CAG: Watu watatu wa MSD walitumia Tsh Milioni 215 kwenda China kujadiliana

Kwanini wasihojiwe na kufunguliwa mashitaka kama wameenda kinyume na taratibu ? Na wahojiwe je ni kweli ni mil 215 au kuna zaidi

Na wale wa bot waliokuwa wanachota ela kila siku imefikia wapi?

vidokozi na vijizi vinakamatwa Kwanini hawa wafujaji mashirika ya umma , taasisi na halmashauri wasikamatwe?
Mkuu hii nchi sheria nyingi zina matobo hao jamaa nahakika hawakutoka nje ya sheria walikaa chini wakaitafskari hii sheria then wakafanya yao hata hospital wauuguzi wakiamua kufata taratibu mtaudumiwa watu wa wili then mda wa chai wakirudi wanaudumiwa wawili tena mda wa chakula Cha mchana akirudi ataudumia wawili mda wa kutoka
 
Kwanini wasihojiwe na kufunguliwa mashitaka kama wameenda kinyume na taratibu ? Na wahojiwe je ni kweli ni mil 215 au kuna zaidi

Na wale wa bot waliokuwa wanachota ela kila siku imefikia wapi?

vidokozi na vijizi vinakamatwa Kwanini hawa wafujaji mashirika ya umma , taasisi na halmashauri wasikamatwe?
Wangeanza kwanza na bungeni ndiyo kuna ufujaji mkubwa kuliko hata huu
 
Bila kuwa na mashushu kwenye taasisi za serikali upigaji utaendelea tu, kwanini wameondoa utaratibu wa kuomba vibali vya kwenda nje ya nchi. Bilashaka hayo maombi yalikuwa yanataja dhumuni ya safari, siku za kukaa, idadi ya wanaoenda na watatumia sh? JPM aliweka utaratibu mzuri kabsa ili kuzuia upigaji wa kijinga kama huu.
Umesoma lakini hujaelewa kuhusu barua CEA.169/178/03/18 ya Oktoba 13, 2020 ya uteuzi wa maofisa watatu kwenda China? Ni tarehe 13 Oktoba 2020 sio 2021 ndugu. Maana yake hao wamepiga wakati wa huyo role model wenu.
 
Inasikitisha lakini sidhani kama kuna kosa hapa kisheria. Taasisi nyingi za umma watu wanafuata taratibu kujipatia fedha kimagumashi kwa staili hii, swali ni je is it illegal? Kuna mwongozo unaokataza mfanyakazi kwenye kufanya majadiliano kwa siku 61? Ndio ugumu upo hapo, upigaji mwingi ni watu kutumia mashimo kwenye taratibu za kiofisi, na ndio maana hata kesi haziendi kokote.
Kwa nini ukajadiliane China? Kama unahitaji suppliers wa hizo machine, weka international tender watakutafuta wenyewe. Simu zipo, video conferences facility zipo, kwa nini mpaka uende China? Huu ni ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Too much!
Watajwe.
Huyu jamaa na yeye huwa kilaza sasa anatutajia wizi ili tufanye nini?
Unapokuja mbele ya wananchi ukaeleza jinsi watu wanavyoiba na kiwango walichoiba kwenye serikali unayoisimamia,unataka wananchi wafanye nini?wakupigie makofi?
Anachotakiwa kufanya ni kutia watu adabu kisheria tuone watu wamefungwa,na wamelipa pesa yetu!!huyu jamaa huwa nixstory tu,ilikuwa hivi hivi kwenye wizi pale hazina,Alipiga story mpaka leo hakuna mrejesho,ile tume ya kuchunguza wale kenge polisi walioua mwananchi,Mtwara mpaka leo kimya,
 
Hata kuwataja majina yao tu anaogopa!

Yeye anajua, akishasema hivyo, amemaliza kazi. Kusudi ni kutaka asikike akilalamika watu wajue Waziri mkuu ni mfuatliaji. Kumbe anatoa hewa tu, hakuna lolote la maana.
Ripoti za CAG zimejaa uchafu, lakini wahusika ni kama ni maluhani, hawana majina na hawatakiwi kujulikana kabisa.

Hii hatua ya kutaja majina ingekuwa ni hatua ya mwanzo kabisa katika kuwawajibisha hawa watu. Jamii inasikia mtu fulani kafuja pesa ya serikali, mtu huyo watu watamjua na kama kanunua au kajenga, atakuwa anaona aibu kwa kudhaniwa kuwa mali hiyo ni ya ufujaji wa pesa za wananchi.
Hatua ya pili muhimu ni kuwafikisha mahakamani mafisadi hawa, siyo kuwaacha tu na kuendeleza ufisadi wao.
Yaani nchi hii ukiangalia inavyotafunwa sidhani kama kuna mtetezi wa wanyonge, hawa wote watafunaji na wanasiasa ni ndugu moja tusitarajie jipya.
Labda vizazi vijavyo vitaamua kukataa upuuzi huu na kuchukua hatua.
 
Kwa nini ukajadiliane China? Kama unahitaji suppliers wa hizo machine, weka international tender watakutafuta wenyewe. Simu zipo, video conferences facility zipo, kwa nini mpaka uende China? Huu ni ubadhirifu wa mali ya umma.
Labda hujanielewa... mimi sijaongelea busara, nimeongelea sheria. Je kuna sheria inayokataza au kuelekeza namna na wapi kwa kufanya majadiliano? Ndio hapo kwenye udhaifu na watu wanatembelea humo humo.
 
Majaaliwa yuko sahihi, raisi akiwa Michael Didicoff subordinates wake watakuwa akina kaole
 
Anaendeshwa na remote za Msoga sasa hivi ni toothless person, jaribu tu kumlinganisha na Majaliwa wa enzi za Magufuli ni watu wawili tofauti japo ni mtu mmoja

Magufuli alishampasha tena hadharani kuwa asingebweteka kwani hakukuwa na uhakika wa yeye kuendelea kama Waziri Mkuu!! Sidhani kama angeendelea wa wadhifa huo kwa speed aliyokuwa nayo! Hata hivyo huyu alikuwa kwenye kundi lilokuwa linataka kumuhujumu Hangaya asirithi kiti ; sijui ilikuwaje akaachwa kwenye huo wadhifa.
 
Bila kuwa na mashushu kwenye taasisi za serikali upigaji utaendelea tu, kwanini wameondoa utaratibu wa kuomba vibali vya kwenda nje ya nchi. Bilashaka hayo maombi yalikuwa yanataja dhumuni ya safari, siku za kukaa, idadi ya wanaoenda na watatumia sh? JPM aliweka utaratibu mzuri kabsa ili kuzuia upigaji wa kijinga kama huu.
Kumbuka kuwa huo upigaji ulifanyika mwaka 2020 wakati huo JPM ndo Rais.
 
Mama anasema anataka watu wawe na nidhamu ya kutoka ndani,mara wale kufuatana na urefu wa kamba zao,mara waziri mkuu anasema kuna watu watatu wametumia 215 milioni.... anaishia hapo,tutafika kweli?
Nchi ina mambo ya hovyo sana,ndomaana JPM alikua anawawajibisha hapohapo watu wanao mess up.Ujinga mtupu.
Mbona hao hakuwawajibisha na walienda China Oktoba 2020?? Madudu haya yameibuliwa na ripoti ya CAG ya mwaka wa fedha 2020/2021. Hebu soma vizuri mwanzoni mwa huu uzi uelewe mada sio unadandia mjadala katikati.
 
Kama watu watatu tu ni mapesa yote hayo vipi ile royo tuhuwa

Wiki mbili marekani, Arusha, Zanzibar na Dar.

Kwa msafara wote ule.

Ndio maana hatupewi majibu mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom