CAG Prof. Mussa Assad amjibu Spika Ndugai, Asema Katiba ya JMT haina kifungu kinachomtaka ajieleze

Kamusi ya Assadi ipo wapi? Utuoneshe maana ya neno Dhaifu. Assadi namfahamu sana, ni Kiburi sana, na kujifanya anasimamia misimamo isiyo na kichwa wala miguu. Aondoke kwenye utumishi wa umma, awe mwanaharakati, huko atafaa zaidi. Kwenye utumishi wa umma kuna taratibu zake, huwezi enda huko nje ya nchi ukadhalilisha nchi yako. Ajitathmini, na achie ofisin.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona unalia mkuu? Prof Assad anakuumiza sana?
 
CAG ni mkombozi mpya wa Taifa, hesabu za hela zinakwenad halijojo - wapinzani wamebwanwa mbavu hawahemi yaani wamepigwa ngeta - sasa Mungu kamnyemya mtetezi wetu mpya wa hesabu za umma - ila hawakawii kumkalia vikao na kumshughulikia maana Shetwain siku zote ni kivuruge...
 
Tafadhari mkuu, nakuomba uniteuwe kuwa CAG nitakutunzia siri za wizi wako wa mali za watz wanyonge.
 
Serikali na Bunge ni vitu viwili tofauti...hivyo Ndugai aache uongo. Rais hawezi kuwa sehemu ya Bunge hata kama anasaini yanayopitishwa na Bunge.

Mihimili ipo mitatu. Spika Ndugai aache chuki binafsi na CAG, kwanza CAG hakusema bunge ni dhaifu ila alisema "kama mapendekezo ya CAG kuhusu upotevu wa pesa hatua hazitachukulia haitakuwa suala lake bali litakuwa ni udhaifu wa bunge" hapo amejibu swali kutokana na jinsi alivyoulizwa.

Hapa linaloendelea kutokea ni kuwa kuna ubadhirifu mkubwa sana wa fedha za umma kwa hiyo wanaona jinsi ya kulificha hili tatizo ni kumtibua CAG na kumsemea uongo ili afukuzwe.

Hakuna asiyejua nia ya ndugai na Magufuli....kumfukuza CAG na kumuweka mtu wa aina ya Doto James ili waendelee kuchukua fedha zisizo idhinishwa.
Kama ni kweli, na kama nilivyomsikia CDF juzi, basi kuna jambo zito ndani ya hivi vitisho!!
 
Nimemsikiliza Ndugai ... bado anasisitiza kuwa hawatafanya kazi na Assad wakati huo huo report wameipokea na wanadai wataifanyia kazi ..... I am lost!!
 
Hizo hoja za CAG ziko wapi hapo?
Anyway, Ndugai hajui maana ya Separation of power, asijaribu kuuingiza mhimili wa serikali katika hili suala.
CAG hakusema Rais ni dhaifu alisema "Bunge lina udhaifu" na wala hakusema bunge ni dhaifu.
Ndugai apambane na hali yake!. Asitafute huruma ya Magufuli.
Ndugai anasema CAG anampa rais wakati mgumu bure. Hapa uchambuzi unaibua maswali mengi kuliko majibu.
 
Mkuu CAG yupo sahihi kwa hakika. Ni ajabu kuona Spika anaingiza siasa kwenye taaluma. Neno dhaifu kwa wakaguzi ni neno la kawaida.

Kuna udhaifu (weaknesses) kwenye vitu mbalimbali kama mfumo, utekelezaji au ufuatiliaji wa jambo na hili sio tusi au kashfa.

Spika asiwatafuatie watalaamu maneno ya kutumia au kutumia ambayo yatamfurahisha yeye
Mbona JK aliitwa dhaifu na Mnyika na maisha yaliendelea. Ujue wameipa pro hii neno dhaifu na MTU ambaye hakusikia mjadala nimejua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona JK aliitwa dhaifu na Mnyika na maisha yaliendelea. Ujue wameipa pro hii neno dhaifu na MTU ambaye hakusikia mjadala nimejua

Sent using Jamii Forums mobile app
Shule ya msingi kulikuwa na utani sana, sasa wakipewa jina la utani na wakikutania wewe usiwajali vinginenvyo basi hilo ndilo litakuwa jina lako kweli kweli.

(Weka lafudhi ya kimakonde) Sasa kama ntu akikuita dhaifu wakati wewe unajijua si dhaifu sasa checheto wa ninii bwana wewe baaa!!
 
Ndugai akijiuzuru yeye ndio tutafanya sherehe...sio CAG anaemulika wezi wa kodi zetu zinavyitafunwa...
 
Back
Top Bottom