Kaparo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 1,997
- 4,827
Kutokana na forensic science niliyoipitia,Kama ya tukio hili hapa chini kwenye youtube:
Jamaa aliondoka kwenye crime scene na jani la mti lilidondokea kwenye cabin ya pick-up yake. Na hili wanakiri kuwa ni tukio ambalo kwa mara ya kwanza DNA ya mti ilitumika kama ushahidi mahakamani na kumtia hatiani mtuhumiwa. Kabla ya hapo, DNA ya mti ilikuwa haijawahi kutumika, isipokuwa ya binadamu tu. Hawa jamaa huwa wanatumia akili kubwa hadi huwa inanipa maumivu mwilini nikianza kufikiria wanavyofanya kazi! Acha kabisa
Kuna case study moja niliicheki jamaa alifanya mauaji ya mwanamke na kwenda kumtupa kwenye majalala huko eneo jingine.
E.g Kwa mkoa wa mara tarime ina ardhi tofauti na Musoma Manispaa,
Hivyo katika uchunguzi wa gari ulipofanyika kwa suspect wa mauaji alikutwa katika gari lake tyres zina udongo (soil sample tofauti na ya eneo husika)
Katika soil sample analysis (evidence) iliyofanyika kwenye eneo la mauaji ili match na ile iliyoko kwenye tyres za gari lililokamatwa la suspect. Hapa unaona hata udongo pia unaweza kutumika..
- Kuna trace evidences kama hair,blood stain, saliva n.k