CAG Vs SPEAKER: Mgogoro usio wa lazima

Feb 18, 2019
14
30
Ndugu Wanajamii,

Sina shaka weekend yenu imekua mwanana na mmejipanga na kuanza juma jipya.

Na imani mmeshaskia mengi juu ya mvutano kati ya CAG na kiongozi wa taasisi ya bunge sio nia yangu kuwachosheni wala kuegemea upande wa nani ni sahihi nani kakosea. Tukirudi kwenye kiini cha mzozo,ile kauli aliyotoa CAG kwamba kwa bunge kushindwa kuisimamia serikali imeonyesha udhaifu,je haikua busara kwa speaker kui counter hiyo kauli kwa kutoa vielelezo namna ambavyo bunge lake limeisimamia serikali ipasavyo ili CAG aonekane muongo na mdhalilishaji?kwangu mimi naamini hoja hujibiwa kwa hoja na si jazba wala mihemko.

Speaker hajachelewa nimuombe iwapo atasoma ujumbe huu au mtu wa karibu wa kumfikishia atumie busara ndogo tu yakuonyesha maeneo ambayo bunge limeisimamia serikali ipasavyo contrary to what CAG is accusing it for kwa kufanya hivyo atajijengea heshima yake,ya bunge tukufu na atamnyamanzisha Prof.Assad kwa hoja.

Naomba kuwasilisha.
 
Mheshimiwa Spika jana kwenye mkutano wake alitumia maneno mengi ya kumkejeli Professor na kuonyesha bado ana hasira nae mpaka kufikia kumshauri ajiuzuru.

Kana kwamba haitoshi alimwingiza Raisi kwenye hilo jambo akidai "Professor asimpe shida Raisi". Bahati nzuri si rahisi kumfukuza CAG labda watumie ubabe.

Utamu wa mkutano wake ni pale alipojaribu kumtenganisha CAG na Assad. Sioni kama hili linawezekana kwani bila Assad kuidhinisha report itoke sioni itatokaje, yeye ndiye mwenye dhamana.

Anasema field wanaokwenda huko sio Assad anasahau Assad ndiye msimamizi wa hiyo offisi na ndiye mwenye offisi-ukimgomea ina maana reporti zake pia utazigomea jambo ambalo hata supika anajua haliwezekani.

Sana sana aseme hataongea na professor hilo linawezekana lakini sio kutofanya kazi nae.

Wenye kufahamu wanajua, reporti ya CAG ikishatua bungeni, ni lazima bunge liifanyie kazi lipende lisipende labda wabadilishe vifungu husika.

Kuendelea kung'ang'ana na Professor ni udhaifu mwingine wa supika na hao wanao muunga mkono.
 
Hawamtaki kwasababu sio mtu wao, wamefukuza watu wa viongozi waliopita kwa kisingizio ni mafisadi na wakaweka watu wao. sasa huyu analindwa na katiba, wamemkosa kwenye uadilifu wanataka kumfukuza kwa nguvu.
Wasifanye kazi naye mpaka muda wake utakapoisha. Au wamrudishe kule walikomtoa kabla, au wasubiri muda ufike walete mtu wao.
Ajiuzuru ili iweje? hajashindwa kufanya kazi yake, sasa sababu ya kujiuzuru itakuwa ni ipi?
 
Speaker hajachelewa nimuombe iwapo atasoma ujumbe huu au mtu wa karibu wa kumfikishia atumie busara ndogo tu yakuonyesha maeneo ambayo bunge limeisimamia serikali ipasavyo contrary to what CAG is accusing it for kwa kufanya hivyo atajijengea heshima yake,ya bunge tukufu na atamnyamanzisha Prof.Assad kwa hoja.

👆🏻Hicho ndicho Spika alitakiwa afanye hapo kabla kuliko kudhamiria kutumia mabavu ya Bunge (azimio) ambayo hayakuhitajika kabisa.

Lakini wenye akili wameng'amua jambo kwamba; kuna matumizi mabaya sana ya fedha za umma katika awamu hii ya 5 ya uongozi na CAG kasimama kidete kubainisha hizo corruptions ndipo hapo alipotengeneza UBAYA hasa na "serikali" na siyo Bunge kama jinsi tuonavyo, Bunge linaikingia serikali kifua na ndiyo maana Spika anataka CAG ajiuzulu na anasema maneno ya ajabu kwamba " CAG anampa taabu sana Rais" kana kwamba leo Spika kawa msemaji wa Raisi!!!🤔🤔

Kuna nini behind the scene??!.
 
Spika ndugai kapewa assignment na jiwe kuhakikisha CAG anajiuzuru, maana inaonekana CAG sio mtiifu kwa jiwe na kwa mujibu wa jiwe hawezi tumbuliwa na jiwe, kumbuka jiwe anataka kulipa kisasi kwa.Asad kwa kuonyesha uovu wa jiwe hadharani toka akiwa waziri, kwa hiyo unatafutwa upenyo wa kumlazimisha anajiuzuru kwa hiari maana kumtumbua haiwezekani, sasa kwa vile ndugai anataka kuendelea kuwa spika tena japo anaweza kugeuziwa kibao kama sita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ya CAG ni kuibua wizi na ufisadi na kuleta bungeni ili hatua zichukuliwe. Maana halisi ni kuwa CAG ndio jicho letu wananchi na Bunge ni meno ya kung'ata waovu hao.
Bunge halitaki kushirikiana ( wabunge wa CCM) na CAG na zaidi tuseme Ndugai ndio halitaki jicho letu, na yeye Assad kasema anaibua mambo lakini hayatekelezwi kutokana na "udhaifu wa Bunge".
Sasa tunajiuliza kama wote hao tumewaajiri sie wananchi jee nani AJIUZULU?.
Tunamtaka Ndugai ajiuzulu mara moja kwa kulifanya Bunge letu dhaifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaomdharau Ndungai wanamdanganya Assad kile kichwa kitaliwa soon. Huyu Assad mswahiliswahili sana.
 
Angekuwa mswahili asingefika level hizoaizonazo mpaka kuminiawa na UN kukagua mahesabu yao. Licha ya kuaminiwa na nchi. Ni dhamana kubwa.. hapewi mwanasiasa hiko cheo. Ndio maana CAG sio kada. Assad anasimamia ukweli .. na ukweli unauma.
Wanaomdharau Ndungai wanamdanganya Assad kile kichwa kitaliwa soon. Huyu Assad mswahiliswahili sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom