CAG Vs SPEAKER: Mgogoro usio wa lazima

Wana JF nimejaribu kufuatilia ubishi wa wakubwa hawa wawili naona wao wameamua kutuchang'anya sisi wananchi wakawaida ili wasikie ya kwetu.
Kwanza, CAG anadai neno "udhaifu" nilakawaida katika taarifa ya ukaguzi kuhusu mahesabu ya kiuhasibu. Sawa hapo mimi sijabisha.
Tatizo langu ni kwamba, kama katika mahesabu yaliyokaguliwa na CAG na kutoa ripoti yake ya juzi, hakuna neno "Bunge ni dhaifu" ina maana alivyosema kule nje ya nchi alikua anasengenya Bunge. Na kama hili neno linaloleta ubishi kwa Mheshimiwa lipo ndani ya Ripoti basi CAG atakuwa sawa kwamba kule nje ya nchi hakuwasengenya. Wale muliorusha vipande vya ripoti ya CAG nitafutieni hicho kipande mukirushe hapa JF.
Haiwezekani kwenye ripoti uwasifie lakini kule kwa wazungu uwaite Dhaifu.
Hilo neno hata lisipokuwepo kwenye report sio ishu sana yeye alikua anafanya majumuisho na maoni yake kwa experience aliyofanya kazi na bunge na pia kusemea ndani au nje ya nchi sio kusengenya uhuru wa kuongea hauangalii eneo kama angekua kateleza angeomba msamaha lakini mbona anasisitiza kuendelea kulitumia.weka pembeni taaluma ya mtu na siasa ndio shida yetu watz tunashindwa hapo.
 
Ndugu Wanajamii,

Sina shaka weekend yenu imekua mwanana na mmejipanga na kuanza juma jipya.

Na imani mmeshaskia mengi juu ya mvutano kati ya CAG na kiongozi wa taasisi ya bunge sio nia yangu kuwachosheni wala kuegemea upande wa nani ni sahihi nani kakosea. Tukirudi kwenye kiini cha mzozo,ile kauli aliyotoa CAG kwamba kwa bunge kushindwa kuisimamia serikali imeonyesha udhaifu,je haikua busara kwa speaker kui counter hiyo kauli kwa kutoa vielelezo namna ambavyo bunge lake limeisimamia serikali ipasavyo ili CAG aonekane muongo na mdhalilishaji?kwangu mimi naamini hoja hujibiwa kwa hoja na si jazba wala mihemko.

Speaker hajachelewa nimuombe iwapo atasoma ujumbe huu au mtu wa karibu wa kumfikishia atumie busara ndogo tu yakuonyesha maeneo ambayo bunge limeisimamia serikali ipasavyo contrary to what CAG is accusing it for kwa kufanya hivyo atajijengea heshima yake,ya bunge tukufu na atamnyamanzisha Prof.Assad kwa hoja.

Naomba kuwasilisha.

Kutoa vielelezo eti kuthibitisha uimara wa bunge, it's too long way to go....

Busara ya watu wazima na wasiopenda kujikweza ama kujiinua, ilikuwa kusema (kama angeulizwa).....

".....nimemsikia CAG wetu akirusha lawama kwetu kuwa sisi kama taasisi, tuna udhaifu wetu.......

Mimi kama kiongozi wa taasisi ya bunge, nakubali kuwa hutuwezi kuwa wakamilifu, inawezekana kabisa tukawa na mapungufu yetu yanayoitwa "madhaifu yetu"........

Na kwa kuwa, CAG haja sight specific ulipo udhaifu wetu, nashindwa kujitetea moja kwa moja unless aki - sight maeneo ulipo udhaifu wetu, hapo naweza kutoa maoni yangu na Mimi......"

Sasa huyu mzee wetu (Job Ndugai - Spika wa Bunge), kwa sababu ambazo actually mpaka sasa watu wenye hekima, hawajaona sababu za mwitikio wake mkuu huu namna hii tena ukiwa hasi kabisa kiasi ambacho ameiingiza taasisi yote ya Bunge kwenye mgogoro ambao hata haukuwa na ulazima....

Very unfortunately kuwa hili lilitokea wakati ndani ya Bunge kukiwa na wabunge wenye uzoefu, wanasheria kama Andrew Chenge pamoja na mwanasheria mkuu wa Bunge na wa serikali kwa wakati mmoja ambao wangeweza kushauri namna bora ya kulitatua jambo hili....

Na moja ya jambo ilikuwa ni kumweleza Spika Ndugai kuacha Mara moja kuli - drag bunge kwenye ishu ambayo direct inaonesha kuwa ni "personal vendetta" baina ya Spika na MTU aitwaye Prof Assad....!!

This is really too bad.......
 
Hata mimi nilishtuka sana. Rais amekuwa mbunge lini? Kwa mfano akisaini hitma ya mtu aliyehukumiwa kifo atakuwa mahakama?Ndugai nasikia ni mwanasheria ametoa wapi akili hiyo?
Mwache Rais a hape kazi yake! Usimletee madudu yako!
 
Spika ndugai kapewa assignment na jiwe kuhakikisha CAG anajiuzuru, maana inaonekana CAG sio mtiifu kwa jiwe na kwa mujibu wa jiwe hawezi tumbuliwa na jiwe, kumbuka jiwe anataka kulipa kisasi kwa.Asad kwa kuonyesha uovu wa jiwe hadharani toka akiwa waziri, kwa hiyo unatafutwa upenyo wa kumlazimisha anajiuzuru kwa hiari maana kumtumbua haiwezekani, sasa kwa vile ndugai anataka kuendelea kuwa spika tena japo anaweza kugeuziwa kibao kama sita.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yebaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo neno hata lisipokuwepo kwenye report sio ishu sana yeye alikua anafanya majumuisho na maoni yake kwa experience aliyofanya kazi na bunge na pia kusemea ndani au nje ya nchi sio kusengenya uhuru wa kuongea hauangalii eneo kama angekua kateleza angeomba msamaha lakini mbona anasisitiza kuendelea kulitumia.weka pembeni taaluma ya mtu na siasa ndio shida yetu watz tunashindwa hapo.
Mku naona hukunipata vizuri hoja yangu. Nachosema ni hivi neno Udhaifu ni kawaida sana kama amekagua tasisi akakuta mapungufu na ndo madhaifu ya kuyafanyia kazi. Na kwa mantiki hiyo Prof.Assad anakuwa sahihi.
Lakini kama mimi hujaja kunikagua katika uwanja au eneo husika, huwezi kunambia kwamba nina udhaifu katika eneo hilo hapo ni tusi kwangu. Mana ukisema nina udhaifu katika ukaguzi, lazima uwe na vielelezo jinsi navyo paswa kufanya kazi na hali halisi ulioikuta wakati waukaguzi.
Ndo maana nkauliza, kwani ripoti ya CAG ya ukaguzi kuhusu Bunge, iliyasema humo ndani ya ripoti yake au aliona aende kuyasema huko kwa Wazungu?
 
Mnanishangaza Sana mnavyotekwa kirahisi na kutegeka.kwa hiyo mnaamini Kuna siku spika atakuwa na beef na CAG?Wote hao Ni maofisa wa serikali na msifikiri kwamba hawapigiani simu Kuongea pamoja.kazi zao zote Ni kwa ajili ya watu.msipoteze nguvu zenu kuhadaika na michezo ya kisiasa tu mwishowe mnaingia king baadae kick ikipatikana mnabaki nyie kuaibika.come one!wake up brothers.
 
Ngoma mbichi mkuu.

Unafikiria karibu sana.hii ngoma unavyoiona ndivyo ilivyo hivyo hivyo wala haijatiwa mkono

Na siaijii kaamua liwe liwalo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rejea kichwa cha habar hapo juu cha husu neno `DHAIFU' huu mkanganyiko hata humu wanabodi mnachanganya mambo, tutofautishe kati ya taasisi , mhimili NA MTU binafsi. CAG alilenga mhimili wa bunge , kwahyo CAG alikosea kutamka mhimili flani ni dhaifu. Nani kampa hayo mamlaka ya kufanyia tathmini bunge ? Nanyi humu mnashagilia! Kama VP mjiite nyie wenyewe neno DHAIFU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu sisi kila siku tunaitwa wanyonge mbona hatununi? dhaifu ni synomy ya nyonge hivyo yana maana sawa.
 
Rejea kichwa cha habar hapo juu cha husu neno `DHAIFU' huu mkanganyiko hata humu wanabodi mnachanganya mambo, tutofautishe kati ya taasisi , mhimili NA MTU binafsi. CAG alilenga mhimili wa bunge , kwahyo CAG alikosea kutamka mhimili flani ni dhaifu. Nani kampa hayo mamlaka ya kufanyia tathmini bunge ? Nanyi humu mnashagilia! Kama VP mjiite nyie wenyewe neno DHAIFU.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1073230
 
Bunge ni dhaifu na Ndugai ni dhaifu zaidi.
 
Rejea kichwa cha habar hapo juu cha husu neno `DHAIFU' huu mkanganyiko hata humu wanabodi mnachanganya mambo, tutofautishe kati ya taasisi , mhimili NA MTU binafsi. CAG alilenga mhimili wa bunge , kwahyo CAG alikosea kutamka mhimili flani ni dhaifu. Nani kampa hayo mamlaka ya kufanyia tathmini bunge ? Nanyi humu mnashagilia! Kama VP mjiite nyie wenyewe neno DHAIFU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ninyi ni baadhi ya wajinga wachache mnao mjaza ujinga spika na bunge lake

udhaifu upo popote pale na taasisi yeyote ile yaweza kuwa dhaifu kama haitekelezi wajibu wake ipasavyo na jina hilo limeitwa kwenye taasisi nyingi tena zingine zimeambiwa mazito zaid ya hilo la udhaifu

Ni ujinga na uwendawazimu nchi nzima kuhangaika na jambo jepesi kama hili na kuacha mambo ya msingi yenye manufaa kwa taifa
 
Rejea kichwa cha habar hapo juu cha husu neno `DHAIFU' huu mkanganyiko hata humu wanabodi mnachanganya mambo, tutofautishe kati ya taasisi , mhimili NA MTU binafsi. CAG alilenga mhimili wa bunge , kwahyo CAG alikosea kutamka mhimili flani ni dhaifu. Nani kampa hayo mamlaka ya kufanyia tathmini bunge ? Nanyi humu mnashagilia! Kama VP mjiite nyie wenyewe neno DHAIFU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja:TAASISI STRONG HAIWEZI CHAGUA KIONGOZI DAHAIFU.Pili: Muhimili wa Bunge,Muhimili wa mahakama na Muhimili ule uliojichimbia chini-wote boss wao ni wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaitwa WANYONGE au DHAIFU na wanapiga vigelegele kweli,sasa sijui bunge linaundwa na watu wa nchi gani? Tatu:-Kama bunge kama taasisi halina uwezo wa kufanya kazi zake basi ni dhaifu.
 
Rejea kichwa cha habar hapo juu cha husu neno `DHAIFU' huu mkanganyiko hata humu wanabodi mnachanganya mambo, tutofautishe kati ya taasisi , mhimili NA MTU binafsi. CAG alilenga mhimili wa bunge , kwahyo CAG alikosea kutamka mhimili flani ni dhaifu. Nani kampa hayo mamlaka ya kufanyia tathmini bunge ? Nanyi humu mnashagilia! Kama VP mjiite nyie wenyewe neno DHAIFU.

Sent using Jamii Forums mobile app
Usilete siasa kwenye taaluma, muulize CAG sababu za kusema hivyo, au muulize daktari aliyekupima kusema wewe Ni mgonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wewe ni kiwete tegemea kuitwa kiwete, na huo ndio ukweli wala hakuna tusi hapo.
 
Kiukweli katiba yetu ina upungufu inaitaji marekebisho ya haraka.There is great need for separation of powers of 3 pillars.Spika hatakiwi awe kada wa chama chochote.Haiwezekani referee wa kuchezesha mpira Simba na Yanga akatoka klabu mojawapo .akajifanya referee mzuri hapo impartiality hatakuwepo daima malalamiko hayataisha ikiwa nchi yetu itakazania kutumia katiba ya sasa iliyotungwa kwa mfumo wa chama kimoja.Hata hii iliyopo inakuwa abrogated je ni mfumo hupi wa uongozi tunaufuata?
 
Mku naona hukunipata vizuri hoja yangu. Nachosema ni hivi neno Udhaifu ni kawaida sana kama amekagua tasisi akakuta mapungufu na ndo madhaifu ya kuyafanyia kazi. Na kwa mantiki hiyo Prof.Assad anakuwa sahihi.
Lakini kama mimi hujaja kunikagua katika uwanja au eneo husika, huwezi kunambia kwamba nina udhaifu katika eneo hilo hapo ni tusi kwangu. Mana ukisema nina udhaifu katika ukaguzi, lazima uwe na vielelezo jinsi navyo paswa kufanya kazi na hali halisi ulioikuta wakati waukaguzi.
Ndo maana nkauliza, kwani ripoti ya CAG ya ukaguzi kuhusu Bunge, iliyasema humo ndani ya ripoti yake au aliona aende kuyasema huko kwa Wazungu?
Kaka naona hukuelewa udhaifu unaozungumziwa si kwamba ukaguzi wa bunge ulifanyika na kukutwa udhaifu,udhaifu aliousema CAG ni ule ambao bunge limeshindwa kuisimamia serikali katika kuhoji matumizi ya fedha za kodi za wananchi.Bunge linapaswa kuihoji serikali kila senti iliyokusanywa imetumikaje.ndio wajibu wake KUISIMAMIA.
 
Back
Top Bottom