Cambridge Analytica Saga: Namna taarifa zinavyofanya kazi kwenye siasa

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Job saga. Ili ni vugu vugu ambalo wote tumekuwa mashuhuda kwani limeweka historia kwa nchi.

Baada ya kuwa na spika wa kwanza kujiuzulu akiwa madarakani.

Je, unafahamu Cambridge anlytica saga? Fuatana nasi, ila usisahau kufollow, like na kuacha maoni yako
hivyo ni muhimu zaidi kwetu.

Cambrige analitika (soma hivyo hivyo kwa sababu tumeandika kiswahili kabisa). Ni utafiti ambao ulifanyika kupitia mtandao wa Facebook (Meta kwa sasa). Ulilenga kuwahusisha wamerekani zaidi ya laki mbili.

Uliowahusu watumiaji wa mtandao wa fesibuku. Ulikuwa utafiti wa kawaida ambao uliwalipa wamarekani hao ili kupata taarifa zao binafsi. Kiongozi wake akiwa bwana Alexander Nix. Yaani mtu anakupa maswali mepesi mno kisha anakulipa pesa.

Hii ni raha ya kiasi gani? Lakini licha ya kuwa wazungu ni watu wenye weledi. Hawakuelewa malengo ya utafiti huo!

Kwanini inasemekana utafiti huo ndio chanzo cha Trump (usiyempenda). Kuingia white house. Dozee kuwa mpole. Mdogo mdogo tutaelewana muhimu ni kuweka utayari wa kuelewa kichwani mwako. Kisha achana na kubisha usiyoyajua mengine muachie muandishi.

Mwanzo tulisema kuwa utafiti ulilenga kuwafikia wamarekani laki mbili lakini kulingana na sera za fesibuku wakati huo. Zikawezesha utafiti huo kuwafikia wamarekani milioni 50 inashangaza eeenh! Na unafikiri ni kwanini fesibuku umekuwa mtandao unaokutwa na madhira kila mara. Sababu ni hii ya sera yake ya faragha.

Sifahamu kwa sasa mara baada ya kubadili jina la kampuni lakini kitambo hiyo ni kuwa. Ikiwa ungeenda fesibuku kununua taarifa zangu mimi @falsafa70 Basi ungeweza kuwa na taarifa za marafiki zangu wote.

Bado inashangaza, basi tulia. Hii ndio ilisababisha watu laki mbili kufikia milioni 50. Sababu walihusishwa na wale marafiki zao. Sasa inshu ikaja kwanini wawalipe watu kwa kuawauliza maswali mepesi mno na ujira ulikuwa mkubwa. Mwenye akili ataohoji, mpumbavu atakubali.

Wanasema ukiondoa mafuta na madini basi taarifa ndio biashara ghari zaidi kwa sasa ulimwenguni. Why, kwanini?. Kwa sababu pale wanapokuwa na taarifa zako ni rahisi zaidi kukushawishi kwenye chochote kile chenye uelekeo wako. Mfano ikiwa wewe ni mpenz wa mpira ni rahisi kukubetisha. Ikiwa wewe ni mpenzi wa konekisheni ni rahisi kukuwekea saiti za porn.

Ndivyo mambo yanavyokwenda kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia. Sasa watu wale walikuwa wamepata ni nini wananchi wale wanapenda. Kupitia maswali yale mepesi waliyo ulizwa.

Na taarifa zile zilikuja kuwa muhimu kwenye uchaguzi wa Marekani wa mwaka 2016 na kumpatia Trump ushindi? Uchaguzi huo ambao ulijawa na visa na mikasa mingi. Mingine isiyo simulika kwa urahisi. Na hatupa hapa kwa ajili ya hayo ila tupo hapa kukuelezea ile iliyo kuwa ikisimulika. Sasa usie mpenda aka Trump aliwasiliana na Cambrige anaritika na kununua taarifa hizo.

Ambazo zilisaidia kusoma upepo wa raia umekaaje kisiasa? Taarifa zile zilimsaidia Trump kuwafikishia watu kile walichotaka kusikia. Iko hivi mara nyingi ukitaka watu wakuelewe kwa urahisi wape kile wanachokihitaji na sio uhalisia wake.

Ndio alichokifanya mzee baba. Hii ilijulikana na wamarekani wenyewe kama walichezewa akili zao (brainwash). Sasa taarifa zile zilitumika kupitisha matangazo ya kampeni kulingana na mtu husika na hapa fesibuku ilihusika na show.

Mfano kupitia ule utafiti ulionesha wewe unapenda kilimo. Basi makampenist wa Trump wangekuletea matangazo ya kumchagua mzee baba ili akutatulie matatizo hayo. Sijui nimeeleweka ila kwa urahisi ni hivi:- hapa nchini tatizo ni ajira kwa vijana si ndio!.

Basi apatikane mgombea ambaye aseme kuwa atatua changamoto hiyo. Vipi hapo hatakuwa kakugusa kweli? Jibu baki nalo. Hivyo ndivyo walivyofanya au rudi nyuma fuatilia kampeni za gwajiboy. Sasa achana bongo land twenzetu mbele. Mfano wa sera alizozitumia Trump ni ile ya kuruhusu mtu wa chini kumiliki bunduki. (pengine ndio sababu ya kuwepo kwa matukio mengi ya kuuwana kipindi chake).

Lakini sasa taarifa zilikuwa zikiwafikia wapiga kura kwa mfumo. Mfumo huo ulikuwa ni kama new feed yaani chapisho jipya. Lakini lilinifikia mimi niliyeoneshwa kuwa napendezewa na hilo tu. Inakuja kama post kama bhana mkitupa nchi sisi tutaruhusu watu wa chini kuwa na mijegejo. Ila watakao iona ni wale wanaopendezwa na hilo kwa mjibu wa tafiti. Ila iliwapelekea watu sasa kuambiwa wao ni kina nani na watakiwa kufanya nini.

Akili mtu wangu....akiii

Pia akapewa msemo ambao kulingana na tafiti bwana Nix alijua ndio wamarekani walitaka kuusikia. Msemo huo ulikuwa drain the swamp kama ilivyokuwa kwa hapa kazi tu iliyokuwa ikitumiwa na jasiri.

Kwenye siasa za Marekani neno hili ni kubwa mno. Kwani lina historia na limetumika karibuni marais wanne nyuma yake. Mzee baba mwenyewe anakili ya kuwa alipotumia neno hilo alipata shangwe ambalo hakuwahi kulipata Sera hii ilimpa shavu kubwa Trump kwa sababu. Mtu kukubali alivyoambiwa hakupo katika yale aliyoambiwa bali namna alivyoambiwa. Wataalam wa mahusiano mnalijua hili vyema nami sio mtaalam wa hilo.

Ili uelewe ni kuwa ndio maana mara nyingi inakuhitaji kumtafuta mtu wa karibu wa mtu. Ili akufikishie taarifa zako kwake. Konekisheni. Sababu kisaikolojia ni rahisi wewe kumsikiliza mtu wako wa karibu. Kwasababu ni mnafahamiana na sio kile anachokwambia. (take note)

Hivyo ndivyo bwana Trump alivyo pata kiki la ajabu mno na la kushangaza katika uchaguzi huo. Na hivyo ndivyo namna ulimwengu wa taarifa unavyo fanya kazi.

Kwanini nimeyaunganisha matukio haya sababu ni kama yanaendana. Ukiangalia Trump alikuwa hapendwi kabisa na hakuwa na umaarufu wa kisiasa ila akawa rais. Mh. Job alikuwa akipendwa sana na kijani wenzie hawamu 5. Ghafla awamu ya 6 kaamua kujiuzulu.

Sababu ni ile ile taarifa. Alianza kwa kusema mambo ambayo ni muhimu kuyahoji kama kiongozi wa muhili wa kuunda taifa. Lakini njia aliyoitumia kufikisha taarifa zile haikuwa sahihi. Na ndio maana wale wale waliokuwa wakimpigia makofi wakamta ajiuzulu.

Hivyo kwa ulimwengu wa sasa taarifa ni sehemu nyeti katika kukufanya. Upate umaarufu au uchukiwe ni wewe kuchagua.
 
Back
Top Bottom