Cag sasa tumechoka kila siku ubadhirfu;usikubali kuwa msukule wa rais;tunaitaji watu waende ndani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cag sasa tumechoka kila siku ubadhirfu;usikubali kuwa msukule wa rais;tunaitaji watu waende ndani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Apr 30, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,464
  Likes Received: 5,707
  Trophy Points: 280
  JAMANI HUYU RAIS KIKWETE YUPO DUNIAN AMA NDIO KASIMAMA PALE KIVUKON KAMA MSUKULE WA CCM HIZI TAARIFA ZA CAG KILA SIKU ANA KUJA NA MABILION YAMEPOTEA MABILION YAMELIWA WANAAOKULA WAKOWAPI AWAKAMATWI JAMANI AIIII CAG EMBU PUMZIKA JAMAN WASIKUFANYE NAWE MSUKULE WAO WAJIONYESHE WALIKUWA SIRIASI HUU UPUUZI IMETOSHA MREMA ANAPITA KILA MKOA ANKUTA MANISPAA OOH HALMASHAURI ZIMETAFUNA MILLION 500/MARA MORO 450 TENA ZA MAREHEMU WALIOKUFA WANALIPWA MSHARA AKUNA KINACHOFANYIKA MNATUMBIA ILI IWE NINI TUKAFUE MIFUPA KAMA MNATANGAZA AMFANYII KAZI KAENI KIMYA NA KAMA MNAONA RIPOTI ZENU AZIFANYIWI KAZI WAAMBIEN WALIOWACHAGUA IMETOSHA MPAKA WALIOTAJWA WALIPE HELA ZA WALIPA KODI AMUWEZI FANYA WATANZANIAA MISUKULE KIASI HIKI JAMANI KILA GAZETI KILA SIKU CAG KATOBOA HIKI MREMA KAFUMUA HIKI KINACHOFANYIKA NININI??CHA AJABU KULE ROMBO ATI MREMA ANASEMA WAHASIBU WAMEOINEKANA WAMEIBA MILLION 490 WAKATWE KWENYE MISHAHARA HUU SIO UPUUZI KAMA KUTAKA KUJIONYESHA KWA WATU WANA LIPWA SH NGAPAI WAKATWE KWA MUDA GAN AMA WAKATWE NA WAJUKUU ZAO WANAOSUBIRIWA KUZALIWA...HII DUNIA FEKI TUPU JAMANI TWENDE WAPI SASA...KULE TEGETA WAMAKAMATA MAJUZI WACHINA WAMETENGENEZA SABUNI FEKI ZA CHAPA YA OMO WAKIDAI ZINATOKA CHINA ..WALE JAMAA WAKAENDA NA LANDCRUISER NA JAMAA WA LIOKUJA KUCHUNGUZA ZILE SABUNI MAMILION

  USIKU WANAKUJA KUPAKUA MZIGO MALORI KWA MALORI TENA YAKISIMAMIWA NA POLISI ZAIDI YA TANO WAKIWA NA MITUTU YA BUNDUKI...KESHO YAKE MCHANA WANARUDI NA KUJIFANYA WANASHANGAA MIZIGO IMEKWENDA WAPAI JAMANI HIZIZ LAANA HIZI TUTAENDA WAPI NA KIPIGO CHA MUNGU JAMANI???KWELI SABUNI NGAPOI ZA KLEIN ZIKO MJINI FEKI NA LEO HII UNAKAMATA MTU ANAKUPELEKA SEHEMU UNARUDI KUTANGAZA MZIGO AUPO NA WAMEKAA KIMYA... ATUTAKI TENA HIZI SHIT ZENU JAMANI KAMA MNATANGAZA FWATILIEN KIMEENDELEA NINI


  KESI YA EPA INAYOMUHUSU YULE FISADI MAANDA HAKIMU KALA KONA JAMANI HUU UPUUZI MPAKA LINI NA TUNAVYOENDELEA UTASIKIA AMEJITOA WAKATI LEO ILIKUWA SIKU YA HUKUMU HUU UPUUZI UNAENDELEA HII NCHI SERIKALI IKO WAPI JAMANI?? TUKIANDAMANA KWA MAKOSA YA KIPUMBAVU KAMA HAYA WATU WAJIREKEBISHE UNAAMBIWA UPINZANI JAMANI JAMANI TUNAELEKEA WAPI??

  GAZETI LA LEO LIMETANGAZA MANISPAA YA TEMEKE WAMENUNUA SHANGINGI LA MILLION 200 JAMANI NA DOCS ZIMEKAMATWA UTASIKIA KESHO AMEKULA PANYA DOCUMENTS ZOTE USHAHDI UMEKWISHA..TWENDE WAPI KUJINUSURU NA ADHABU YA MUUMBA


  CAG abaini ufisadi wa Sh50 bilioni serikalini Send to a friend Saturday, 30 April 2011 10:00 0diggsdigg

  [​IMG]Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),Ludovick Utouh

  Boniface Meena
  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini ufisadi wa Sh50.6 bilioni serikalini ukiwamo wa malipo yanayotia shaka ya Sh15.7 bilioni katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010.

  Katika ripoti yake ya ukaguzi iliyoishia Juni, 30, 2010, CAG amesema fedha nyingi zilitumika kufanya ununuzi bila kufuata taratibu.

  Katika ripoti yake, amesema wizara, idara, wakala na sekretarieti za mikoa, zilitumia fedha katika kipindi cha mwaka 2009/2010 kufanya ununuzi ambao haukuwa kwenye mpango wa mwaka.

  Alisema matumizi hayo ni kinyume cha kifungu cha 45 cha Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004 kinachozitaka taasisi za ununuzi kuweka mpango wa mwaka kwa lengo la kuepuka ununuzi wa dharura, kupata thamani ya fedha, kupunguza gharama za matumizi na kufanya ununuzi sahihi kwa njia ya kandarasi.

  "Ukaguzi umebainisha kwamba katika mwaka wa fedha 2009/2010, taasisi zilizoonyeshwa hapa chini zilifanya ununuzi yenye thamani ya Sh50.6 bila kufuata kifungu cha sheria," imeeleza sehemu ya ripoti hiyo.

  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kati ya fedha hizo, Sh650.7 milioni zilitumika katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, kununulia samani kwa maofisa wanaoishi katika nyumba binafsi

  Wizara nyingine ni Nishati na Madini, Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Maliasili na Utalii, Habari, Vijana na Michezo na Tume ya kurekebisha Sheria.

  "Ununuzi wa samani kwa maofisa hao ulikuwa si sawa kwa kuwa hawana stahili ya kununuliwa vitu hivyo na ni kinyume cha waraka wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (Utumishi) Na. C/CA/134/213/01/G/69 wa Januari 30, 2006, unaohusu malipo ya posho ya nyumba na ununuzi wa samani kwa nyumba za Serikali kwa maofisa wenye stahili," imesema ripoti hiyo.

  CAG ameeleza pia kuwa eneo jingine ambalo fedha hizo zimetumika vibaya ni matengenezo ya magari ya serikali na taasisi zake ambako Jumla ya Sh176.7 milioni zimeliwa.

  Alisema wakati kanuni ya 5 ya Kanuni za Ununuzi wa Umma (mali, kazi, huduma zisizo za ushauri na uuzaji wa mali ya umma kwa zabuni) ya mwaka 2005, ikitaka wizara, idara, wakala na sekretarieti za mikoa kutengeneza magari yake Temesa (Wakala wa Ufundi na Umeme), au kupeleka katika karakana zilizoidhinishwa na wakala huyo, magari mengi yalikuwa yanatengenezwa kwenye karakana binafsi.

  "Magari hayo yametengezwa kwenye karakana hizo bila kuwa na kibali kutoka Temesa kama sheria inavyotaka."

  CAG amebaini pia kuwa serikali na taasisi zake imetumia Sh13.8 bilioni kulipia mali na vifaa ambavyo hata hivyo, havikupokewa au vilipokewa pungufu.

  "Hii ni kinyume na kanuni ya 122 ya kanuni za Ununuzi ya Umma (mali, kazi, huduma zisizo za ushauri na uuzaji wa mali ya umma kwa zabuni) ya mwaka 2005," alisema.

  Taarifa hiyo ilisema katika kipindi cha mwaka wa fedha 2009/2010, wizara, idara, sekretarieti za mikoa mitatu zilifanya malipo yenye shaka yanayofikia Sh15.7 bilioni.

  Malipo hayo yalikosa viambatanisho ambavyo vingeonyesha taarifa za kina pasipo kuacha shaka yoyote kuhusiana na usahihi wa malipo hayo.

  MH CAG AHSANTE KWA KAZI NZURI ILA SASA HIVI SITISHA UCHUNGUZI WAKO EMBU FWATILIA TOKA UANZE KUTAJA UBADHIRIFU WAMEFANYA NINI NA UOMBE MAMLAKA YA KUPELEKA WATU MAHAKAMANI KAMA POSSIBLE ILA KUENDELEA KUTANGAZIANA MTARUDIA MABO YA EPA
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  hata mie nashangaa maneno kibao tu huyu CAG lkn meno hana aaaagh
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,646
  Likes Received: 82,373
  Trophy Points: 280
  Kila mwaka anaibua tuhuma nzito za matumizi mabaya ya mabilioni ya pesa za walipa kodi ambazo zimetumika bila kufuata taratibu zilizowekwa au hakuna ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha kwamba matumizi hayo kweli yamefanyika. Cha kushangaza kila mwaka hakuna anayewajibishwa na ufisadi huo katika Wizara, Balozi zetu nchi za nje, Ofisi ya Rais, Ofisi ya waziri Mkuu, Mikoa na Wilaya mbali mbali.
   
 4. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  jamani mjue kazi za auditor ni kutoa ripoti tu, hukumu inatolewa na watu wengine, si kazi yake kufukuza mtu kazi au kumpeleka polisi au vinginevyo
   
 5. kussy

  kussy JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Jun 15, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  jamani mjue kazi za auditor ni kutoa ripoti tu, hukumu inatolewa na watu wengine, si kazi yake kufukuza mtu kazi au kumpeleka polisi au vinginevyo
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mwizi akishakajulikana dawa yake kumweka ndani yeye cag kila siku analeta story za wizi lkn hamna hatua zozote wanazochukuliwa hao anaodai ni wabadhirifu. Wakati umefika wa kuwachukulia hatua na siyo maneno maneno kila siku.
   
Loading...