CAG Prof. Mussa Assad amjibu Spika Ndugai, Asema Katiba ya JMT haina kifungu kinachomtaka ajieleze

CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.
Msomi atashinda,kwakua ana hoja za msingi,kuwa dhaifu ni kawaida kwa kitu,mtu,hata mbwa pia wapo dhaifu.

Mbwa anaye mbwekea anayemlisha kwa kuwa karuka getting ni mbwa mzuri Sana ,kuliko mbwa anaye mbwekea anayemlisha ili mlishaji aone Kuna mbwa!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daaah hivi ndugae ugonjwa ambao alilazwa India hauhusiani na upstairs kidogo?maana anagaragazwa na kuchakazwa
 
neno hkili ni sawa na wanasiasa aanavyotuita wananchi wanyonge kwani sisi tunape da kuitwa wanyonge WAO DHAIFU SISI WANYONGE
Mkuu hakika umenena,eti sisi wanyonge wao kuitwa dhaifu nongwa,inabidi watufafanulie mwananchi ni nani,nahuyo mwananchi mnyonge ni yupi.Kumbe wao so wananchi na si wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usimuhusishe mpendwa wetu katika hili, hawezi kuingilia jambo dogo kama hili hawezi kuingia mtego wa kubishania neno dhaifu tena katika nchi ya watu maskini na wanyonge. Yuko busy tuletea maendeleo wananchi.
Tukutane 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania wote wanyonge, Acha kutetea wezi na wabadhirifu wa pesa za umma (Kodi zetu), Pesa zinaibiwa bila huruma, upendeleo umekuwa jambo la kawaida. Rais huyu siyo mkweli.
 
Kamusi ya Assadi ipo wapi? Utuoneshe maana ya neno Dhaifu. Assadi namfahamu sana, ni Kiburi sana, na kujifanya anasimamia misimamo isiyo na kichwa wala miguu. Aondoke kwenye utumishi wa umma, awe mwanaharakati, huko atafaa zaidi. Kwenye utumishi wa umma kuna taratibu zake, huwezi enda huko nje ya nchi ukadhalilisha nchi yako. Ajitathmini, na achie ofisin.

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safari hii nitakuwa makini wakati wa kumchagua mbunge wangu wa jimbo la kinondoni walau afanane fanane kidogo na mbunge wa Singida mashariki kitaaluma.

Haiwezekani CAG aielewe vizuri katiba kuliko mbunge wangu.

Maendeleo hayana vyama!
Hahaaaaaaa........

Kweli Mkuu Johnthebabtist umenena!
 
Mihimili ya utawala iko mitatu lakini Rais wa Nchi ndo mkuu wa mihimili yote hiyo. Baada ya Uchaguzi Mkuu ni Rais anayelifungua Bunge rasmi,je kaka Rais siyo sehemu ya Bunge ni kwa nini alifungue? Majaji wa Mahakama Kuu huteuliwa na Rais, je Rais siyo sehemu ya Mahakama?
Raisi anaapishwa na jaji mkuu..Jee Jaji Mkuu ni juu ya raisi?
 
neno hkili ni sawa na wanasiasa aanavyotuita wananchi wanyonge kwani sisi tunape da kuitwa wanyonge WAO DHAIFU SISI WANYONGE
Pia wao wanavyopenda kuitwa MHESHIMIWA, hivi walishatuuliza sisi wananchi ikiwa tunapenda kuwaita hilo jina. Kinyume cha MHESHIMIWA kuna MDHARAULIWA.

Wote tuitane ndugu, Ndugu Spika Job Ndugau, Ndugu Rais nk.
 
CAG ni mwenyekiti wa chama gani cha kisiasa ?? kwa Maana yupo busy kweli kupambana na hoja za kisiasa Badala ya kutekeleza majukumu yake kitaalam.
 
Hii ni intellectual fight haihitaji muscles elongated. Sasa sijui kama hao wapiganaji wanazo weapon za kutosha kusimama kwenye battle hii. Naona wanapigana Watu ambao hawapo katika level moja
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom