CAG: Uwanja wa Ndege Chato ni mradi usio na faida

Hivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Vichaa dalili zao nyingi, Kichaa hagombani na kichaa mwenzie
 
Tofauti ni kuwa viwanja vya Musoma na Mtwara vimejengwa miji mikuu ya mikoa sehemu ambazo kuna watu na biashara nyingi wakati uwanja wa Chato umejengwa kijijini kwenye watu wachache ni biashara chache!

Tunakwenda kuwa Mkoa wa Chaatooo weka akiba ya maneno yatakusaidia mbeleni
 
Kabisa, yaani Sasa hivi Kuna magofu ya bilioni 11 kwenye mapori
Mama katumia billion 11 kurekodi royal tour,sinibora magufuri aliyekeza kwenye hotel maana kuna watu watapata ajira,kuliko huyu Mama aliyewapelekea wazungu ajira,huyu Mama bure kabisa
 
Hivi uwanja wa ndege wa Chato unatofauti gani na Uwanja wa Ndege wa Musoma unaojengwa? Au wa Mtwara? Hizo faida anazotaka CAG ni zipi? Zionekane baada ya mda fani? Maana nina hakika ata ujenzi wa terminal 3 Mwaimu Nyerere bado hatujaanza kupata faida

Sent using Jamii Forums mobile app
Tofauti iliyopo ni uwanja wa ndege wa Musoma na Mtwara ni viwanja ambavyo vilikuwepo na vimekuwa vikitoa huduma kwa muda flani hivyo kutokana na mahitaji ya wateja ya sasa ikaonekana kuna haja ya kuboresha / kujenga baada ya kufanya upembuzi yakinifu ambao unatoa mwongozo wa nini cha kufanya. Uwanja wa ndege wa Chato ni mpya kabisa ambapo ujenzi umefanyika huku wataalam wakiangalia hali ya wateja itakuaje, na concern za CAG ni hakukuwa na upembuzi yakinifu na kupelekea kutumia fedha zaidi ya bajeti kitu na pia fedha zilizotumika kujenga uwanja wa Chato zilichukuliwa kwenye miradi mingine ili baadae zirudishwe pindi ela iliyopangwa kujenga Chato itakapotoka, hata hivyo fedha zilikuwa hazirudishwi kwa wakati na zingine hazikurudishwa kabisa.

Kimsing CAG yeye anafanya kazi yake ya kuangalia taratibu za kihasibu na manunuzi hivyo sio kama yeye anataka hizo faida (tusimwone mbaya kwa hizi headings tunazosoma kwenye vyombo vya habari)
 
Back
Top Bottom