CAG: Upotevu wa trilioni 1.5 Watanzania mjue sio jukumu langu kuchukua hatua, mie natekeleza majukumu yangu tu

Elewa wewe,kwenye ripoti yake amesema hizo pesa hazina maelezo ya namna zilivyotumika.Kwahiyo haieleweki zimefanya kazi gani,kwa utaratibu hakuna hata shilingi moja inayopaswa kutumia bila viambatanisho kuwekwa wazi,Kwahiyo kilichofanyika ni ukiukwaji wa utaratibu.Sasa utaamua wewe jambo hilo kulipa jina utakalolipenda.
Hahahaha!!!!!umesomeka mubasharaaa!!!hakuna janja janja ya kupindua maneno.....kasema hazionekani hakusema zimeibiwa,Mfano rahisi umekuasanya shilingi Elfu 1000....umetumia shilingi 800....imebaki shilingi 200.....lkn Balance Bank inasoma zero.....sasa Mia 200 imeenda wapi?
 
nikipata kauli yake baada ya ile ya hakuna pesa iliyoibiwa na baada ya maelezo ya serikali akiindorse report yake au akiunga mkono ufafanuzi mpya itapendeza. bado hakuna msawazo mzuri kutoka pande zote mbili kama sio tatu.

Ukishasikia kuna hela zimetumika bila vielelezo unataka mpaka uambiwe zimeibiwa, huwezi kujiongeza? Huyo CAG kasinamamishwa na kuulizwa aliye juu ya sheria ulitegemea aseme zimeibiwa? Kwani yy hajaona kilichompata Lissu? Haoni hao wanaoelea kwenye viroba pwani? Acha hizo bana.
 
Slow slow alisema hyo 1.5 t haijaiva,ikiiva mtaiona tu,hvyo kuweni na subira!!
 
Watanzania wengi hawana Elimu..Ujinga bado haujaisha kabisa Hayati baba wa Taifa alilisema hili janga la UJINGA. Mungu saidia kufuta UJINGA nchini..Wasomi gani wamekaa kimya huko vyuoni hawawezi kuonesha Baba/Mama/Ndugu 1.5 Trillion IPO/HAIPO?
 
sakata_la_trilioni_15_cag_atoa_msimamo_wake_h16185_2e3d0.jpg



Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG, Prof. Mussa Assad amefunguka kufuatia majadaliano yanayoendelea nchini juu ya trilioni 1.5 amabzo zinadaiwa kutofahamika zimetumika katika shughuli gani yake ametoa msimamo wake kwa kutanabaisha kwamba anajali zaidi majukumu yake na kudai kwamba hatumii utashi binafsi au kufuata maoni ya mtu yeyote bila kujali nafsi yake.

Amesema ataendelea kutekeleza wajibu wake kwa weledi huku akizingatia sheria za nchi na kuutaka umma wa Watanzania utambue kuwa si jukumu lake kuchukua hatua juu ya suala hilo mara baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa mamlaka husika.

Aidha, Chama cha Kijamii cha (CCK), kimesema hakihitaji hesabu za magazijuto katika kukokotoa upotevu wa Trioni 1.5 zilizoibuliwa na Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe baada ya kuchambua ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG, Prof. Mussa Assad.

CCK kimeongezea kuwa, CAG amemaliza kazi yake kwa mujibu wa sheria, ni wajibu sasa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuipitia na kutoa majibu kwa kutumia busara zao ili suala hilo lijibiwe na serikali kwa kina na sio kwa viongozi wa Serikali kutoa majibu mepesi kama ambavyo yamekuwa yakitolewa toka kuibuliwa kwa suala hilo.
Mambo hadharani mwaka huu
 
Back
Top Bottom