Canada yaungana na Marekani na Uingereza kuelezea wasiwasi wao juu ya kuzorota kwa Haki za raia Nchini

Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
37,161
Points
2,000
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
37,161 2,000
Nasikia ni ya korosho, ila sijajua aligundua korosho inafanyaje, na inakuwaje baada ya hiyo korosho kufanya hivyo?
Maganda ya korosho yanazuia kutu lakini machapisho yake huwezi kuisoma popote pale duniani.
 
Emery Paper

Emery Paper

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2019
Messages
448
Points
500
Emery Paper

Emery Paper

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2019
448 500
Ndo kusema hawataki tena kutuuzia Bombardier ?. Sema watakuwa wamesahau kuwa sisi ni Donor Country.
 
M

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Messages
3,583
Points
2,000
M

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2018
3,583 2,000
Haya mataifa yamebanwa kwa sababu yalikuwa na national interests zao hapa kwetu Tanzania,sijawahi kusikia wakibwabwaja kwenye mataifa yasio na rasilmali kama za kwetu mfano Burundi ambapo jamaa kabadili katiba na hakuna mtu kumtoa Rais Kurunziza,Uingereza,Marekani,Norway,Canada wote hao wana makampuni ya utafiti na uchimbaji wa Mafuta ,gas na Madini hapa kwetu Tanzania ambayo yote baba JPM kapiga PIN
Watu kama wewe ndio mnaotutukanisha na kusababisha Watanzania wote tuonekane kuwa hatuna akili.
 
Allency

Allency

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,529
Points
2,000
Allency

Allency

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,529 2,000
Uzuri hawajaanza leo na matamko yao, hawawezi kufanya lolote sababu Watanzania wamesimama imara na Rais wao kwa hiyo hizi kelele zao mwisho buza tu. Mawimbi ya infrared
Kwanin lumumba mnapenda kusemea nafsi za wengine, mimi binafsi siko na jiwe, na wewe sema wewe binafsi uko naye
 
kirumbiu

kirumbiu

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2016
Messages
223
Points
250
kirumbiu

kirumbiu

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2016
223 250
Watoto wa 2000 watajulia wapi hayo, wao waulize historia ya Diamond Platinumz watakwambia hadi babu yake na babu wa Diamond alikuwa na wake wangapi.
Umesahau na mkeka na simba na yanga bongo zao ndizo zimejaa
 
Allency

Allency

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,529
Points
2,000
Allency

Allency

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,529 2,000
Ukiona mtu ana PhD alaf ataki kukosolewa ujue hata PhD yake ni fake. All genuine PhD holders are always open to new ideas and constructive criticism. Huyu wa kwako hataki kabisa hayo makitu. Angekuwa kasoma kwa wenzetu, PhD yake wangekuwa wameisha ifukunyua. Huku kwetu alijaribu kidogo Ben kuoji uhalali wa jamaa kumaliza PhD ndani ya miaka mitatu kasoro pamoja majukumu ya uwaziri juu. Wakati huo other fulltime students wasiokuwa na majukumu wanaoshinda maabara wakitafiti pale UDSM, wengi wao wanakata 6-7 yrs kikiwa hakijaeleweka. Masikini sijui kapotelea wapi Ben, angetusaidia sana kuifukunyua hii PhD ya huyu jamaa. Kuna watu wamejipa u-mungu hapa duniani wanawapoteza wenzao as if wao wataishi milele. Hacha tukae kimya maana hawakawii kutunyamazisha wote hawa jamaa awataki kabisa kuongelea PhD zao.
PhD fake
 
Lizarazu

Lizarazu

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2015
Messages
4,508
Points
2,000
Lizarazu

Lizarazu

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2015
4,508 2,000
Naona siku hizi zile kauli za uchochezi zimepotea!!

maana wanaozitamka si wachochezi wa siku zote.

Acha tu wachozi wa nje waendelee kutusemea!
 
J

John7371

Member
Joined
Apr 29, 2018
Messages
38
Points
125
J

John7371

Member
Joined Apr 29, 2018
38 125
Mbumbumbu huwa hawajui hii kitu japo wapo wanaojua na kujifanya hawajui kwa interests za kisiasa, biashara zetu(Africa) na developed countries zina impact ndogo sana kwenye uchumi wao.
WASHINGTON (Reuters) - U.S. President Barack Obama on Monday gave a preview of a summit he will hold with African leaders next week, saying African nations should look inward for solutions to economic woes and not make "excuses" based on a history of dependence and colonization.
"At some point, we have to stop looking somewhere else for solutions, and you have to start looking for solutions internally," Obama told the enthusiastic audience.
“And as powerful as history is, and you need to know that history, at some point, you have to look to the future and say, ‘OK, we didn’t get a good deal then, but let’s make sure that we’re not making excuses for not going forward.’"

Obama’s remarks amounted to a rejection of comments last month from Equatorial Guinea President Teodoro Obiang Nguema, who said Western "neo-colonial" domination of Africa has impeded the continent’s development. Nguema blasted what he said were too-low exchange rates, problems with natural resources’ pricing and Western-imposed “barriers to international trade” at a summit of the 54-nation African Union.

Obama said there was not a “single country” in Africa that could not be doing better with the resources it had.

"There are a lot of countries that are generating a lot of income, have a lot of natural resources, but aren’t putting that money back into villages to educate children. There are a lot of countries where the leaders have a lot of resources, but the money is not going back to provide health clinics for young mothers," he said.

Nashukuru sana kwa kumwelimisha
 
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2015
Messages
4,703
Points
2,000
Waziri wa Kaskazini

Waziri wa Kaskazini

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2015
4,703 2,000
Magufuli piga marufuku wasomi wa Canada kuja kuchukua degree zao kwenye vyuo vyetu hapa nchi!!!!
 
Qwy

Qwy

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2018
Messages
1,147
Points
2,000
Qwy

Qwy

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2018
1,147 2,000
.
Pichani ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Tinde, Josephine Otieno (AMO) ambaye ameshurutishwa kupiga magoti na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mabala Mlolwa, ili kumuomba msamaha Mbunge wa jimbo la Solwa, Ahmed Salim kwa niaba ya watumishi wa kituo chake ambao wanatuhumiwa kutoa lugha chafu za kashfa na matusi kwa wagonjwa.

KWA NINI NASEMA HUU NI UDHALILISHAJI?

DHAMBI moja haihalalilishi DHAMBI nyingine na wala kosa moja halihalalishi kosa lingine. Binafsi napinga na kulaani vitendo vya baadhi ya Watumishi wa afya kuwakashifu, kuwatukana na kuwadhalilisha wagonjwa. Vitendo hivi vinafaa kushughulikiwa na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria.

Watumishi wa afya wana mwajiri na mamlaka ya kinidhamu ya kuwashughulikia. Alichofanya huyu Mwenyekiti wa CCM ni udhalilishaji. Ameidhalilisha taaluma ya udaktari, amewadhalilisha Watumishi wa idara ya Afya, amemdhalilisha huyu mwanamke. Hii sio sawa hata kidogo.

Wanasiasa wa nchi hii wamejawa na kasumba ya ulimbukeni, kibri na dharau dhidi ya Watumishi wa umma. Hii si mara ya kwanza udhalilishaji kama huu kufanyika hadharani.

Nani hakumbuki tukio la Mkuu wa Wilaya kuamuru Walimu wacharazwe viboko hadharani na kweli Walimu kwa HOFU na UOGA wakasalimu amri na kucharazwa bakora tena mbele ya wanafunzi. Yule DC alifanywa nini? Hakuna!

Nani hakumbuki kitendo cha yule Diwani kule Tanga alivyomdhalilisha Mwalimu. Mwalimu kasaini kitabu cha mahudhurio saa 6.45 A.M. Diwani anamuuliza Mwalimu umeripoti kazini saa ngapi, Mwalimu kamjibu saa moja kasorobo. Diwani anamwambia Mwalimu wewe nakuona una kiburi na jeuri kwa nini unanidanganya wakati kwenye kitabu umesaini saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano. Anaanza kumtisha Mwalimu na kumuambia atatoa amri aondolewe kwenye halmashauri yake.

Nani hakumbuki sakata la udhalilishaji Ali Hapi aliomfanyia yule mama wa idara ya Ardhi, akimtisha tena mbele ya umma kwamba yeye ni mtu hatari sana. Hivi unategemea nini mfanyakazi anapotishwa na Mkuu wa mkoa?

Nani hakumbuki Bashite akiwatisha Walimu kuwa kama wangedhubutu kunyanyua mabango ya kudai nyongeza ya mshahara, kupandishwa madaraja na malimbikizo ya madeni yao angewacharaza viboko Walimu hadharani pale pale uwanjani. Yani mtu mwenye tuhuma za kufoji vyeti anapata ujasiri wa kuwatisha na kuwanyamazisha Walimu kwa sababu tu yeye ni mwana CCM mwenye madaraka ya uongozi. Kwake anaona taaluma za watu si chochote wala lolote.

Mambo mengi ya kitaaluma kwa sasa yanakabiliwa na shinikizo la wanasiasa wa CCM wanaotaka kumfurahisha mwenyekiti wao wa CCM.

Wafanyakazi wamebaki kama mayatima hakuna wa kuwasemea. Wamejawa HOFU na UOGA, kila mwanasiasa anayezuru eneo lao la kazi anakuja na vitisho na maagizo ya kipuuzi. Udhalilishwaji umekuwa sehemu ya maisha ya Wafanyakazi.

Hata kama tuhuma zilizotolewa ni za kweli. Tujiulize je Mwenyekiti wa CCM ndizo mamlaka za kinidhamu za kuwawajibisha Watumishi wa idara ya Afya?

Je adhabu ile ndio iliyoainisha kwenye kanuni za utumishi wa umma? Kwamba washurutishwe kupiga magoti kwenye mkutano wa hadhara wa CCM na kuomba msamaha?

Hivi Wafanyakazi wa nchi hii wameikosea nini serikali hii ya CCM? Kuwapandisha mishahara na madaraja imeshindikana wamekaa kimya wameamua kufa kwa njaa kimya kimya kama wafuasi wa Kibwetere. Hiyo haitoshi bado mnaamua kuwadhalilisha kwa nini?

Maeneo mengine Walimu wanashurutishwa kufundisha hadi weekend, hakuna likizo. Naibu Waziri anasema amesitisha uhamisho mwalimu asijisumbue kuomba uhamisho. Hii maana yake nini?

NANI WA KULAUMIWA?

Wa kwanza anayestahili kidole cha lawama ni hivi vyama vya Wafanyakazi. Tuna vyama vya Wafanyakazi vya hovyo haijawahi kutokea Duniani. Madaktari na wauguzi wanadhalilishwa chama cha Madaktari na kile cha Watumishi wa afya kipo kipo tu. Walimu wanacharazwa bakora hadharani, chama cha Walimu (CWT) kipo tu kinakula asilimia za mishahara ya Walimu kila mwezi.

Pili ni serikali ya CCM. Wanasiasa wa CCM Mpya wanadharau na kupuuza taaluma za watu. Yani Diwani au Mwenyekiti wa CCM ambaye anajua tu kusoma na kuandika kwa tabu ana ujasiri, dharau na kiburi cha kudhubutu kumdhalilisha Mwalimu, Daktari, Muuguzi, Injinia au Muhasibu mwenye vyeti vyake. Huu ni upuuzi ambao ukifumbiwa macho siasa itazidi kuangamiza elimu, idara ya afya n.k. Tujifunze kuheshimu taaluma za watu. Penye makosa watu wawajibishwe na mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria, taratibu na kanuni. Acheni mizuka, nchi hii mnaipeleka korongoni kwa sababu mnaendesha nchi kwa mizuka. Lazima kuwe na clear line inayotenganisha mpaka wa siasa na taaluma.

Mwisho nimnyooshee kidole cha lawama huyu Daktari na Watumishi wengine wengi wanaokubali kuweka kando taaluma zao na kudhalilishwa na wanasiasa hawa uchwara. Wafanyakazi mna haki zenu, zipo Sheria za kuwalinda acheni kujidhalilisha, kataeni kudhalilishwa. Hivi kwani huyu Daktari angedinda kupiga magoti hapo huyo Mwenyekiti wa CCM angemfanya nini? Ana jeuri ya kumfuta kazi kwa Sheria ipi na kwa mamlaka gani?

Aidha nanyi ndugu zetu baadhi ya Madaktari, wauguzi n.k. Chonde chonde kazi hii ni wito tunapokuja hospitalini hebu kuweni na UTU, hekima, adabu na busara. Wapo Watumishi wa afya wanaofanya kazi hii kwa weledi, wito, hekima na upendo mkubwa. Lakini baadhi yenu hata mgonjwa usipokuwa na uvumilivu unaweza ukamchapa nesi makofi, mnakuwa na kiburi na dharau utadhani mmelazimishiwa kazi. Badilikeni hii kazi ni zaidi ya utume.

Nanyi wanasiasa kama mwanataaluma anatuhumiwa, mpelekeni kwenye mamlaka za kinidhamu kwa kuzingatia taratibu, Sheria na kanuni akawajibishwe kwa mujibu wa Sheria pasipo kudhalilishwa.
 

Forum statistics

Threads 1,326,245
Members 509,448
Posts 32,215,659
Top