CAG mstaafu Uttoh: Hakuna Shirika lolote la ndege duniani lililopata faida baada tu ya kuanzishwa, ATCL haijawahi kulipa Gawio Serikalini

Alijigeuza mwanasiasa badala ya professional...

Mwenye fani yake kaongea hapo bila politics
Hahaaaa! Assad kaingiza siasa lini? Kipindi yupo kazini au baada ya kutolewa? Huyo Uttoh hafikii level za Assad kwa weledi, huyo Uttoh ni mfia chama tu, leo anatuambia shirika la ndege haliwezi pata faida kwa muda mfupi ila wakati mwendazake na mkurugenzi wa kampuni wanasema wamepata faida huyo Uttoh alikaa kimya hakujua kama shirika lina muda mfupi, Kilichompoza Assad ni kusimamia anachokiamini tu, Bunge dhaifu limeshindwa isimamia serikali
 
CAG mstaafu mh Uttoh amesema hakuna shirika la ndege lolote duniani lililowahi kupata faida katika miaka ya mwanzo ya operations zake.

Kuhusu gawio mh Uttoh amesema dividend hutolewa baada ya biashara kupata faida na huamuliwa na bodi kiasi gani cha faida kigawiwe kama dividends
Uttoh amesema kwa uelewa wake ATCL haijawahi kulipa dividend kwa serikali, na kama kuna fedha ziligawiwa kwa serikali na ATCL hicho ni kitu kingine siyo dividend

CPA Uttoh amesema kimsingi mashirika ya umma hayapaswi kulipa dividend kwa sababu hayafanyi biashara na ametoa mfano UDSM wanalipa dividend serikalini kwa biashara gani wanayofanya?!

Source: ITV kipindi cha Kipima Joto
Akili kubwa hizi,Jiwe Ngosha alitaka hata polisi walipe gawio,lakini sikubalisni kulinganisha taasisi za Elimu na mashirika kama ATCL,posta,au TTCL,haya mashirika inabidi yafsnye biashara na yatoe gawio,mbona MTN ya Afrika kusini inatoa gawio?au haya ya kwetu ni kuuza sura tu,
 
Kwanza tuelewe kwamba kuna tofauti ya ATC (Air Tanzania Corporation) ya enzi za mwalimu na ATCL (Air Tanzania Company Limited) hii ya Sasa hivi pamoja na kuwa ni public owned lakini ni biashara inayotakiwa kutengeneza faida. Kwahiyo yes lazima ilipe park fee na hizo tozo nyingine zote kama wanavhofanya Precision na wengine.

Na uelewe kwamba as of now ATCL hawamiliki ndege hata Moja ndege zote zinamilikiwa na serikali chini ya wakala wa ndege za serikali na ATCL no mkodishaji Tu. Kwa maana kwamba kama serikali imeamua kufanya biashara ya jukodisha ndege basi hata precision au auric wanaweza kwenda kukodi. Lakini kwasababu zinazoeleweka tukasema kwanini tumpe mtoto wa jirani chakula ilihali wa kwetu ana njaa? So wakapewa ATCL na mpaka Leo hii Kati ya tozo ya 75b waliyotakiwa kulipa Kwa kukodisha ndege hizo wamelipa 8b Tu.

Sasa ukirudi kwenye maana halisi ya gawio (Dividend) ni faida ambayo hupewa wawekezaji (Kwa maana ya serikali/umma) kwenye issue ya ATCL baada ya bodi kukaa na kupewa taarifa ya fedha ya mwaka pamoja na mipango ya maendeleo ya mwaka unaofuata so Ile faida itawekwa kwenye mipango iliyopitishwa na baadae wataamua kiasi gani wanakiacba Kwa dharura then kinachobaki ndio inakuwa gawio. Kwa muktadha huu inamaanisha ATCL walikuwa wanapata faida ya zaidi ya 28b jambo ambako sio sahihi ukaguzi umeonyesha wanapata hasara tena kubwa. Ndio maana Uttoh anasema like walichokitoa kiutaratibu hakiwezi kuwa dividend itakuwa kitu kingine tu

Jambo la msingi hapa la kukumbuka ni kwamba ATCL haimiliki uwanja wote wa ndege, pamoja na huduma zote zotolewazo hivyo lazima wazilipie na kwenye hesabu zao lazima zitokee kama cost of operations.
Nadhani hajamwelewa mhusika, nadhani sina uhakika maana unacho andika wewe ni tofauti na maelezo aliyotupa...
 
Nadhani hujamwelewa mhusika, nadhani sina uhakika maana unacho andika wewe ni tofauti na maelezo aliyotupa
 
Hebu niambie Serikali za nchi za Ulaya zinazofanya biashara yoyote ile. Serikali wajibu wake ni kukusanya kodi na kutoa huduma. Nchi za Afrika Serikali zinajiingiza kwenye biashara na matokeo yake ni kuingia mkenge wa hasara kubwa kwa walipa kodi.
Qatar airway
Emirate
Egypt air
Ethiopian airlines
Etihad
35% ya makampuni ya kibiashara China yanamilikiwa na serikali
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Otoh usiwatetee, kufufua biashara bila ya upembuzi yakinifu matokeo yake ndiyo haya....watulipe tu Bil 59 zetu yaishe.
 
Linapata faida ila inamezwa na running costs kutokana na upya (BEP)... na faida inapunguza hasara from 113B to 60B.

Anaposema watumishi hawafai thats BS... nikupe mifano zaidi?
Hahaaaa! Assad kaingiza siasa lini? Kipindi yupo kazini au baada ya kutolewa? Huyo Uttoh hafikii level za Assad kwa weledi, huyo Uttoh ni mfia chama tu, leo anatuambia shirika la ndege haliwezi pata faida kwa muda mfupi ila wakati mwendazake na mkurugenzi wa kampuni wanasema wamepata faida huyo Uttoh alikaa kimya hakujua kama shirika lina muda mfupi, Kilichompoza Assad ni kusimamia anachokiamini tu, Bunge dhaifu limeshindwa isimamia serikali
 
Huyu ndio CAG. Enzi zake alikuwa smart sana na ndiye aliyenifanya nianze kufuatilia ripoti za CAG. Halafu haropokiropoki kama yule CAG aliyetaka kujifanya Mhimili!
Chuki zitakuua mzee, bunge dhaifu linashindwa kuisimamia serikali
 
Tanzania hakuna Watanzania wenye uwezo wa kupanda ndege kutokana na wengi vipato vyao kuwa vidogo sana. Hivyo kutegemea 5% ya population ya 60 millions wenye uwezo wa kupanda ndege ili ATCL iingize faida ni kujidanganya.
Kwa hiyo Tanzania haihitaji kuwa na ndege? Iwapo Tanzania ina watu takriban milioni 60, na ndege moja inachukua abiria wasiozidi 200, unaona kuwa hiyo ni 0.0003% tu ya watanzania wanaoweza kutumia ndege hizo ambayo ni chini sana ya hiyo 5%.
 
Kwa hiyo tutegemee faida baada ya miaka 100? Watanzania tulimuonya dikteta kwamba ununuzi wa ndege si kipaumbele cha Watanzania na biashara ni hasara tupu kama ASINGEKURUPUKA hiyo zaidi ya 3 trillions si ingeweza kutumia kuongeza mishahara ya Wafanyakazi nchini!?
Subiria povu kutoka praise team
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mashirika yote hayo hayaendeshwi na Serikali Serikali imeweka tu mazingira mazuri ya uwekezaji na kuwaachia management wafanye decisions bila ya kuingiliwa na Serikali kwa namna yoyote ile. China Serikali imekuwa ikifanya biashara tangu enzi za ukomunisti. Kule Hong Kong private sector ilikuwa imeshamiri sana. China imeingilia hivi karibuni uchumi umeanguka.
Pia kama Nchi za Magharibi zitatoa incentives nzuri kama walivyofanya Japan ili Makampuni ya nchi hizo yaliyowekeza China basi uchumi wa China utaporomoka vibaya sana kwani makampuni hayo yameajiri mamilioni ya Wachina.
Qatar airway

Emirate
Egypt air
Ethiopian airlines
Etihad
35% ya makampuni ya kibiashara China yanamilikiwa na serikali
 
Yes tena nalifundisha kabisa hilo somo, mbali zaidi ni expwrt wa project management na pia ni mchumi kwahiyo napoeleza situmii hisia natumia utaalamu na practical experiences
Duh! hao wanafunzi wako nawaonea huruma.

Na wao huwa unawaambi dividend maana yake sio gawio?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Linapata faida ila inamezwa na running costs kutokana na upya (BEP)... na faida inapunguza hasara from 113B to 60B.

Anaposema watumishi hawafai thats BS... nikupe mifano zaidi?
Ndugu maana ya faida ni (Mapato - Matumizi) hapo kwenye matumizi no pamoja na running costs kwahiyo huwezi kusema unapata faida lakini inamezwa na running costs that's called loss mzee
 
Hebu acheni kuandika uongo kwenye mambo ambayo hamna ufahamu nayo, ni bora upite kimya kimya. Hawa wanapataje faida kwa zaidi ya miaka 30 continuously!?
Kama hakuna faida chadema waliwekaje kwenye ilani
 
wewe jamaa huwa una matatizo ya akili kabisa fuatilia kabisa unachocoment mara nyingi unaonekana ni mtu mwenye uelewa mdogo sana na kama ulisoma basi wazazi wako walipoteza hela bure yaani ni full kilaza kwa kitaalamu tunasema you are mentally retarded
Tatizo mnakipenda chama kupita kiasi, hamsikii wala hamuoni hta km ukweli upo wazi kbsa bado mtaukataa...tht y mko very emotional chama chenu kinapoguswa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
BAK unaniangusha, yaani unaendekeza mambo ya from hands to mouth?

Mishahara itapanda kama tutazalisha kiwango cha juu na hakiji tu bila kutoka jasho...Imagine miradi yote ya kimkakati iishe mishahara si ita triple?

So far hayati alijitahidi sana kwanza kupunguza inflation na deflation kwenye riba, kisha social service kama elimu na afya aliiongezea budget even three times mlitakaje? Aliigawa cake ya taifa kwa wemgi zaidi...Wafanyakazi Tanzania hawafiki hata 11% kisha wanachukua 60% ya budget...Aliilipa mishahara bila kuchelewesha hata sekunde na in a very sustainable way
BAK yupo sahihi kabisa na ukosoaj8 wako haupo technical. Ambacho unapaswa ufahamu hao 11% ndio wanaweza expand au contract uchumi.

Ndege za trillion 3 plus pesa inaenda Canda huko lakini Trillion 3 ikitumika ndani whether kulipa wazabuni au kuajiri/kupandisha mishahara ina maana pesa itazunguka kwenye uchumi na kuchochea biashara kupitia spillover effects.

Na ndio maana duniani mabillionea na washika mitaji wakubwa hawafiki 5% lakini dunia nzima tunawategemea kwa kila kitu kuanzia ajira mpaka supply ya bidhaa muhimu so uchumi hauangalii namba ya direct wanufaika bali inaangalia wale wanufaika watatawanyaje pesa baada ya kuzipata.

Ndio maana mwaka juzi Prof.Luoga alishusha reserve ratio requirement ya benki za biashara pale BOT ili kwamba benki za ndani ziwe na ukwasi ziweze kuajiri,kukopa,kuwekeza n.k ili pesa zitoke kwenye mashelf ya BOT ziende kwa raia kuchochea biashara mpaka ya boda boda na mama ntilie!! Uchumi unafanya kazi hivyo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom