CAG Prof. Mussa Assad amjibu Spika Ndugai, Asema Katiba ya JMT haina kifungu kinachomtaka ajieleze

Hizo hoja za CAG ziko wapi hapo?

Anyway, Ndugai hajui maana ya Separation of power, asijaribu kuuingiza mhimili wa serikali katika hili suala.
CAG hakusema Rais ni dhaifu alisema "Bunge lina udhaifu" na wala hakusema bunge ni dhaifu.

Ndugai apambane na hali yake!. Asitafute huruma ya Magufuli.
Bado hamjajua kuna Spika kubwa sana mithili ya zile za kwenye mikutano ya injili zimefungwa Dodoma na Mic ipo Mkoa mmoja Mashariki ya Tanzania?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa ndiyo ma- Prof wasomi wachache waliobakia nchini kwetu ambao wanausimamia usomi wako na si matumbo - Hongera CAG kulitumikia Taifa lako bola kuogopa vitisho, tunajua; tunafahamu Rais wetu kwa sababu ni mpinga Rushwa na Ufisadi tunajua atakuwa pamoja na wewe maana wewe ni taa unamulika mbele kisha yeye anasafisha.
 
Serikali na Bunge ni vitu viwili tofauti...hivyo Ndugai aache uongo. Rais hawezi kuwa sehemu ya Bunge hata kama anasaini yanayopitishwa na Bunge.

Mihimili ipo mitatu. Spika Ndugai aache chuki binafsi na CAG, kwanza CAG hakusema bunge ni dhaifu ila alisema "kama mapendekezo ya CAG kuhusu upotevu wa pesa hatua hazitachukulia haitakuwa suala lake bali litakuwa ni udhaifu wa bunge" hapo amejibu swali kutokana na jinsi alivyoulizwa.

Hapa linaloendelea kutokea ni kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana wa fedha za umma kwa hiyo wanaona jinsi ya kulificha hili tatizo ni kumtibua CAG na kumsemea uongo ili afukuzwe.

Hakuna asiyejua nia ya ndugai na Magufuli....kumfukuza CAG na kumuweka mtu wa aina ya Doto James ili waendelee kuchukua fedha zisizo idhinishwa.
Tatizo ni kwamba hafukuziki. Kinachojaribiwa hapo ni kumtia shinikizo hadi ajiuzulu. Je, ataufyata kwa shinikizo hilo au atagangamala? Nadhani itategemea watakavyofanya upgrading ya hayo mashinikizo, labda watafikia threshold, na kwa kiasi kikubwa inategemea threshold ya Prof ilipo.
Hawajaipata 'tap-out spot' yake, pale ambapo pakifigiswa hataweza kuvumilia tena, ndipo wanapopataka sasa.
 
Yale mashavu kuumuka vile ni afya kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app



Nimejikuta nacheka sio kwa kupenda kabisa mimi nimejiuliza pia. Afya ina mgogoro wa hali ya juu huenda inatafuna na ubongo wake kwanini Ndugai hareason jamani anaibisha sana mno. Ni aibu kwa mhimili mkubwa km bunge kuwa na kiongozi mjinga kama huyu sidhani hata kama ni mjinga au ni mpumbavu
 
Kamusi ya Assadi ipo wapi? Utuoneshe maana ya neno Dhaifu. Assadi namfahamu sana, ni Kiburi sana, na kujifanya anasimamia misimamo isiyo na kichwa wala miguu. Aondoke kwenye utumishi wa umma, awe mwanaharakati, huko atafaa zaidi. Kwenye utumishi wa umma kuna taratibu zake, huwezi enda huko nje ya nchi ukadhalilisha nchi yako. Ajitathmini, na achie ofisin.

Sent using Jamii Forums mobile app
OK OK. Asipojiuzulu itakuwaje? Kuna hatua gani za kumchukulia?
 
Kwa jicho pana Rais yupo nyuma ya Spika.

Mwaka jana alipokea Live ripoti ya CAG na kuichambua madudu kadhaa yaliyoainishwa.

Mwaka huu ni kama hajui kuna ripoti ipo, aliipokea kimya kimya na sekeseke linaloendelea ni kama hasikii.

Siku zote Rais tulie nae kitu anachopinga huwa hanyamazi maana hana kariba ya kujizuia. Ila kwa hili kanyamaza. Ipo sababu.

Hapa ndipo tunasema kwa jicho pana magufuli anamsapoti ndugai, maana madudu yote ni ya uongozi wake, 1.5 trilion, zisizofahamika matumizi ni awamu yake.

Manunuzi yasiofata sheria, zabuni na kadhalika, magufuli apendi kusemwa, anaamini yeye anajua kila kitu. Na ana uwezo wa kila kitu ilimradi tu yeye ni Rais. Kauli zake nyingi huthibitisha hilo.

Sasa anasaka kichwa cha CAG na uwezo wa kukipata hana. Sasa anamtumia yule dhaifu bungeni kufikia lengo.

Rudia kauli ya dhaifu jana. "Eti" CAG akajisalimishe kwa Rais. Na ajiuzuru. Hii ndio nia ya Dhati ya Magufuli, Assad aondoke maana ni kikwazo kwake

Magufuli hapendi kukosolewa wote mnajua ya Lissu, wote mnajua ya Wapinzani leo, wote mnajua kilichompata msajili wa hazina alipotoa maoni ya wazi clouds 360 kuwa kuweka fedha za umma bank kuu kutapunguza mzunguko wa fedha na si kosa kisheria kuweka katika mabenki ya kawaida, aliliwa kichwa.
Dumelang
ukiona JIWE katengeneza ZIARA isiyokuwa na ratiba na nyingine anajiongezea juu kwa juu ujue ANAKIMBIA KUONA RIPOTI YA ASSAD.. Hebu ona baada ya makelele kibawwo ya ****** kupinga kupokea ripoti ya CAG itakayosainiwa na ASSAD..
****** na JIWE wamegundua kuwa ASSAD ni NGANGARI nae ****** akatafuta safari ili mradi tu asiwepo kwenye upokeaji wa RIPOTI YA ASSAD. karudi kakuta imeshapokelewa ileile iliyosainiwa na WASIEMPENDA. Ndio kaamua kujitoa ufahamu kwa kuropoka mbele ya wanahabari.
sijui kwanini waandishi hamkumuuliza ****** Kwanini mbona ameipokea ileile iliyosainiwa na WASIYEMPENDA!! SI WALISEMA WATAMPOTEZEA??
 
hivi ndugai angeitwa mnyonge je ? si angepasuka mbona sisi tunaitwa wanyonge japo wengine hatupendi ila tumekausha tu,
Usimuhusishe mpendwa wetu katika hili, hawezi kuingilia jambo dogo kama hili hawezi kuingia mtego wa kubishania neno dhaifu tena katika nchi ya watu maskini na wanyonge. Yuko busy tuletea maendeleo wananchi.
Tukutane 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mihimili ya utawala iko mitatu lakini Rais wa Nchi ndo mkuu wa mihimili yote hiyo. Baada ya Uchaguzi Mkuu ni Rais anayelifungua Bunge rasmi,je kaka Rais siyo sehemu ya Bunge ni kwa nini alifungue? Majaji wa Mahakama Kuu huteuliwa na Rais, je Rais siyo sehemu ya Mahakama?
Hapo ndio ubovu wa Katiba unapoonekana. Je, Rais akimteua msajili wa vyama unategemea msajili atatenda haki? Katiba mpya ni ya muhimu kwa mazingira ya sasa na hata Jaji Mkuu hakupaswa kuteuliwa na Rais

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwanini wasimyamaze kama JK alivyokuwa na staili hii?
Kazi wanae
Hawa hawawezi kaa kimya kwani ni waongo kupita kiwango, yeye jk alikubali kuwa ni kweli kuna udhaifu, ndio maana wakati mwingine alikuwa anakaa kimya,sasa awamu hii hawataki kukubali mapungufu yao, yaani waaminishe watu kuwa kila jambo liko sawa!!! Sasa wanapoamua kuingia kwenye ligi ndio wanazidi kujivua nguo kabisa
 
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.

Hawa watu wanapimana ubavu. Kila mmoja anatetea hoja yake.
Udhaifu ni udhaifu tu. Kama mtu ni dhaifu hatakama ukiambiwa si dhaifu haiondoi udhaifu wake.
Kinachohitajika ni kuondoa huo udhaifu kama inawezekana na si kuuficha kwa kutishia kutofanya kazi na aliekuita dhaifu.


NB:
Kama hakubali kuwa bunge ni dhaifu, aende mahakamani
 
Nchi imevurugwa asilimia mia moja, ivi ccm wataacha lini kuongoza nchi kwa maagizo ndugai aonekana wazi nyuma yake kuna mtu ana nguvu kubwa, huyu CAG akiacha kazi atakaekuja ni wazi ataibua kilichowapendeza walio juu ivi hii nchi itafika wapi?

Ni kiongozi gani tena atakayekuja Tz na kusema atapiga vita ufisadi akamaanisha kweli nia yake ni ufisadi? Huyu CAG ameleta ripoti ina mambo kibao ya kuyafanyia kazi kama nchi lakini zaidi kilicho trend ni nguvu ya spika kujiona na ubavu wa kumuondoa CAG
 
Sasa ukisema hutaki kufanya kazi na sieji then,taarifa zote zilizo mezani kwako zinasignature yake huo ni zaidi ya utahira
 
CAG ameamua kumjibu mheshimiwa spika baada ya press conference ya jana ambayo spika amemtaka ajiuzulu.

Katika majibu hayo CAG amebainisha vizuri akitumia vipengele vya Katiba kuainisha wajibu wake bila kutetereka.

Hii ngoma ni kali kweli kweli, maana hapa kuna msomi vs mwanasiasa.

Sijui mshindi ataibuka nani.
CAG

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom