CAG Mstaafu Ludovick Utoh: Kuna ukakasi kusema Rais ametoa hela inapaswa kuwa Serikali imetoa hela kutekeleza miradi

La muhimu hizo fedha zikatumike kuleta maendeleo.

Hata wakisema wametoa Chadema sioni tatizo kama zitaenda kutumika ipasavyo na kwa mujibu wa sheria!

Punguza unafiki,najua kuacha uwezi.Fedha ni kodi za wananchi Rais anatoa wapi fedha.Zake au familia yake ebu acheni upuuuzi.
 
Mzee Ludovick Utoh, Sasa akiongoza taasisi iitwayo wajibu, alikuwa CAG kwa miaka 8.

CAG mmoja hivi amenyooka Kama rula, akipiga kila palipostahiki pasi na kusita mradi tu maslahi ya imma yasipindishwe.

Akihojiwa na Chief Odemba wa Star TV, Jana usiku alupoulizwa Kama, ni sawa kwa Viongozi kusema raisi ametoa hela za kutekeleza mradi fulani?

Lutoh anajibu, hapana, si sawa, anasema hela ni za wananchi, za umma, bunge huidhinisha matumizi yake kwa niaba ya wananchi.

Serikali Ni wakala tu, anasimamia yakiyopitishwa/ yakiyoidhinishwa na bunge. Si sawa kubinafsisha jukumu la utoaji hela za serikali (za watu) kwa Rais, sio zake.

Kwa maana hiyo, baada ufafanuzi huo wa Mh. LUDOVICK Utoh tunategemea kuona viongozi wakianza kutumia neno, SERIKALI IMETOA HELA YA MRADI X, badala ya kutumia neno RAIS ametoa, wenye akili hutafsiri kuwa hiyo ni lugha ya kujikomba kwa Rais na kumpa Ukuu wa Uwezo kifedha ambao kimsingi sio wake yeye bali ni wa wananchi.

Jumapili njema!
Lakini tambua kabisa Raisi ndio kiongozi na mkuu Serikali.
 
Lakini tambua kabisa Raisi ndio kiongozi na mkuu Serikali.
Mazoea yakiachwa yaendelee yanakua sehemu ya taratibu za jamii. Ukiona Jambo baya UNDO fasta.

Let's All Undo hizo tabia za viongozi kujikomba kwa RAIS NA RAIS kujimwambafy kuwa ataleta hela.

No, aseme Serikali italeta hela,. Basi.

Hii inafanyika kwa niaba ya watu, SISI, ndio wenye hizo hela , RAIS Ni Mtumishi wetu anafanya kwa niaba yetu kupitia Uongozi wake tuliompa sisi, kuwa mkuu wa Serikali.
 
Mzee Ludovick Utoh, Sasa akiongoza taasisi iitwayo wajibu, alikuwa CAG kwa miaka 8.

CAG mmoja hivi amenyooka Kama rula, akipiga kila palipostahiki pasi na kusita mradi tu maslahi ya imma yasipindishwe.

Akihojiwa na Chief Odemba wa Star TV, Jana usiku alupoulizwa Kama, ni sawa kwa Viongozi kusema raisi ametoa hela za kutekeleza mradi fulani?

Lutoh anajibu, hapana, si sawa, anasema hela ni za wananchi, za umma, bunge huidhinisha matumizi yake kwa niaba ya wananchi.

Serikali Ni wakala tu, anasimamia yakiyopitishwa/ yakiyoidhinishwa na bunge. Si sawa kubinafsisha jukumu la utoaji hela za serikali (za watu) kwa Rais, sio zake.

Kwa maana hiyo, baada ufafanuzi huo wa Mh. LUDOVICK Utoh tunategemea kuona viongozi wakianza kutumia neno, SERIKALI IMETOA HELA YA MRADI X, badala ya kutumia neno RAIS ametoa, wenye akili hutafsiri kuwa hiyo ni lugha ya kujikomba kwa Rais na kumpa Ukuu wa Uwezo kifedha ambao kimsingi sio wake yeye bali ni wa wananchi.

Jumapili njema!
Hata Jaji Warioba alikataa huu upuuzi wa kusema Rais katoa pesa kama mali yake binafsi, tuna taifa la watu wajinga sn
 
Hiyo ilianzia enzi za Mwendazake, lakini naona hata sasa inaendelezwa.

Inashangaza sana.

Hata Mkapa aliwahi kuonya lakini wala hakusikizwa.

Mambo ya Praise and Worship?!

Ni mpaka kiongozi mwenyewe akatae na kutoa msimamo wake juu ya hilo lakini kiukweli werevu huwa linawashanga sana!
 
Ni wale viongozi wajinga na punguani kabisa, wenye uwezo duni, wanafiki, wanaopenda kujikomba, ndiyo hutumia hiyo lugha, eti Rais ametoa hela. Ni uwendawazimu wa hali ya juu.

Hela ni za wananchi. Rais mwenyewe anatunzwa na kuhudumiwa na hela ya wananchi, halafu eti atoe hela kuwapa wanaomhudumia na kumlipa mshahara na marupurupu mengine.
 
Siku hizi eti wanaita POCHI LA MAMA!! Kuna watu kwenye nchi hii wana utani sana na kodi zetu.
Watanzania wakati mwingine huwa tunapenda sana kujadili "marginals" ambazo hata hazina tija kwa taifa letu achilia mbali hata kwenye maisha yetu binafsi. Mama ni Rais wa nchi na anafanya kila jambo kwa niaba yetu,; hajengi hotel zake za kitalii kwa fedha yetu bali kila kitu anchofanya ni kwa ajili yetu sisi. Akisema kwa mfano leo fungu A la fedha hizi ziende kwenye miradi ya maendeleleo, linaenda; kadhalika akisema fungu B liende kwenye kujenga madarasa ya Shule za Msingi, fungu hilo linaenda huko. Hii maana yake ni kwamba tumempa mamlaka ya kuamua kwa niaba yetu, tukiwa tunakubaliana na kila kitu anchoamua kwa niaba yetu. Sasa kama ukweli uko hivi, kuna shida gani mtu akisema Mama ametoa fungu B kwa ajili ya kujenga madarasa ya Shule ya Msingi, au ametoa fungu A kwa ajili ya miradi ya maendeleo? Mtu askiema hivyo kwa mfano, maadarasa ya Shule ya Msingi au miradi ya Maendeleo itakuwa ni mali ya Rais na si ya Watanzania? Mimi naomba tafadhali watu wamkosoe Mama kwa mambo ya Msingi, kama yapo. Hata yeye mwenyewe tayari alishatushauri tufanye hivyo bila kusita. Vinginevyo tumwacheni afanye kazi, tuwaombeeni Mawaziri wake waendelee kufanya kazi vizuri na waepuke kufanya kazi kwa au na mitandao
 
MSOMENI UMMY MWALIMU AKIENDELEA KUONA PESA NI ZA SAMIA:

Waziri Ummy mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa Uapisho wa Viongozi Wateule Ikulu leo Tarehe 11.10.2021.

1. Mhe Rais tunakushuuru kwa kutupa Ofisi ya Rais TAMISEMI fedha nyingi za utekelezaji wa miradi, nakuahidi kuwa tutakwenda kusimamia fedha hizo.
2. Fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa tumepokea na kesho tarehe 12.10.2021 tutatoa Mkeka wa mgawanyo wa fedha hizo za vyumba vya madarasa kwa kila Mkoa umepata madarasa mangapi kulingana na idadi ga wanafunzi wanaotegemewa kujiunga na kidato cha kwanza ukilinganisha na idadi ya wanafunzi waliomaliza kidato cha nne. Ile Gap ndio itatupa picha ya madarasa mangapi yanayohitajika ila nikuhakikishie Mhe. Raia hakuna halmashauri itakayokosa mgao wa vyumba vya madarasa.
3. Kwenye Afya Kwa Mkoa wa Shinyanga kuanzia Julai-Sept fedha zilizopelekwa ni Sh. Bil 5.2 ambazo zinaenda kujenga Zahanati 23, Vituo vya Afya 6 na Hospitali za Wilaya 5.
4. Upande wa TARURA Bajeti ya Mkoa wa Shinyanga kwa mwaka wa Fedha 2020/21 ilikua Bil 6.6 ila kwa mwaka huu wa fedha 2021/22 Bajeti ni Shilingi Bil. 16.3
5. Kwa Upande wa Mapato ya ndani Mkoa wa Shinyanga umepanga kukusanya Shilingi Bil 25.9 nitapenda kuona Mhe. Sophia Mjema asilimia 40 ya Fedha hizo takribani Sh. Bilion 9 zinakwenda kwenye miradi yabmaendeleo na Shilingi Bilioni 2 zinakwenda kwenye Mikopo ya Wanawake vijana na watu wenye Ulemavu.
6. Mhe. Rais umetupa fedha nyingi kazi yetu ni kwenda kuzisimamia tu.
 
Back
Top Bottom