Cameroon yashindwa kufuzu fainali za kombe la Dunia

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
YAOUNDE, CAMEROON

HATIMAYE mabingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika, Cameroon, wameshindwa kuonesha ubora wao na kujikuta wakitolewa katika michuano ya kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.


Mabingwa hao walipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye michezo hiyo na kufuzu Kombe la Dunia kutokana na uwezo wao waliouonesha kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika, huku ikiwatumia wachezaji wengi vijana, lakini wamekutana na ushindani wa hali ya juu na kutolewa nje.


Juzi walishuka dimbani mjini Yaounde na kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Nigeria, jambo ambalo limewafanya washindwe kufuzu Kombe la Dunia kwa kuwa sare hiyo wanakuwa na jumla ya pointi 3 baada ya kucheza michezo minne sawa na Nigeria wenye pointi 10, kabla ya mchezo wa jana kati ya Zambia dhidi ya Algeria kwenye kundi hilo B.


Nigeria walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 30 lililowekwa wavuni na nyota wao, Moses Simon, lakini Cameroon waliweza kusawazisha katika dakika ya 75 kupitia kwa mchezaji wake Vincent Aboubakar.


Dakika 15 za mwisho, Cameroon walionekana kupambana ili kutafuta bao la ushindi lakini mlinda mlango wa Nigeria, Ikechukwu Ezenwa, alionesha kiwango cha hali ya juu kwa kuokoa mipira miwili ya hatari iliyopigwa na Arnaud Djoum na Collins Fai.


Cameroon imekuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kushindwa kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, huku ikiwa chini ya kocha wao Hugo Broos.


Kocha huyo amesema, japokuwa ameshindwa kufuzu, lakini bado ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo na kupambana kuhakikisha anatwaa tena taji la Kombe la Mataifa ya Afrika msimu ujao.


“Bado ninahitaji kuendelea kuwa hapa, sina mpango wa kujiuzulu, lengo langu ni kuhakikisha ninashinda tena taji la Mataifa ya Afrika kwa mara ya pili mwaka 2019 kwenye ardhi ya nyumbani. Sijatangaza kujiuzulu kwa kuwa mimi si miongoni mwa makocha ambao wanaachana na timu baada ya kufanya vibaya,” alisema.


Afrika kuna makundi matano, hivyo vinara wa makundi hayo watajihakikishia wanakata tiketi ya kushiriki michuano hiyo, timu ya Tunisia, Nigeria, Ivory Coast, Burkina Faso na Uganda zinaongoza kwenye makundi hayo kabla ya michezo ya jana.

Chanzo: Mtanzania
 
Hili kundi lao ndio kundi la kifo. Ilibidi tu giant mmoja afe tatizo "kameruni" imekufa kinyonge.
Unapoweka Algeria, Zambia, Nigeria na Cameron kundi moja ni wazi kuwa hali ni tete kwa kila timu.
 
sasa unataka kundi jepesi kucheza world cup... africa kuna nchi almost 60.. ila kuna nafasi 5 tu za world cup... hapo ni kukaza tu afe kifa afe beki kila mtu ametoa macho ukizembeaaa umekosa tiketi hizo 5


Hili kundi lao ndio kundi la kifo. Ilibidi tu giant mmoja afe tatizo "kameruni" imekufa kinyonge.
Unapoweka Algeria, Zambia, Nigeria na Cameron kundi moja ni wazi kuwa hali ni tete kwa kila timu.
 
sasa unataka kundi jepesi kucheza world cup... africa kuna nchi almost 60.. ila kuna nafasi 5 tu za world cup... hapo ni kukaza tu afe kifa afe beki kila mtu ametoa macho ukizembeaaa umekosa tiketi hizo 5

Sijasema popote kwamba nataka kundi jepesi......
All i said is hili kundi ni kundi la kifo, wanamichezo wameelewa.
 
okwi uganda anapata namba kweli? maana mataifa africa hakuchaguliwa hata kukaa benchi.... anakula mshahara wa bure tanzania
Unajuaje kutumia JF ukashihdwa ku-google. Last week Uganda ilipiga Misri 1,Okwi akiwa nfungaji na man of the match
 
uganda si mwenzetu kabisaa... leo anaongoza kundi sisi tumezubaaaa tu na samatta wetu...

juzi tu kacheza mataifa africa sisi tunashangaa tu na anaweza akacheza world cup kama utani
Ninkweli waganda si wenzetu,jana wamepiga mpira mwingi sana ila hawaongozi kundi,jana walifungwa moja bila wana point 7 misri ana 10.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom