CAG Mstaafu Ludovick Utouh: Bunge halisimamii mapendekezo ya CAG

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,366
2,000
Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovock Utouh amesema Bunge limeshindwa kusimamia mapendekezo ya ripoti za CAG kwa Serikali huku akimtetea Profesa Mussa Assad aliyepishana kauli na chombo hicho cha kutunga sheria hivi karibuni.

Mbali na Bunge, Utouh ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwajibikaji wa Umma (Wajibu), amewakosoa baadhi ya mawaziri aliosema wamekimbilia kujibu mapigo ya ripoti ya CAG kwa kuwa hawahusiki.

Akizungumzia kauli za Utouh, Spika wa Bunge, Job Ndugai licha ya kukataa kutoa maoni, alihoji kwa nini Utouh asipeleke maoni hayo Bungeni.

Utouh ameyasema hayo leo wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi wa ripoti za CAG za miaka mitatu, jijini Dar es Salaam.

"Katika umri wangu huu sijawahi kusikia mambo haya popote duniani, lakini sasa nayasikia Tanzania. Msuguano kati ya Spika na CAG. CAG spoke (alizungumza) Bunge ni dhaifu. Anaiagiza Serikali na Bunge linatakiwa lisimamie, tumeona hapa takwimu, is that strong (Je, lina nguvu)?" amehoji Utouh.

Awali, akiwasilisha uchambuzi wa ripoti tano za ufanisi za CAG, ofisa wa Wajibu, Andendekisye Mwakabula amesema zilikiwa na mapendekezo 85 kwa taasisi 10, lakini yaliyotekelezwa ni asilimia 26 tu.

Kuhusu mawaziri kujibu ripoti za CAG, Utouh aliendelea kusema, “mawaziri wanapanguaje hoja za CAG? Kwa sababu zile siyo siasa, inaeleza kabisa nani anahusika.”

Chanzo: Mwananchi
 

chaliko

Senior Member
Apr 1, 2019
142
1,000
Siku si nyingi tutaambiwa kuwa huyu anawashwa na ni beberu.

Bunge hili la Ndugai linafanya kazi zaidi ya Chini ya Viwango.
 

kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
3,990
2,000
Bwana yule anagongwa kama mpira wa kona
Mara CAG mara utoh mara masele
 

mnyonge wa hali ya chini

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
856
1,000
Huyu nae anataka kuziba kitumbua chao ajiandae wakishindwa kumwita kwenye ile kamati ya "MADILI" basi ataitwa na wale watu wasiojulikana. ...
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,029
2,000
Utouh ‘alibip’ Bunge, adai halisimamii mapendekezo ya CAG

Tuesday May 28 2019

Kwa ufupi
Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali mstaafu, Ludovick Utouh amemtetea CAG wa sasa akisema Bunge limeshindwa kusimamia mapendekezo yake kwa Serikali.

By Elias Msuya, Mwananchi emsuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) mstaafu, Ludovock Utouh amesema Bunge limeshindwa kusimamia mapendekezo ya ripoti za CAG kwa Serikali huku akimtetea Profesa Mussa Assad aliyepishana kauli na chombo hicho cha kutunga sheria hivi karibuni.

Mbali na Bunge, Utouh ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwajibikaji wa Umma (Wajibu), amewakosoa baadhi ya mawaziri aliosema wamekimbilia kujibu mapigo ya ripoti ya CAG kwa kuwa hawahusiki.

Akizungumzia kauli za Utouh, Spika wa Bunge, Job Ndugai licha ya kukataa kutoa maoni, alihoji kwa nini Utouh asipeleke maoni hayo Bungeni.

Utouh ameyasema hayo leo wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi wa ripoti za CAG za miaka mitatu, jijini Dar es Salaam.

"Katika umri wangu huu sijawahi kusikia mambo haya popote duniani, lakini sasa nayasikia Tanzania. Msuguano kati ya Spika na CAG. CAG spoke (alizungumza) Bunge ni dhaifu. Anaiagiza Serikali na Bunge linatakiwa lisimamie, tumeona hapa takwimu, is that strong (Je, lina nguvu)?" amehoji Utouh.

Awali, akiwasilisha uchambuzi wa ripoti tano za ufanisi za CAG, ofisa wa Wajibu, Andendekisye Mwakabula amesema zilikiwa na mapendekezo 85 kwa taasisi 10, lakini yaliyotekelezwa ni asilimia 26 tu.

Kuhusu mawaziri kujibu ripoti za CAG, Utouh aliendelea kusema, “mawaziri wanapanguaje hoja za CAG? Kwa sababu zile siyo siasa, inaeleza kabisa nani anahusika.”
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,029
2,000
Vikaragosi vya nduli na dikteta wa Ikulu Ndugai na Tulia ndiyo chanzo cha Bunge kuwa DHAIFU.

Dikteta anawatumia hivyo vikaragosi vyake viwili ili kuhakikisha Bunge linaendelea kuwa DHAIFU huku yeye akiwa hakosolewi na hili Bunge DHAIFU na hivyo kuendeleza udikteta na maovu yake mengine nchini.


 

Six-month

Member
May 11, 2019
83
125
Wamezoea kubumbabumba wanaomba kura kwauongo kila kitu uongo hatautaalamu namahojiano makubaliano ya Ofice mbalimbali wanatamani viwe vyauongo ukweli hawataki kuusema walakuambiwa ukweli wenyewe sifa hatakuaribu nchi sisi tunatambua nikosa waokwao nisifa
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,192
2,000
Huu ndio Ukweli wenyewe kwa sasa nna nukuu "Katika umri wangu huu sijawahi kusikia mambo haya popote duniani, lakini sasa nayasikia Tanzania. Msuguano kati ya Spika na CAG. CAG spoke (alizungumza) Bunge ni dhaifu. Anaiagiza Serikali na Bunge linatakiwa lisimamie, tumeona hapa takwimu, is that strong (Je, lina nguvu)?" amehoji Utouh.

Hoja nyingine inayo hitaji Majibu ni hii nna nukuu “mawaziri wanapanguaje hoja za CAG? Kwa sababu zile siyo siasa, inaeleza kabisa nani anahusika.”

Wahusika mtakuwa mme sikia , haya muiteni au kamkamateni na huyu kama mlivyo zoea kutumia Nguvu badala ya Akili.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,029
2,000
CAG mstaafu Utouh anakubaliana na CAG Assad kwamba Bunge ni DHAIFU
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
102,029
2,000
CAG wa zamani achambua utendaji wa Bunge

Wednesday May 29 2019Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh

Mkurugenzi wa Taasisi ya WAJIBU, Ludovick Utouh akizungumza na wandishi wa habari alipohudhuria kongamano la viongozi wa Azaki za Kiraia Kanda ya Pwani, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Foundation for Civil Society, Francis Kiwanga. Picha na Said Khamis
Advertisement

By Elias Msuya, Mwananchi
emsuya@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali mstaafu, Ludovick Utouh amesema Bunge limeshindwa kusimamia mapendekezo ya CAG kwa Serikali huku akimtetea Profesa Mussa Assad aliyepishana kauli na Bunge hilo.
Mbali na Bunge, Utouh ambaye sasa ni mkurugenzi wa taasisi ya Uwajibikaji kwa Umma- Wajibu, amewakosoa baadhi ya mawaziri aliosema wamekimbilia kujibu mapigo ya ripoti ya CAG huku hawahusiki.
Kauli ya Utouh inakuja wakati bado fukuto la mvutano kati ya Spika wa Bunge, Job Ndugai na CAG Profesa Mussa Assad halijaisha, tangu mkaguzi huyo alipoitwa kwenye Kamati ya Maadili baada ya kusema ‘udhaigu wa Bunge’.

Baada ya Profesa Assad kusisitiza kuwa kauli yake haina makosa, Bunge liliazimia kutofanya kazi naye, bali ofisi ya CAG.
Akizungumza jana wakati wa uwasilishaji wa uchambuzi wa ripoti za CAG za miaka mitatu jijini Dar es Salaam, Utouh alisema kati ya mambo yaliyomshangaza hivi karibuni ni pamoja na mvutano kati ya Spika wa Bunge na CAG.

“Katika umri wangu huu sijawahi kusikia mambo haya popote duniani, lakini sasa nayasikia Tanzania. Msuguano kati ya Spika na CAG. CAG spoke (alizungumza) Bunge ni dhaifu,” alisema.

  • Aliendelea, “CAG anaiagiza Serikali na Bunge linatakiwa lisimamie, tumeona hapa takwimu, is that strong (Je, lina nguvu)?” alihoji Utouh.
Akizungumzia kauli za Utouh, Spika wa Bunge, Job Ndugai licha ya kukataa kutoa maoni, alihoji kwa nini Utouh asipeleke maoni hayo bungeni.
“Sitaki kutoa maoni. Sitaki kusema chochote kwa sababu huyo Ludovick tumekuwa naye siku zote na kama kweli anaona Bunge lina matatizo kwa nini asemee Dar es Salaam, awasemee ninyi asije kufanyia presentation (wasilisho) hapa Dodoma na jana (juzi) alikuwapo hapa bungeni?” alihoji Spika Ndugai kwa simu.


Kuhusu mawaziri kujibu ripoti za CAG, Utouh alisema, “mawaziri wanapanguaje hoja za CAG? Kwa sababu zile siyo siasa, inaeleza kabisa nani anahusika.

“Mtu anasimama anasema, sijaona CAG mwongo kama huyu. Wewe ‘issue’ imekuwa questioned (imehojiwa) na ilikuwa ya 2016 leo unawaambia Watanzania kwamba hiyo imekuwa questioned 2016 mzigo uko bandarini. How comes in the name of God (inakuwaje kwa jina la Mungu)?” alihoji Utouh kwa hisia kali
.

Utouh alitoa mfano wa sakata la akaunti ya Escrow ambalo baadhi ya viongozi wa Serikali walisema fedha za akaunti hiyo hazikuwa za Serikali.

“Kama mimi nilivyoumia sana wakati pesa ya Escrow imechukuliwa, nyie Watanzania mnaambiwa fedha za Escrow sio za umma na mkaamini mkapiga magoti.
“Miaka miwili baadaye, Tanesco ambayo ni mamlakaya umma inaelekezwa kulipa Sh232 bilioni. Unajua tuwe na udadisi na courage zaidi kwenye haya mambo,” alisema.


Awali, akiwasilisha uchambuzi wa ripoti tano za ufanisi za CAG, ofisa wa Wajibu, Andendekisye Mwakabalula alisema zilikuwa na mapendekezo 85 kwa taasisi 10, lakini yaliyotekelezwa ni asilimia 26 tu, huku asilimia 48 bado yanaendelea kutekelezwa na mengine 26 hayajatekelezwa kabisa.
Hata hivyo, mchambuzi wa ripoti, Jackson Mmary alisema utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG umeongezeka kwa mwaka 2017/18, Serikali ilitekeleza kwa asilimia 31, asilimia 43 yakiendelea kufanyiwa kazi na asilimia 26 hayakutekelezwa.

Wakati mwaka 2016/17, Serikali ilitekeleza kwa asilimia 21, huku asilimia 53 ikiendelea kutekelezwa na asilimia 26 yakiwa hayajatekelezwa.

Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwaipaja alisema Serikali imekuwa ikitenga bajeti kutokana na bajeti ya makadirio lakini baadaye uhalisia unaonekana kuwa tofauti. Alisema Serikali inategemea vyanzo vya mapato kupitia maduhuli, misaada, kodi, ruzuku na mikopo mbalimbali.

Alisema Serikali inatamani kupeleka fedha hizo kwa asilimia 100 lakini zinazotokana na misaada ya wadau wa maendeleo zimekuwa zikikwamisha utekelezaji huo kwa asilimia 100.

“Hata Waziri (Dk Philip Mpango) amewahi kusema mtiririko wa fedha za wadau si mzuri, lakini kumbuka mwaka huu wa fedha haujamalizika kwa hiyo fedha bado tunaendelea kupeleka,”alisema.

Kuhusu ununuzi, Mmary alisema zaidi ya asilimia 70 ya matumizi ya Serikali hutumika kwenye ununuzi na hivyo kuiweka katika hatari ya vitendo vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu.

Upungufu uliobainishwa na CAG katika eneo la ununuzi na usimamizi wa mikataba ni takribani Sh1,808.73.
“Kuna uwezekano Serikali imepata hasara ya takribani Sh1.74 trilioni kwenye ukusanyaji wa mapato, usimamizi wa matumizi, usimamizi wa manunuzi na mikataba,” alisema.


Kuhusu viashiria vya rushwa, udanganyifu na ubadhirifu, mchambuzi Mwakabalula alisema japo CAG hajaonyesha moja kwa moja kuwa kuna uwepo wa rushwa,
udanganyifu na ubadhirifu, kuna uwezekano wa kuwepo vitendo hivyo vilivyopoteza kiasi kikubwa cha fedha

Alifafanua kuwa viashiria vya makosa hayo ni kutokana na kukosekana kwa hati za malipo, mapato kutopelekwa benki, hati za malipo kuwa na nyaraka pungufu , kukosekana kwa vitabu vya risiti za kukusanyia mapato na kwenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za ununuzi.
Makosa mengine ni malipo ya huduma ambazo hazitolewa au kupokelewa au kupokelewa, malipo ya watumishi hewa, malipo katika viambatanisho vilivyorudifiwa na kupokea huduma au bidhaa isiyo sahihi au ambayo haikidhi mahitaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom