Camouflagers na informers

Kuna movie nimewahi kuona jamaa anajifanya muuza cd bar kumbe ni informer alijifanya anauza cd kwa bei nafuu halafu mchangamfu kumbe alikuwa amemtegea jamaa kinasa sauti kwenye key holder aliocha mezani
 
KISWAHILI ni wazugaji na wafichua habari
Ni watu maalum lakini wa kila jinsia umri na kaliba... Kati yao wapo mpaka wezi matapeli, wakabaji na wachawi.. Lakini kila walipo wapo kwa lengo maalum.... Kutoa taarifa ambazo zitasaidia kubaini waovu na kuzuia hatari ama kulinda usalama wa nchi raia ama viongozi....
Hawa watu hutumika kwa namna tatu
1. Kutoa taarifa muhimu za kihalifu zinazosaidia kuepusha janga fulani katika jamii... Iwe la kiongozi ama jumuiya
2.Hutumika kuwajenga viongozi na propaganda za kukubalika kwa kiongozi fulani katika jamii
3. Hutumika wakati wa hatari ya usalama wa nchi,mipango ya mauaji ya viongozi, mapinduzi ya kijeshi, maandamano migomo nk
Ni aina ya watu wenye elimu na waliopewa mafunzo maalum juu na namna ya kuvaa uhusika fulani bila kujulikana, namna ya kuongea, kuripoti na kutoweka eneo la tukio bila kuacha alama yoyote na kujulikana uhalisia....

Mfano wa kwanza
Kiongozi mkubwa anapotaka kutembelea eneo fulani, wazugaji na watoa taarifa za siri hufika wiki moja ama zaidi kabla ya ziara rasmi... Hapa hujigawa katika makundi mawili
. kundi la kwanza ni la kusoma hali ya hewa kiusalama na kukubalika kwa kiongozi.. Mambo mabaya yanayotendwa na viongozi wa eneo husika na maoni ya wadau
. kundi la pili ni wazugaji. Hawa ni wana kitengo cha propaganda ili kuonyesha kukubalika, kuaminika na kuungwa mkono kwa kiongozi na imani juu ya wale aliowatembelea.. Hapa si ajabu kumkuta kiongozi anakula chakula mtaani kwenye banda fulani bila hofu, kunywa kinywaji kama dafu ama kula kitu kama karanga tunda nk... Wauzaji wa vitu vyote hivi ni watumishi wake waaminifu

Mfano wa pili
Nchi inapopitia kipindi cha mashaka kama maandamano usaliti na mapinduzi..
Hapa huangaliwa kwanza maeneo yenye ushawishi mkubwa wa jambo husika.... Ndipo hupelekwa timu ya watu maalum!! Mfano anafika mtu wa kawaida kwenye bar ya kawaida mtaani, ambapo pembezoni kuna kijiwe na bodaboda nk.. Huyu aliyeko bar anakuwa busy na simu na kinywaji chake... Hana story na mtu... Kisha anakuja mwingine mzugaji kama machinga, anajifanya anauza keyholders kwa bei poa sana na kama huna hela anakukopesha...
Bila kujua zile keyholders zina mawasiliano ya moja kwa moja na jamaa aliyeko pale bar

Mfano wa tatu
Hatari ya kuvamiwa kijeshi... Hapa ni pakubwa na penye mengi lakini wanawake warembo hutumika sana kipindi hiki... N kundi lingine ni wazugaji wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa na watafiti wanaotaka kuwekeza ama kutafiti....
Yote kwa yote jihadhari sana na mikusanyiko yenye dhumuni la maandamano hasa ya kisiasa ama kupinga jambo fulani kitaifa... Ukiachana na wale askari wa fanya fujo uone wenye mabomu ya machozi na risasi za mpira, huwa kuna mdunguaji mmoja tu hatari sana kwa ajili ya kumdungua kiongozi ama walio mstari wa mbele... Kimbia jifiche....

Unaposikia kiongozi kafika mahali na watu fulani wamewajibishwa kwa haki, tambua wazi ni kazi iliyotukuka ya wazugaji na wafichua habari
Unaposikia maandamano, mgomo ama mapinduzi fulani yameshindikana jua fika kwamba kuna kazi kubwa imefanywa na hawa jamaa
ILA unapoona mojawapo kati ya hayo niliyotaja yamefanikiwa vizuri, basi hawa jamaa ama wamefeli ama wanekengeuka miiko yao..!
Kamwe usiwaamini hawa watu hata kama ni ndugu yako... HAWATABIRIKI...!



Jr
Aisee jicho lako la tatu linaona mbali sana
 
Hawa wako chini ya kiwango
IMG-20190605-WA0039.jpeg
 
Kuna movie nimewahi kuona jamaa anajifanya muuza cd bar kumbe ni informer alijifanya anauza cd kwa bei nafuu halafu mchangamfu kumbe alikuwa amemtegea jamaa kinasa sauti kwenye key holder aliocha mezani
Nilikutana na muuza mikanda maeneo ya Sinza nikamshtukia... Nikamkazia sana macho, akaniuliza faza vipi mbona macho kodo kama nimekuchukulia demu wako... Nikamwambia kawaida tu ila kwa kuzuga tu hujambo.. .. Aliondoka fasta sana na Biashara hatukufanya
 
Hizi habari huwa nazielewa sana.

Mshana mwaga uhondo wote bn kuna comment nimeona unasema hii ni sehemu ndogo sana katika uhalisia kama ¼ vile.tunaomba utujuze kwa tunaopenda habari km hizi
 
Hizi habari huwa nazielewa sana.

Mshana mwaga uhondo wote bn kuna comment nimeona unasema hii ni sehemu ndogo sana katika uhalisia kama ¼ vile.tunaomba utujuze kwa tunaopenda habari km hizi
Hapana kuna baadhi ya habari zimepewa hadhi ya classified INFO hizi huwa haziandikwi hata mitandaoni.... Pamoja na uhuru wetu wa kuhabarishana kuna habari hazipaswi kamwe kuandikwa huku mitandaoni..
Unaweza kujikuta kwenye matata makubwa kwa kuulizwa ulijuaje?
 
Yuko mmoja overseerer wa wauza magenge hapa Nanjilinji alifanya kila linalo wezekana kuunga urafiki na mimi nikawa nimemstukia kiaina mapema sana. Nikamleta karibu ili asipate taabu kufanikisha alichokitaka kwangu. Akawa best rafiki na jamaa yangu. Si kuwa na hofu maana mimi ni raia mwema daraja la juu kabisa(raia mkureshi tuseme hivyo). Mahusiano yetu yakawa ni nipe ni kupe, Kila nikipata habari yenye uzalendo ndani yake naianzishia stori tukiwa naye. Kama jamaa au rafiki kahitilafiana na sheria na yuko mahabusu polisi akihitaji dhamana na mtanguliza yeye mbele dhamana inatoka chapu chapu Siku hizi ni marehrmu RIP nimekosa huduma na company yake. Ila nidhamu yake ilikuwa ya kupigiwa mfano na alikuwa wa msaada kweli.
Hapa TUNAITA QUID PRO QUO...
 
138 Reactions
Reply
Back
Top Bottom