Camera ya cannon type ipi iko vizuri kwa picha?

Aaisee Mnataja vyombo Vikali!
Mie nina Canon B500 kumbe si lolote

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Labda kwanza nikuweke sawa
1. Biashara ya picha SIO BIASHARA NDOGO
2. Unapoomba ushauri USIONESHE UNAJUA
Sasa nikushauri, sasahiv camera nzuri ni zile za mfumo wa DSLR(Digital Single Lens Riflex)
Na kuna brand nying mf. Canon, Nikon, Sony, Samsung, Pentax, na nyingine nyingi.
Kwa mahitaji camera ya still pictures nzuri ya gharama nafuu ipo Nikon D40,D3100 hizi ni camera nzuri sana
Thanks
 
Za muda huu,

Mtoa mada na wengineo..!

Naomba nitoe ushauri kidogo juu ya hili bandiko; Vitu vya kuzingatia unapotafuta camera especially DSLR camera
1. Kwa kuanzia hakikisha camera unayonunua ina kianzio cha 16 Megapixel
2. Wekeza zaidi kwenye lens achana na kuhangaika kununua camera kubwa wakati unaanza business,uzuri wa DSLR camera ukitaka ku-advance basi unabadili tu Body maana lens utakuwa nazo
NOTE: Epuka kuanza na camera kubwa kama zilizotajwa na wadau hapo juu Eg. canon EOS 5D Mark 3,2 7D au Nikon D7100, D7200 ni aghali sana hivyo kama huna hela ya kutosha achana nazo, badala yake tafuta camera za kuanzia Eg Canon 1300,Canon 77D, Canon 80D, Canon 750D, Canon EOS 800D, Canon EOS 200D/300D, Canon EOS 700D
au Ukipenda Niko basi Nikon D3200, D3300 au D5600 (pia Nikon D3100 ila tafuta Prime Lens/ Lens Kubwa)

Hizo camera ambazo nimekutajia ni camera nzuri kwa kuanzia na bei zake si mbaya zingonga still na Video kiwango cha 1080p (yaan full HD. Kama una Link marekani Kuna Amazon wanauza hizo camera with full Package( Camera body,lens,wide angle lens, tripod, Flash and 32GB memory card. Kwa Amazon ivyo vitu unavipata betwen $350-400.

Ambapo ukinunua tanzania, huwa hupewi package ya namna hiyo, watakupa tu Camera peke yake tena wakati mwingine Bila Lens so cost ya kuanza kutafuta vitu vingine inakuwa Kubwa.

Personally mimi ni Mfanyakazi nimeajiriwa, ila nafanya business ya photographing and Videographing, nilianza na Nikon D300 for still na D3100 for Video, ni camera ndogo kiasi kwamba wakati mwingine wapiga picha wengine wakiona picha zangu wanashangaa nikiwaambia kuwa zimepigwa kwa Nikon D300, ila nimewekeza kwenye Lens kubwa baasi, tena huwa sifanyi Editing kabisa editing yangu ni from my camera setting tu baasi baada ya hapo nahamisha picha kwenye computer na kuzichambua na kupeleka studio kwa kusafisha, mambo ya Photoshop sijui huwa napiga kwa picha za advert tu (mitandao ya kijamii etc)

MTAZAMO wangu Camera kubwa sio ishu as long as camera ni dslr, una lens za kutosha 18mm-55 and 55-200, pixel from 16 na kuendelea nakuhakikishia utafanya kazi nzuri sana, kitu nilicho note kwa Wapiga picha wengi hawataki kuwekeza kwenye knowledge ya kazi yao, dslr zina setting nyingi sana kiasi kwamba ukiwa unatafuta elimu kuhusu matumizi ya hiyo camera yako unajikuta unafanya kazi nzuri hadi watu watashangaa.
Tunajifunza mengi
 
Bro naomba Msaada

bro Mimi naweza kufanya kazi hiyo Sema sina vifaa
Kama upo serious na hiyo kazi, una customers base njoo inbox nitakukabidhi vifaa vya kisasa ikiwemo canon new model ( 5D mark 3)..njoo na wazo tufanye kazi..sharti ni moja tu uje na idea ya namna gani tutapata pesa na idea iwe realistic
 
Wakuu mimi nataka kuchukua canon 700D kwa ajili ya kuchukua picha mnato na video kwa kuanzia.

Naomba msaada kwa yafuatayo,
Kama nikiagiza kamera hii full set kutoka nje kwa kupitia mitandao kama amazon itanigarimu kiasi gani? Na guarantee ya usalama wa vifaa utakuwaje?
 
Vipi kuhusu Nikon B500 16mp, nimeona mtandaoni kariakoo mall inauzwa 630k, nataka nichukue nitumie kupiga picha mgando tu kwenye senta ndogo, sipo mjini.

Ubora wake upoje? Maana humuzimezungumziwa za viwango vya juu tu za 'mjini'
 
Unajua mkuu issue sio bei bali ni kile unachopata na bei unayotoa.

Mfano wewe umeona inauzwa laki 6 na bei ni rahisi ila hio camera nje ni around dola 200, hivyo unaweza uziwa used kwa laki 6 na ukawa umetoa Hela nyingi kuliko unachopata.

Pia ni Digital camera Ya kawaida ambayo pengine quality yake ya Picha inapitwa na Simu nyingi tu. Haina raw na features nyingi utakazopata kwenye Dslr.

Tafuta Dslr Camera, Hata ikiwa ya Kizamani itakupa Picha Nzuri na kazi yako itaheshimika.

Kwa kariakoo mall
Nikon D3500 W/ AF-P DX NIKKOR 18-55mm lens – Kariakoo Mall

Unapata Dslr second hand kwa laki 5 mpaka 6.
 
Ubarikiwe sana mkuu!
 
Back
Top Bottom