Cameroon: Maofisa wa serikali watekwa na wapiganaji

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,410
2,000
Afisa wa jeshi la Cameroon amesema afisa mwandamizi wa serikali anayefanya kazi katika ofisi ya gavana wa kusini magharibi huko Buea, moja ya mikoa miwili inayotumia Kiingereza ya Cameroon Bw. Franckline Ngwa Che, ametekwa na watu wasiojulikana na kudaiwa fidia ya mamilioni ya Faranga. Mwingine ni mkuu wa kikanda wa Wizara ya Mazingira na Ulinzi wa mazingira Cameroon aliyetekwa katika mkoa wa kaskazini magharibi, mkoa mwingine unaotumia lugha ya Kiingereza.

Afisa huyo ameongeza kuwa wameagizwa kufanya kila wanaloweza kuwaokoa salama, na inaonekana kuwa wateka nyara sasa wanawalenga viongozi wa Serikali.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu laki 4.3 nchini Cameroon wamekimbia migogoro.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom