KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Ninakubaliana nawe juu ya Kabuti Kalamaganda na wengi wengine, hata huyo mama unayempamba hapa hana tofauti na hao.Haya yote ni matunda ya serikali ya mama ya awamu ya sita, kutowajaza wananchi hofu na woga.
Magufuli tutamkumbuka kama mtu katili, aliyejaza watu hofu na woga na kuwaambukiza mazuzu wake kina Profesa Kabudi roho mbaya, na vitisho na kujipendekeza kulikovuka viwango.
Tuliambiwa na Kabudi kwenye awamu ya tano kama ukubaliani nao uwasaidie tu kwa kukaa kimya kabisa.
Nadhani mama afanye afanyavyo huyu Kabudi hastahili kuwemo kwenye cabinet ya awamu ya sita hata kama sifa anazo haijarishi, bado wananchi tukimuona pale nyogo zetu zinaongezeka, hawa ni malaika wa kuzimu wa mungu wa chato.
Kinachokutoa ufahamu juu ya mama ni kwamba yeye badala ya mabavu mengi aliyotumia Magufuli, yeye anatumia dawa tofauti ya kulaza akili za watu huku matokeo yakiwa ni yale yale.
Mama anafaidika na aliyofaidika nayo Magufuli. Kama kuna wajinga wanaoendelea kumjaza upepo mama kwa kupamba "Pochi la mama" ili awaone na kuwazawadia kwa juhudi hizo, tofauti yake na Magufuli ipo wapi?