CAG Vs SPEAKER: Mgogoro usio wa lazima

kimantiki CAG alisema "udhaifu wa bunge"

lakini kiuhalisia alimaanisha "udhaifu wa spika"

na udhaifu ni pale anapomsukumia CAG kwa rais ambapo kwa 'udhaifu wa katiba' cag hajielezi kwa yeyote
 
Ndugu Wanajamii,
Sina shaka weekend yenu imekua mwanana na mmejipanga na kuanza juma jipya.
Na imani mmeshaskia mengi juu ya mvutano kati ya CAG na kiongozi wa taasisi ya bunge sio nia yangu kuwachosheni wala kuegemea upande wa nani ni sahihi nani kakosea. Tukirudi kwenye kiini cha mzozo,ile kauli aliyotoa CAG kwamba kwa bunge kushindwa kuisimamia serikali imeonyesha udhaifu,je haikua busara kwa speaker kui counter hiyo kauli kwa kutoa vielelezo namna ambavyo bunge lake limeisimamia serikali ipasavyo ili CAG aonekane muongo na mdhalilishaji?kwangu mimi naamini hoja hujibiwa kwa hoja na si jazba wala mihemko.
Speaker hajachelewa nimuombe iwapo atasoma ujumbe huu au mtu wa karibu wa kumfikishia atumie busara ndogo tu yakuonyesha maeneo ambayo bunge limeisimamia serikali ipasavyo contrary to what CAG is accusing it for kwa kufanya hivyo atajijengea heshima yake,ya bunge tukufu na atamnyamanzisha Prof.Assad kwa hoja.
Naomba kuwasilisha.
REKEBISHA KICHWA, ONDOA CAG V/s SPEAKER, KELELE ZILIZOPO NI ZA UPANDE MMOJA WA SPEAKER, CAG HAYUMO KWENYE MALUMBANO.
 
Wanaomdharau Ndungai wanamdanganya Assad kile kichwa kitaliwa soon. Huyu Assad mswahiliswahili sana.

Kwa taarifa yako huyo CAG hanyenyekei hicho cheo maana ana uwezo wa kupata kazi popote dunia hii. Mtu wa kutetemekea cheo ni bashite maana yeye hana vyeti. CAG kafanya kazi yake na wananchi tumeona, bunge tu ndio limebaki kujipendekeza kwa jiwe.
 
Wanaomdharau Ndungai wanamdanganya Assad kile kichwa kitaliwa soon. Huyu Assad mswahiliswahili sana.
Mswahilswahili??? udhaifu wabunge na bunge dhaifu ni kauli mbili tofauti. Bunge limeoverreact na kuweka siasa kwenye neno la kitaaluma ambalo naamini lilitumika hivyo na si kwa maana ya lugha ya kawaida
 
Handshake ya Uhuru na Raila imeleta mabadiliko makubwa saana nchini Kenya na sasa wanazungumza lugha moja kwa capital letters.
Namuomba Mwenyezimungu atujaalie tuungane sooote tuwe kitu kimoja na tumuombe yeye muumba wa nchi na mbingu atujaalie na sisi tuwe na a very good hand shake kwa maendeleo ya nchi yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wana JF nimejaribu kufuatilia ubishi wa wakubwa hawa wawili naona wao wameamua kutuchang'anya sisi wananchi wakawaida ili wasikie ya kwetu.
Kwanza, CAG anadai neno "udhaifu" nilakawaida katika taarifa ya ukaguzi kuhusu mahesabu ya kiuhasibu. Sawa hapo mimi sijabisha.
Tatizo langu ni kwamba, kama katika mahesabu yaliyokaguliwa na CAG na kutoa ripoti yake ya juzi, hakuna neno "Bunge ni dhaifu" ina maana alivyosema kule nje ya nchi alikua anasengenya Bunge. Na kama hili neno linaloleta ubishi kwa Mheshimiwa lipo ndani ya Ripoti basi CAG atakuwa sawa kwamba kule nje ya nchi hakuwasengenya. Wale muliorusha vipande vya ripoti ya CAG nitafutieni hicho kipande mukirushe hapa JF.
Haiwezekani kwenye ripoti uwasifie lakini kule kwa wazungu uwaite Dhaifu.
 
Ndugu Wanajamii,

Sina shaka weekend yenu imekua mwanana na mmejipanga na kuanza juma jipya.

Na imani mmeshaskia mengi juu ya mvutano kati ya CAG na kiongozi wa taasisi ya bunge sio nia yangu kuwachosheni wala kuegemea upande wa nani ni sahihi nani kakosea. Tukirudi kwenye kiini cha mzozo,ile kauli aliyotoa CAG kwamba kwa bunge kushindwa kuisimamia serikali imeonyesha udhaifu,je haikua busara kwa speaker kui counter hiyo kauli kwa kutoa vielelezo namna ambavyo bunge lake limeisimamia serikali ipasavyo ili CAG aonekane muongo na mdhalilishaji?kwangu mimi naamini hoja hujibiwa kwa hoja na si jazba wala mihemko.

Speaker hajachelewa nimuombe iwapo atasoma ujumbe huu au mtu wa karibu wa kumfikishia atumie busara ndogo tu yakuonyesha maeneo ambayo bunge limeisimamia serikali ipasavyo contrary to what CAG is accusing it for kwa kufanya hivyo atajijengea heshima yake,ya bunge tukufu na atamnyamanzisha Prof.Assad kwa hoja.

Naomba kuwasilisha.
Likewise, na CAG angetoa mifano yakutosha jinsi Bunge lilivyoshindwa kuisimamia Serikali ili Spika ajidefend kwakutumia mifano hiyohiyo. Hapo tutawaelewa.
 
Wana JF nimejaribu kufuatilia ubishi wa wakubwa hawa wawili naona wao wameamua kutuchang'anya sisi wananchi wakawaida ili wasikie ya kwetu.
Kwanza, CAG anadai neno "udhaifu" nilakawaida katika taarifa ya ukaguzi kuhusu mahesabu ya kiuhasibu. Sawa hapo mimi sijabisha.
Tatizo langu ni kwamba, kama katika mahesabu yaliyokaguliwa na CAG na kutoa ripoti yake ya juzi, hakuna neno "Bunge ni dhaifu" ina maana alivyosema kule nje ya nchi alikua anasengenya Bunge. Na kama hili neno linaloleta ubishi kwa Mheshimiwa lipo ndani ya Ripoti basi CAG atakuwa sawa kwamba kule nje ya nchi hakuwasengenya. Wale muliorusha vipande vya ripoti ya CAG nitafutieni hicho kipande mukirushe hapa JF.
Haiwezekani kwenye ripoti uwasifie lakini kule kwa wazungu uwaite Dhaifu.

Huoni au kuwaza kuwa waweza kuwa dhaifu/sipika kama CAG alivyodai?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona kama hizi mada zinajirudia tu toka hili jambo litokee. Ushauri wangu wakampime mkojo kama walivyotaka kumpima TL madai kama haya sio bure!
 
Back
Top Bottom