Sinkala
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 1,773
- 683
Cameroon imeichapa DRC mabao 3-2 ugenini mjini Kinshasa, lakini haitaenda CAN 2012 kutokana na kuwa ya pili bila hata ya kujali matokeo ya pair nyingine ya mechi kati ya Mauritius na Senegal. Cameroon imemaliza mechi sita kwa kupata pointi 11 huku Senegal ina pointi 13 hata kabla haijaivaa Mauritius. Mechi hizi hazikuchezwa pamoja kwa kuwa hakukuwepo uwezekano wa kupanga matokeo.
Cameroon inasubiri miujiza kuingia katika kapu la washindi wa pili walio na matokeo bora (best run-up) lakini ni kama vile haupo uwezekano, kwani katika timu tatu za best run-up, tayari mmoja (Sudan) ameshaondoa matumaini hayo kwa kuwa wa pili kwa pointi 13. Timu nyingine zilizo za pili na mchezo mmoja mkononi kwenye makundi yao lakini zina pointi 11 sawa na Cameroon ni Libya na Tunisia, huku Nigeria na Angola zikishinda kwenye makundi yao zitafikisha point 12