Camouflagers na informers

KISWAHILI ni wazugaji na wafichua habari
Ni watu maalum lakini wa kila jinsia umri na kaliba... Kati yao wapo mpaka wezi matapeli, wakabaji na wachawi.. Lakini kila walipo wapo kwa lengo maalum.... Kutoa taarifa ambazo zitasaidia kubaini waovu na kuzuia hatari ama kulinda usalama wa nchi raia ama viongozi....
Hawa watu hutumika kwa namna tatu
1. Kutoa taarifa muhimu za kihalifu zinazosaidia kuepusha janga fulani katika jamii... Iwe la kiongozi ama jumuiya
2.Hutumika kuwajenga viongozi na propaganda za kukubalika kwa kiongozi fulani katika jamii
3. Hutumika wakati wa hatari ya usalama wa nchi,mipango ya mauaji ya viongozi, mapinduzi ya kijeshi, maandamano migomo nk
Ni aina ya watu wenye elimu na waliopewa mafunzo maalum juu na namna ya kuvaa uhusika fulani bila kujulikana, namna ya kuongea, kuripoti na kutoweka eneo la tukio bila kuacha alama yoyote na kujulikana uhalisia....

Mfano wa kwanza
Kiongozi mkubwa anapotaka kutembelea eneo fulani, wazugaji na watoa taarifa za siri hufika wiki moja ama zaidi kabla ya ziara rasmi... Hapa hujigawa katika makundi mawili
. kundi la kwanza ni la kusoma hali ya hewa kiusalama na kukubalika kwa kiongozi.. Mambo mabaya yanayotendwa na viongozi wa eneo husika na maoni ya wadau
. kundi la pili ni wazugaji. Hawa ni wana kitengo cha propaganda ili kuonyesha kukubalika, kuaminika na kuungwa mkono kwa kiongozi na imani juu ya wale aliowatembelea.. Hapa si ajabu kumkuta kiongozi anakula chakula mtaani kwenye banda fulani bila hofu, kunywa kinywaji kama dafu ama kula kitu kama karanga tunda nk... Wauzaji wa vitu vyote hivi ni watumishi wake waaminifu

Mfano wa pili
Nchi inapopitia kipindi cha mashaka kama maandamano usaliti na mapinduzi..
Hapa huangaliwa kwanza maeneo yenye ushawishi mkubwa wa jambo husika.... Ndipo hupelekwa timu ya watu maalum!! Mfano anafika mtu wa kawaida kwenye bar ya kawaida mtaani, ambapo pembezoni kuna kijiwe na bodaboda nk.. Huyu aliyeko bar anakuwa busy na simu na kinywaji chake... Hana story na mtu... Kisha anakuja mwingine mzugaji kama machinga, anajifanya anauza keyholders kwa bei poa sana na kama huna hela anakukopesha...
Bila kujua zile keyholders zina mawasiliano ya moja kwa moja na jamaa aliyeko pale bar

Mfano wa tatu
Hatari ya kuvamiwa kijeshi... Hapa ni pakubwa na penye mengi lakini wanawake warembo hutumika sana kipindi hiki... N kundi lingine ni wazugaji wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa na watafiti wanaotaka kuwekeza ama kutafiti....
Yote kwa yote jihadhari sana na mikusanyiko yenye dhumuni la maandamano hasa ya kisiasa ama kupinga jambo fulani kitaifa... Ukiachana na wale askari wa fanya fujo uone wenye mabomu ya machozi na risasi za mpira, huwa kuna mdunguaji mmoja tu hatari sana kwa ajili ya kumdungua kiongozi ama walio mstari wa mbele... Kimbia jifiche....

Unaposikia kiongozi kafika mahali na watu fulani wamewajibishwa kwa haki, tambua wazi ni kazi iliyotukuka ya wazugaji na wafichua habari
Unaposikia maandamano, mgomo ama mapinduzi fulani yameshindikana jua fika kwamba kuna kazi kubwa imefanywa na hawa jamaa
ILA unapoona mojawapo kati ya hayo niliyotaja yamefanikiwa vizuri, basi hawa jamaa ama wamefeli ama wanekengeuka miiko yao..!
Kamwe usiwaamini hawa watu hata kama ni ndugu yako... HAWATABIRIKI...!

Jr
 
Kaka Mshana hivi unaweza eleza chochote kuhudu rais Nkurunziza wa Burundi aliponusulika na kupinduliwa nini kilifanya zoezi lile lililopangwa kwa msaada wa kagame ( inasemekana ) ku '' fail ''
je ni kweli kama inavyosemekana kua TISS ndio walio okoa jahazi na kumrudisha Pierre Bujumbura?

Na kama ni kweli walihusika ni kwa faida ipi?
Ukinijibu i ll feel proudly
 
LOVE U JF... Hilo ni jambo ambalo lilihusu mataifa mengine na sisi tukahusishwa (pengine) kwa kiasi fulani sina hakika sana na hili... Lakini hata kama ingekuwa ni kweli ni ngumu habari kama hizi kuandikwa kwenye open forum mpaka upite muda mrefu sana
 
Always rais akienda sehemu halafu akapiga picha,wale waliopo pembeni yake huwa sio RAIA wa kawaida..ingawa macho ya watu wataona ni raia tu,lakini sio.
Hata huyo muuza bangi ni walewale tu
 
Binadamu unafanya yooote hayo upo zako bafuni unaanguka unapalarazi unakuwa kitandani wanakubadikisha pampers tu.
KISWAHILI ni wazugaji na wafichua habari
Ni watu maalum lakini wa kila jinsia umri na kaliba... Kati yao wapo mpaka wezi matapeli, wakabaji na wachawi.. Lakini kila walipo wapo kwa lengo maalum.... Kutoa taarifa ambazo zitasaidia kubaini waovu na kuzuia hatari ama kulinda usalama wa nchi raia ama viongozi....
Hawa watu hutumika kwa namna tatu
1. Kutoa taarifa muhimu za kihalifu zinazosaidia kuepusha janga fulani katika jamii... Iwe la kiongozi ama jumuiya
2.Hutumika kuwajenga viongozi na propaganda za kukubalika kwa kiongozi fulani katika jamii
3. Hutumika wakati wa hatari ya usalama wa nchi,mipango ya mauaji ya viongozi, mapinduzi ya kijeshi, maandamano migomo nk
Ni aina ya watu wenye elimu na waliopewa mafunzo maalum juu na namna ya kuvaa uhusika fulani bila kujulikana, namna ya kuongea, kuripoti na kutoweka eneo la tukio bila kuacha alama yoyote na kujulikana uhalisia....

Mfano wa kwanza
Kiongozi mkubwa anapotaka kutembelea eneo fulani, wazugaji na watoa taarifa za siri hufika wiki moja ama zaidi kabla ya ziara rasmi... Hapa hujigawa katika makundi mawili
. kundi la kwanza ni la kusoma hali ya hewa kiusalama na kukubalika kwa kiongozi.. Mambo mabaya yanayotendwa na viongozi wa eneo husika na maoni ya wadau
. kundi la pili ni wazugaji. Hawa ni wana kitengo cha propaganda ili kuonyesha kukubalika, kuaminika na kuungwa mkono kwa kiongozi na imani juu ya wale aliowatembelea.. Hapa si ajabu kumkuta kiongozi anakula chakula mtaani kwenye banda fulani bila hofu, kunywa kinywaji kama dafu ama kula kitu kama karanga tunda nk... Wauzaji wa vitu vyote hivi ni watumishi wake waaminifu

Mfano wa pili
Nchi inapopitia kipindi cha mashaka kama maandamano usaliti na mapinduzi..
Hapa huangaliwa kwanza maeneo yenye ushawishi mkubwa wa jambo husika.... Ndipo hupelekwa timu ya watu maalum!! Mfano anafika mtu wa kawaida kwenye bar ya kawaida mtaani, ambapo pembezoni kuna kijiwe na bodaboda nk.. Huyu aliyeko bar anakuwa busy na simu na kinywaji chake... Hana story na mtu... Kisha anakuja mwingine mzugaji kama machinga, anajifanya anauza keyholders kwa bei poa sana na kama huna hela anakukopesha...
Bila kujua zile keyholders zina mawasiliano ya moja kwa moja na jamaa aliyeko pale bar

Mfano wa tatu
Hatari ya kuvamiwa kijeshi... Hapa ni pakubwa na penye mengi lakini wanawake warembo hutumika sana kipindi hiki... N kundi lingine ni wazugaji wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa na watafiti wanaotaka kuwekeza ama kutafiti....
Yote kwa yote jihadhari sana na mikusanyiko yenye dhumuni la maandamano hasa ya kisiasa ama kupinga jambo fulani kitaifa... Ukiachana na wale askari wa fanya fujo uone wenye mabomu ya machozi na risasi za mpira, huwa kuna mdunguaji mmoja tu hatari sana kwa ajili ya kumdungua kiongozi ama walio mstari wa mbele... Kimbia jifiche....

Unaposikia kiongozi kafika mahali na watu fulani wamewajibishwa kwa haki, tambua wazi ni kazi iliyotukuka ya wazugaji na wafichua habari
Unaposikia maandamano, mgomo ama mapinduzi fulani yameshindikana jua fika kwamba kuna kazi kubwa imefanywa na hawa jamaa
ILA unapoona mojawapo kati ya hayo niliyotaja yamefanikiwa vizuri, basi hawa jamaa ama wamefeli ama wanekengeuka miiko yao..!
Kamwe usiwaamini hawa watu hata kama ni ndugu yako... HAWATABIRIKI...!

Jr
 
Kama ni wanaridhaa(amateurs) wataacha alama ila kama ni wajuzi (professionals) kutrace alama zao ni kazi moja kubwa sana

Jr

Haipo crime mission duniani ambayo inaweza ikafanyika halafu ikawa 100% fool proof, na kama ikitokea hivyo basi ujue kuna interaction ya nature, kwamba wakati mission inafanyika, ilitokea natural incidence ika-coincide na tukio lenyewe na hivyo kulifanya lisiwezekane tena kutambulika kwa akili ya kibindamu.

Tukio la D.B. Cooper, the SkyJacker ambalo FBI bado wanazungusha akili hadi leo, mimi nina-suspect kuwa linaweza kuwa katika aina moja ya matukio ninayoongelea hapa, kwamba wakati D.B. Cooper anatekeleza mission yake, lilikuja likatokea tukio natural ambalo hata yeye mwenyewe hakuwa amelitarajia, na hivyo kui-affect mission yake nzima na kumfanya aonekane kama alipanga tukio ambalo binadamu hawezi kuling'amua, kumbe hapa nature nayo iliingilia kati na kumfanya apate credit zaidi.

Kwenye lugha yetu kuna msemo ambao tafsiri yake kwa kiswahili inasema hivi: SISIMIZI HUTEMBELEA CHINI ARDHINI, ukiwa na maana kuwa unaweza ukafanya crime somewhere katika mazingira ambayo unakuwa uko peke yako kabisa na wala hakuna mtu anayekuona.

Na si kwamba unakuwa uko peke yako kwa sababu unakuwa huwaoni watu wakati wapo hapo ulipo, hapana, yaani katika uhalisia ni kweli kabisa unakuwa uko peke yako na hakuna mtu anayekuona, lakini kile ulichokifanya kitakuja kujulikana na utadhani kuwa wakati unafanya tukio, kuna SISIMIZI alikuwa amekufuata mpaka eneo la tukio, ukafanya tukio akiwa anakuona na wewe ukiwa humuoni, na hatimaye SISIMIZI akarudi tena kule ulikotka naye na akaenda akatoa taarifa zote bila wewe kujua! Narudia tena, hakuna Crime mission unayoweza kufanya halafu ikawa 100% fool proof.
 
Usimwamini mtu yeyote, zaidi ya wewe mwenyewe, wapo kila mahali, na ni ngumu kuwatambua. Chunga sana ulimi.

Hata muokota makopo simuamini.

Lakini sasa na sisi binadamu, tuwe tunaishi maisha ya uhalisia wetu. Yaani inakuwa kama hawa watu wasingekuwepo, tungeweza kuwa tunasema chochote kile tunachoweza kusema, ila wao ndiyo wamesababisha tusifanye hivyo.

Ukiona una tabia ya kuchunga sana ulimi wako, ujue una tatizo na inabidi ulifanyie kazi na inamaanisha kuwa ukiwa huru katika mazingira yako, unaweza kuwa criminal. Wazungu wana msemo wanasema kuwa MAN'S REAL CHARACTER IS "WHAT HE WOULD DO IF HE KNEW HE WOULD NOT BE FOUND".

Binadamu tunatakiwa kuwa na tabia ambayo inabidi ufiche machache sana, na ikiwezekana yale ambayo ni ya maisha yako binafsi tu, na ambayo ni mema pia. Ukiona unaficha mengi sana na unachunga sana ulimi wako, ujue UKO NEGATIVE, KWAKO NA KWA WATU WENGINE PIA wakiwemo viongozi wako na ndugu zako pia!
 
Hapana kuna baadhi ya habari zimepewa hadhi ya classified INFO hizi huwa haziandikwi hata mitandaoni.... Pamoja na uhuru wetu wa kuhabarishana kuna habari hazipaswi kamwe kuandikwa huku mitandaoni..
Unaweza kujikuta kwenye matata makubwa kwa kuulizwa ulijuaje?
Unatoa siri za watu eeh!
So yule mama aliyemuuzia anko magu matunda kule bandarini alikuwa mzugaji?
 
Maswali ya msingi ya kujiuliza ...
1. Utawajuaje?

2. Wapi huchukua hayo mafunzo?

Nikipata majibu ya hayo maswali nitaongeza mengine ..
Nimeuliza maswali haya kwa sababu zifuatazo ...
Ninapoishi kuna ofisa mmoja .. nilimpa habari za uhakika .. akabeza na kuniuliza kuwa nimepataje taaarifa muhimu kama hizo kabla yake .. nilimjibu apige simu kwa yeyote aliyeko kwenye kituo chake cha kazi ili apate uhakika. Kabla hajapiga nilimeongezea habari kuwamuda mfupi gari litapitisha wahusika wakipelekwa panapohusika.
Alipopiga simu aliambiwa kuwa habari ni za kweli ...
Mpaka leo huwa hataki tukae sehemu moja, nikiingia sehemu alipo lazima yeye atoke. Akinikuta sehemu atasalimia na kuondoka tu.
Hisia zangu zinanituma kuwa nahisi mimi ni aina ya hao watu wakati mimi siko kabisa kwenye kazi za ajabu-ajabu kama hizo.
Macho na masikio kwako wewe ulosoma hii chango yangu.

Inasemekana kuwa wanawake wawili waliosababisha kifo cha mdogo wa Mh. Rais wa Korea ya Kaskazini kwa kumpaka sumu usoni akiwa uwanja wa Ndege, hawakujua kuwa walichokuwa wanampaka usoni ni ilikuwa ni na sumu ambayo ingeweza kusababisha kifo chake; na wala pia hawakuwa na nia ya kuondoa uhai wake, ila inasemekana kuwa walikuwa kwenye michezo yao ya kuigiza or something similar!
 
Nimekua na rafiki yangu kwa muda mrefu kidogo, bahati mbaya ni yatima.Nimesoma nae advance huko pomerini iringa. Alikua mtu wa kusoma sana novel,alikua na kipaji cha kushawishi mnoo, yani akikaa na wewe ukawa unaamini katika jambo flani,basi akianza kujenga hoja lazima mwisho wa siku unakubaliana nae,kimsingi ana sifa za kipekee sana,ni mkimya kama mimi, but ukimya wake nilikua nauona kama sio ukimya as ukimya tu! ila alikua kama ni mtu anaechakata vitu flani katika akili yake,ofcoz ni miongoni mwa watu wenye iq kubwa kuwahi kukutana nao,digrii yake kasoma sauti mwanza, na misimu yote akiwa anasoma pale nilikua nakutana nae sana tu, ingawaje kuna vipindi kadhaa naeza kuwa kwenye mihangaiko mikoa mingine ghafla nakutana nae stand, ukimuuliza anakwambia natoka kwa shemeji yako sehemu flan (mkoa).na kwakweli huyu bwana alikua mtu wa totozi sana. aliwahi kufanya field office mbili za mambo ya kisheria na mabosi wote wa office zile ni wanawake na alifanikiwa kuwanyanyua (Fu£$%&),nilikua namuuliza unawezaje kufanya hivyo? alikua ananijibu tu,ni kazi rahisi sana ,moja kati ya vitu vilivyokua vikinishangaza ni lifestyle yake,hakua mtu wa kupata shida ya kipato kabisa, nilikua nikimchunguza sana mienendo yake lakini sipati jibu. Baada ya kumaliza chuo mwaka mmoja mbele nakuja kukutana nae morogoro. akanipeleka kwake katika appartment flan ni mkabala na fieldforce morogoro, alikua vizuri sana. usafiri mzuri nk.nk nikamdadisi lkn majibu mafupi tu. kilichotokea baada ya hapo ni kwamba yule bwana hakutaka mawasiliano na mimi tena,ila ni baada ya kumchana kwa kumwambia nimekuelewa wewe ni nani. nikafuta na namba yake...
Ulifanya blunder ni utoto! Next time ukaona kitu kama hicho, kaa kimya!
 
Absolutely.

Umenikumbusha mbali sana.

"Locard Exchange Principle".

Trace huachwa ili kutumika ku-track jambo lililolengwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sahihi sana locard's principle inadai hivyo na ......
Proudly sponsored by
RUDI NYUMBANI KUMENOGA!

Jamaa aliondoka kwenye crime scene na jani la mti lilidondokea kwenye cabin ya pick-up yake. Na hili wanakiri kuwa ni tukio ambalo kwa mara ya kwanza DNA ya mti ilitumika kama ushahidi mahakamani na kumtia hatiani mtuhumiwa. Kabla ya hapo, DNA ya mti ilikuwa haijawahi kutumika, isipokuwa ya binadamu tu.

Hawa jamaa huwa wanatumia akili kubwa hadi huwa inanipa maumivu mwilini nikianza kufikiria wanavyofanya kazi! Acha kabisa
 
Back
Top Bottom