ni ya hovyohovyo
Manufaa ya mtu sio kwenda tu shule na kupata elimu;manake upate elimu na uelimike otherwise ni bure.
 
Usitulishe matangopori,njoo na real data utueleze contribution ya madini yetu kwenye uchumi wao;Obama alishwaulizwa swali Ghana alipoitembelea Africa kuhusu nchi za magharibi hasa marekani zinavyoinyonya Africa kibiashara;ilibidi Obama ashangae,na akasema kwa data kabisa kwamba biashara inayofanywa na wao na Africa ni ndogo mnoo mnoo na haina mchango wa maana kwenye chumi zao;wao wanafanya biashara sana Asia na hata ukiangalia bidhaa za wazungu tu bongo ni za kuhesabu;hata kama tunalalamika kunyonywa bora uwataje wachina manake ndo tunapigana nao vikumbo mpaka kariakoo
Hii pointi nimeilewa sana
 
Manufaa ya mtu sio kwenda tu shule na kupata elimu;manake upate elimu na uelimike otherwise ni bure.
Huko sahihi kabisa, maana ya elimu ndiyo hii uliyoitoa. Kuna baadhi wanaenda shule kutafuta vyeti na siyo elimu. Tena wengine mfano akina palamagamba kabudi, kitila mkumbo, n.k wana vyeti vingi kweli kweli lakini hawajaelimika hata kidogo. Kipimo kimojawapo cha kuelimika ni kuwa na msimamo wa mambo unayoyaamini. Siyo leo ukiwa mwalimu pale udsm unasema hivi, kesho ukishateuliwa kuwa mlamba miguu kwa kacheo ka kupewa na wenye viatu unasema tofauti kabisa na uliyosema jana. Watu wa aina hii hawajaelimika bali wana vyeti tu kuonyesha kwamba walipita shuleni/vyuoni.
 
Acheni ujinga ,hizi nchi zote mboa nazo zina matatizo kuhusu haki za kibinadamu kuliko hata Tazania au nyie mnaishi Kandahar kiasi kwamba hamjui dhuluma na ubaguzi au ukosefu wa haki za binadamu za nchi hizi,nadhani mumekuwa mazwazwa hata kusoma au kuangalia matukio ya habari duniani hamuangalia,na pia nadhani wengi wenu ufahamu wa mambo ya kisiasa,kiuchumi na kitamaduni ya ulimwengu huu ,uelewa wenu ni sifuri,au mumesahau raisi wa Marekani anavyowafanya 'watu wa rangi' huko Marekani? au Canada walivyomfunga mtoto wa mmiliki wa kampuni ya Huawei kwa hutuma kama za akina Kabendera,je mnajua kwanini Marekani inaipiga vita Huawei au ni kwanini Marekani imezitisha nchi na mashirika yote nayotoa tahadhari kwa raia /wafanyakazi wake kuwa wasisende Marekani kutokana na Marekani kutokuwa salama?Nchi yangu Tanzania kwanza ,ujinga mwingine hukoo,na ndio maana hata raisi wa Marekani anasema nchi yake kwanza ujinga mwingine huko.
 
These are facts;-
Firstly,Meng Wanzhou ( Huawei CFO ) anasubiria kuwa extradited from Canada to US Ili aweze kujibu mashtaka ya kukwepa vikwazo vya Marekani juu ya Iran;na sehemu ya vikwazo hv ukiachilia vilivyowekwa na marekani vingine ni vya UN;hvyo suala la kusema Meng kafungwa ni porojo na kuonyesha kutokuelewa kwako Mambo,Uhalisia ni kwamba Meng yupo kizuizini Canada akisubiria taratibu za kisheria Ili apelekwe Us kujibu tuhuma.
Secondly,Swala la haki ya umiliki bunduki US linalindwa na katiba hao yaani Second Amendment rights ambayo ilipitishwa na wananchi wao wenyewe.
Thirdly;Marekani anaipinga huawei sababu ni Arm ya serikali ya china katika kushiriki ujasusi;wanatengeneza back door kwenye software zao Ili serikali ya china iweze kuiba technology na taarifa muhimu;Huawei walipewa contract ya kujenga mifumo ya mawasiliano ya jengo la AU addis Abbaba ambapo server zikagunduliwa zinatuma taarifa China baada ya kupewa intelligence na Israel,pia makampuni ya watu wa china wanabanwa na policy ya gvt yao kuweza kutuma taarifa za kijasusi nyumbani;Maafisa wengi wa Huawei wengi wameajiriwa na PLA(People liberation Army);China wameshikwa wa ki hack india kupitia ZTE,maofisa wa huawei wameshikwa Poland kwa kijasusi huku ni wafanyakazi wake and etc.So be well informed usiwadanganye wasiojua
 
"
But in January 2018, French newspaper Le Monde Afrique dropped a bombshell.
It reported that the AU’s computer system had been compromised.
The newspaper, citing multiple sources, said that for five years, between the hours of midnight and 0200, data from the AU’s servers was transferred more than 8,000km away - to servers in Shanghai.
This had allegedly continued for 1,825 days in a row.
Le Monde Afrique reported that it had come to light in 2017, when a conscientious scientist working for the AU recorded an unusually high amount of computer activity on its servers during hours when the offices would have been deserted.
It was also reported that microphones and listening devices had been discovered in the walls and desks of the building, following a sweep for bugs"From BBC
 
Uzuri hawajaanza leo na matamko yao, hawawezi kufanya lolote sababu Watanzania wamesimama imara na Rais wao kwa hiyo hizi kelele zao mwisho buza tu. Mawimbi ya infrared
Subiri wastop kutoa ARV ndio akiri zitawakaa sawa
 
Vodacom ni ya mchepuko wako? (unajua inaingiza kiasi gani?)
Internet?
Petrol nayo?
Mikopo ya world Bank, IMF na creditors wengine?
Madawa karibu 95% ya hospitals?
Mbegu, mbolea, pembe jeo za kilimo katibu zote?
Pamba, dhahabu, tumbaku, korosho, ufuta, chai, Kahawa, almasi, makinikia?
Spears za vyombo vya usafiri vya aina zote?
Bidhaa za electronics?
Makampuni ya kihandisi?
Hapo ni India , Singapore na China mzee achilia mbali Uarabuni. Kajipange upya
 
Wazungu wakati mwingine huingilia kati kutusaidia, Hata serikali ya mwalimu Nyerere kama siyo Muingereza kuingilia kati kuinusuru mwaka 1964 kwa kuleta makomandoo kuzima jaribio lile la mapinduzi la akina Kamanda Ilogi sasa hivi huenda CCM insingelikuwa madarakani!.

Maana kama Muingereza aliinusuru serikali ya TANU ising'olewe, hawa vijana wa CCM ya leo wanaowatukana wazungu kwa kuwaita Mabeberu wajue tu Baba wa chama chao yaani TANU ilinusuriwa na Beberu muingereza!. La sivyo wasingekuwepo hapa wanapayuka eti "CCM itatawala milele" thubutu!, Nendeni mkamshukuru kwanza beberu Muingereza kwa kuwanusuru!
Nadhani hawasomi historia hawa watanzania
 
Back
Top Bottom