Camouflagers na informers

Kuna watu hamjitambui kweli na msizungumze kama vi2 hamvijui, eti TISS wanaanzisha mada ya kumsema vibaya magufuli, ukiunga mkono mkono hoja wanakuchukua, labda hiyo TISS ya ccm, majukumu ya TISS ni makubwa sio kama mnavyodhani et kudeal na wanaomtusi rais
Labda hiyo TISS ya ccm.... na pengine yenye sisitiivii
 
Camouflage na informers wapo wengi sana...

Haswa wengine utawakuta maeneo ambayo kwa hali ya kawaida mtu hawezi kuthubutu kuweka bishara ya kuuza vipipi na karanga eneo hilo...

Ningeyataja hayo maneno ila wacha niake kimya...


Cc: mahondaw
Pale morogoro mjini Kuna kijiwe karibu na stendi ya ice wana shoe shiner kibao na magazeti wanaongea siasa muda wote na wazee wakazi wamo


Shomariiii
 
Mi ndo mana huwa simwamini mtu hafu wengi huja na mada chokonozi kwenye group kwa malengo yake, nakumbuka nilisoma kisa cha CIA kumpandikiza muislamu mwenye msimamo Mkali kwenye msikiti na yeye ndo aliyekuwa ana plan ugaidi kumbe ni agent wenzake wakaenda kumshitaki nikajua hii dunia nikuwa makini na Ku angalia mambo ya kuongea ukiwa na watu unao wa fahamu na usio waelewa

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku hizi hawa wachokoza mada wametapakaa kila mahali.yani unakuta baba zima na midevu chekwaa,likisifu vitu vya kijinga kabisa.

Lengo lao hua ni kuamsha tu hisia.usipo wajua unapoteza nguvu/muda mwingi ku jibizana nao.ila wanakera hatarii
 
KISWAHILI ni wazugaji na wafichua habari
Ni watu maalum lakini wa kila jinsia umri na kaliba... Kati yao wapo mpaka wezi matapeli, wakabaji na wachawi.. Lakini kila walipo wapo kwa lengo maalum.... Kutoa taarifa ambazo zitasaidia kubaini waovu na kuzuia hatari ama kulinda usalama wa nchi raia ama viongozi....
Hawa watu hutumika kwa namna tatu
1. Kutoa taarifa muhimu za kihalifu zinazosaidia kuepusha janga fulani katika jamii... Iwe la kiongozi ama jumuiya
2.Hutumika kuwajenga viongozi na propaganda za kukubalika kwa kiongozi fulani katika jamii
3. Hutumika wakati wa hatari ya usalama wa nchi,mipango ya mauaji ya viongozi, mapinduzi ya kijeshi, maandamano migomo nk
Ni aina ya watu wenye elimu na waliopewa mafunzo maalum juu na namna ya kuvaa uhusika fulani bila kujulikana, namna ya kuongea, kuripoti na kutoweka eneo la tukio bila kuacha alama yoyote na kujulikana uhalisia....

Mfano wa kwanza
Kiongozi mkubwa anapotaka kutembelea eneo fulani, wazugaji na watoa taarifa za siri hufika wiki moja ama zaidi kabla ya ziara rasmi... Hapa hujigawa katika makundi mawili
. kundi la kwanza ni la kusoma hali ya hewa kiusalama na kukubalika kwa kiongozi.. Mambo mabaya yanayotendwa na viongozi wa eneo husika na maoni ya wadau
. kundi la pili ni wazugaji. Hawa ni wana kitengo cha propaganda ili kuonyesha kukubalika, kuaminika na kuungwa mkono kwa kiongozi na imani juu ya wale aliowatembelea.. Hapa si ajabu kumkuta kiongozi anakula chakula mtaani kwenye banda fulani bila hofu, kunywa kinywaji kama dafu ama kula kitu kama karanga tunda nk... Wauzaji wa vitu vyote hivi ni watumishi wake waaminifu

Mfano wa pili
Nchi inapopitia kipindi cha mashaka kama maandamano usaliti na mapinduzi..
Hapa huangaliwa kwanza maeneo yenye ushawishi mkubwa wa jambo husika.... Ndipo hupelekwa timu ya watu maalum!! Mfano anafika mtu wa kawaida kwenye bar ya kawaida mtaani, ambapo pembezoni kuna kijiwe na bodaboda nk.. Huyu aliyeko bar anakuwa busy na simu na kinywaji chake... Hana story na mtu... Kisha anakuja mwingine mzugaji kama machinga, anajifanya anauza keyholders kwa bei poa sana na kama huna hela anakukopesha...
Bila kujua zile keyholders zina mawasiliano ya moja kwa moja na jamaa aliyeko pale bar

Mfano wa tatu
Hatari ya kuvamiwa kijeshi... Hapa ni pakubwa na penye mengi lakini wanawake warembo hutumika sana kipindi hiki... N kundi lingine ni wazugaji wanaojifanya ni wafanyabiashara wakubwa na watafiti wanaotaka kuwekeza ama kutafiti....
Yote kwa yote jihadhari sana na mikusanyiko yenye dhumuni la maandamano hasa ya kisiasa ama kupinga jambo fulani kitaifa... Ukiachana na wale askari wa fanya fujo uone wenye mabomu ya machozi na risasi za mpira, huwa kuna mdunguaji mmoja tu hatari sana kwa ajili ya kumdungua kiongozi ama walio mstari wa mbele... Kimbia jifiche....

Unaposikia kiongozi kafika mahali na watu fulani wamewajibishwa kwa haki, tambua wazi ni kazi iliyotukuka ya wazugaji na wafichua habari
Unaposikia maandamano, mgomo ama mapinduzi fulani yameshindikana jua fika kwamba kuna kazi kubwa imefanywa na hawa jamaa
ILA unapoona mojawapo kati ya hayo niliyotaja yamefanikiwa vizuri, basi hawa jamaa ama wamefeli ama wanekengeuka miiko yao..!
Kamwe usiwaamini hawa watu hata kama ni ndugu yako... HAWATABIRIKI...!



Jr
Mkuu kwenye kutotabirika ni kwa sababu ya miiko au? Maana nasikia hata ndugu yako anaweza kukuruka ukajifia, ni kama watoa kafara eeeee?
 
138 Reactions
Reply
Back
Top Bottom