Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ameyataja makampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Shirika la Ndege Tanzania (ATC) kuwa yana idadi kubwa ya wafanyakazi ambao elimu yao ni darasa la saba.
Alisema hayo jana wakati akitoa mafunzo kwa kamati nne za Bunge juu ya mambo ambayo wanatakiwa kuhoji wanapokuwa kwenye vikao vya bajeti yanayohusu ripoti za CAG.
Akizungumzia kuhusu ATCL na TTCL, Profesa Assad alisema mashirika hayo yamekuwa hayana faida kwa Serikali zaidi ya kuitia hasara ya kulipa wafanyakazi mishahara wakati hakuna kazi zinazofanyika.
Alisema matatizo yanayokabili mashirika hayo ni ukosefu wa mitaji na kuwa na waajiriwa ambao wana uelewa mdogo hivyo kushauri yafutwe.
“Mfano hili shirika la TTCL halina faida yoyote kwenye nchi hii kwa zaidi ya miaka 10 sasa, watu wanalipwa mishahara lakini hakuna kinachofanyika, ukienda pale asilimia kubwa ya wafanyakazi ni darasa la saba” alisema na kuongeza kuwa lilitakiwa lisiwepo kabisa lakini limekuwa linavumiliwa na wakati huohuo na wabunge wapo.
“Naongea haya nikiwa ninajiamini kwa sababu ninayafahamu vizuri... ATC ina ndege mbili tu lakini ukienda pale kuna wafanyakazi zaidi ya 300 wote wanalipwa mishahara hakuna kodi inayopatikana pale.”
Profesa Assad alisema hata hizo ndege mbili zilizopo nazo hazifanyi kazi na kwamba shirika hilo lilitakiwa kuwa na wafanyakazi wachache na ofisi mbili tu.
Wabunge wanena
Baadhi ya wabunge wamisema kuna mashirika mengi na taasisi ambazo haziridhishi katika utendaji lakini bado zinalelewa. Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Raisa Abdallah Mussa alisema mashirika hayo mara nyingi yanapohojiwa kuhusu utendaji wao yanadai kupewa bajeti ndogo na Serikali.
“Tumejaribu pia kuhoji juu ya mashirika haya likiwamo la ATC wanadai bajeti wanazopewa na Serikali kuendesha mashirika zinakuwa hazikidhi mahitaji na haziji kwa wakati ndiyo maana zinashindwa kujiendesha” alisema.
Source: TTCL, ATCL kumejaa ‘vihiyo’