CAG, Prof. Mussa Assad, Atoa Dawa ya Kutibu Ugonjwa Hatari wa Deni la Taifa, ni Nidhamu ya Matumizi kwa Kubudget Kutumia Kile tuu Tutachokipata

PROF. ASSAD HII HADITH YA MTUME (SAW) UNAIJUA ?.

Na Bashir Yakub.

Mtu mmoja alimuuliza Mtume swallah llahu 'alayhi wasallah

“Ipi ni jihad(harakati) bora?” Mtume Akasema:

“Maneno ya haki mbele ya Mtawala muovu”

Kwa maneno mengi ya Assad ni wazi kwake kwamba Magufuli alikuwa mtawala muovu.

Assad haya maneno unayoita ya haki unayobwabwaja kila sehem mda huu uliwah kuyatoa mbele ya mtawala muovu.

Wakati akiwa hai na we si ulikuwa hai, ulishindwa nini kuyatamka mbele yake ili ukawa katika wale waumini wa kweli aliowasema Mtume katika hii Hadith ambao husema kweli.

Unakula nyama ya mfu kwa confidence, unajitutumua leo hayupo halafu unajifanya muumini.

Ina maana ulimuogopa kuliko unavyoogopa haya maneno ya Mtume Mtukufu . Iko wapi imani yako.

Unasubiri kufanya harakati juu ya mwili wa mfu.

Umeingia katika wanafiki wakubwa, watu waoga, na kada ya wasomi wasiojiamini.

Kama hukumwambia yeye hakuna haja ya kutwambia sisi. Unatwambia tumwajibishe nani sasa, kaburi lake ama familia yake.

Umbweha ni tabia ovu sana.
Mkuu Bashir Yakub , kwanza asante kwa hii. Vipi uliwahi kumsikia Prof. Asad hapa?.
Msikilize kwa makini sana, na maneno haya tena aliyasema akiwa CAG

P.
 
Wanabodi,
Moja ya ugonjwa mkubwa na mbaya kuliko magonjwa yote yanayolikabili taifa letu, ni ugonjwa wa kukua kwa deni la taifa, ambalo linakuwa kwa kasi kubwa kuliko uchumi wetu. Ukuaji wa uchumi wetu wa taifa ni wastani wa asilimia 7% kwa mwaka, wakati ukuaji wa deni la taifa ni asilimia 20% kwa mwaka!. Rate hii ikiendelea, tutafikia kiwango ambacho deni litakuwa halihimiliki kwa kufikia kiwango cha mwisho cha uwezo wa kukopesheka, hivyo taifa letu kuwa halikopesheki.

Sababu kubwa ya kukua kwa deni la taifa ni kutokana na nchi yetu kupanga bajeti tegemezi ambayo ni bajeti kubwa kuliko makusanyo yetu, hivyo bajeti yetu ziku zote inategemea mikopo na misaada ya nchi wafadhili, inapotokea nchi wafadhili wamepunguza misaada, nchi yetu hujikuta inalazimika kukopa ili kutekeleza bajeti, both recurrent, na development.

CAG Prof. Mussa Assad ambaye kitaaluma ni mchumi, hapa anatoa dawa ya kutibu ugonjwa huo wa kutegemea budget tegemezi.
Msikilize.

Paskali.

Kuna vitu hapa CAG wa wakati huo Prof. Mussa Assad alivisema, Bunge ndilo lilitakiwa kusimamia, but they did nothing!.

Sasa leo msikilize huyu Mheshimiwa

View attachment 2060338
Haya sasa...
Halafu watu wakiitwa mazuzu!, wanakasirika!.
P
 
Wanabodi,
Moja ya ugonjwa mkubwa na mbaya kuliko magonjwa yote yanayolikabili taifa letu, ni ugonjwa wa kukua kwa deni la taifa, ambalo linakuwa kwa kasi kubwa kuliko uchumi wetu. Ukuaji wa uchumi wetu wa taifa ni wastani wa asilimia 7% kwa mwaka, wakati ukuaji wa deni la taifa ni asilimia 20% kwa mwaka!. Rate hii ikiendelea, tutafikia kiwango ambacho deni litakuwa halihimiliki kwa kufikia kiwango cha mwisho cha uwezo wa kukopesheka, hivyo taifa letu kuwa halikopesheki.

Sababu kubwa ya kukua kwa deni la taifa ni kutokana na nchi yetu kupanga bajeti tegemezi ambayo ni bajeti kubwa kuliko makusanyo yetu, hivyo bajeti yetu ziku zote inategemea mikopo na misaada ya nchi wafadhili, inapotokea nchi wafadhili wamepunguza misaada, nchi yetu hujikuta inalazimika kukopa ili kutekeleza bajeti, both recurrent, na development.

CAG Prof. Mussa Assad ambaye kitaaluma ni mchumi, hapa anatoa dawa ya kutibu ugonjwa huo wa kutegemea budget tegemezi.
Msikilize.

Paskali.
Mayalla naomba kukuuliza swali nje ya mada.

Je channel yako umeilipia?
 
Mayalla naomba kukuuliza swali nje ya mada.

Je channel yako umeilipia?
No Channels za youtube zinazopaswa kulipiwa ni zile public youtube channels zilizo monetized na zimekuwa branded kama TV. Mimi ni private channel, sio monetized, sio TV, hakuna kukumbia like wala subscribe, hivyo siingii kwenye anga za TCRA.
P
 
😁😁😁
16407039515591.jpg
16407039395440.jpg
 
Hiki alichokisema Prof. Asad ndicho kile kile alichokisema Spika Ndugai!.
P
Mkuu kwenye nidhamu ya matumizi ni bora Spika anyamaze, si aliwahi kuhamishia ofisi India, au ndio mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu ?

Hiki alichokisema Prof. Asad ndicho kile kile alichokisema Spika Ndugai!.
P
Kwa kipato kipi sasa,?
Mapato kwa mwezi ni Trilion 1.2
Mishahara ya wafanyakazi bilioni 700.
Ruzuku elimu dawa, mafuta bilioni 400
Spare, kulipa madeni, etc bilioni 300.
Hizi ni estimate zangu, kiufupi hela haitoshi,
Two option
1-Kukopa
2-kutoza kodi, tozo, kwa bidii, yaani watu mtozwe kodi za kutosha ili kujenga infrastructures za matrilion
 
Back
Top Bottom