CAG Mstaafu Ludovick Utoh: Kuna ukakasi kusema Rais ametoa hela inapaswa kuwa Serikali imetoa hela kutekeleza miradi

potokaz

JF-Expert Member
Jul 19, 2011
530
486
Mzee Ludovick Utoh, Sasa akiongoza taasisi iitwayo wajibu, alikuwa CAG kwa miaka 8.

CAG mmoja hivi amenyooka Kama rula, akipiga kila palipostahiki pasi na kusita mradi tu maslahi ya imma yasipindishwe.

Akihojiwa na Chief Odemba wa Star TV, Jana usiku alupoulizwa Kama, ni sawa kwa Viongozi kusema raisi ametoa hela za kutekeleza mradi fulani?

Lutoh anajibu, hapana, si sawa, anasema hela ni za wananchi, za umma, bunge huidhinisha matumizi yake kwa niaba ya wananchi.

Serikali Ni wakala tu, anasimamia yakiyopitishwa/ yakiyoidhinishwa na bunge. Si sawa kubinafsisha jukumu la utoaji hela za serikali (za watu) kwa Rais, sio zake.

Kwa maana hiyo, baada ufafanuzi huo wa Mh. LUDOVICK Utoh tunategemea kuona viongozi wakianza kutumia neno, SERIKALI IMETOA HELA YA MRADI X, badala ya kutumia neno RAIS ametoa, wenye akili hutafsiri kuwa hiyo ni lugha ya kujikomba kwa Rais na kumpa Ukuu wa Uwezo kifedha ambao kimsingi sio wake yeye bali ni wa wananchi.

Jumapili njema!
 
Magufuli ndio katuletea mkosi wote huu, unashangaa jitu kubwa zima limesimama mbele ya mwendakuzimu linaomba kitu "eti ikikupendeza" naomba abcd.

Na lenyewe likajiaminisha isipompendeza imekula kwenu, wakati ni kodi zenu.

Utamsikia eti ukiweka betri na gunzi tochi itawaka kweli?
 
La muhimu hizo fedha zikatumike kuleta maendeleo.

Hata wakisema wametoa Chadema sioni tatizo kama zitaenda kutumika ipasavyo na kwa mujibu wa sheria!
Kwa hiyo unapingana na Mzee Lutoh?

Hili haliko sawa. Hatukuwahi kulisikia kwa JK, Mkapa, Mwinyi na Nyerere.

Tuungane na Mzee Lutoh kupinga hizi lugha za kilaghai.

Mnawapa utukufu viongozi wasioustahili matokeo yake mamalaka ya wananchi ambao ndio wenye hela zao yanakua yamedogoshwa Sana.
 
Wazee wanasema sawa Sasa. Lutoh kaupiga mwingi Sanaa.
Haya yote ni matunda ya serikali ya mama ya awamu ya sita, kutowajaza wananchi hofu na woga.

Magufuli tutamkumbuka kama mtu katili, aliyejaza watu hofu na woga na kuwaambukiza mazuzu wake kina Profesa Kabudi roho mbaya, na vitisho na kujipendekeza kulikovuka viwango.

Tuliambiwa na Kabudi kwenye awamu ya tano kama ukubaliani nao uwasaidie tu kwa kukaa kimya kabisa.

Nadhani mama afanye afanyavyo huyu Kabudi hastahili kuwemo kwenye cabinet ya awamu ya sita hata kama sifa anazo haijarishi, bado wananchi tukimuona pale nyogo zetu zinaongezeka, hawa ni malaika wa kuzimu wa mungu wa chato.
 
La muhimu hizo fedha zikatumike kuleta maendeleo.

Hata wakisema wametoa Chadema sioni tatizo kama zitaenda kutumika ipasavyo na kwa mujibu wa sheria!
Basi sehemu zote zenye kutamka serikali ibadilishwe na iwekwe Rais!
Mfano mswada wa sheria unaoenda bungeni iwe inasomeka Rais kapeleka mswada Wa sheria na sio serikali!

Serikali ikipata hasara/faida basi tuseme Rais amepata hasara/faida!
Serikali ikishindwa kesi, tuseme Rais ameshindwa kesi!

Mzee Mkapa pia alilizungumza hili enzi za mwendazake!
 
Haya yote ni matunda ya serikali ya mama ya awamu ya sita, kutowajaza wananchi hofu na woga.

Magufuli tutamkumbuka kama mtu katili, aliyejaza watu hofu na woga na kuwaambukiza mazuzu wake kina Profesa Kabudi roho mbaya, na vitisho na kujipendekeza kulikovuka viwango.

Tuliambiwa na Kabudi kwenye awamu ya tano kama ukubaliani nao uwasaidie tu kwa kukaa kimya kabisa.

Nadhani mama afanye afanyavyo huyu Kabudi hastahili kuwemo kwenye cabinet ya awamu ya sita hata kama sifa anazo haijarishi, bado wananchi tukimuona pale nyogo zetu zinaongezeka, hawa ni malaika wa kuzimu wa mungu wa chato.
Chuki binafsi iliyopitiliza!
 
Mzee LUDOVICK UTOH, Sasa akiongoza taasisi iitwayo wajibu, alikuwa CAG kwa miaka 8.

CAG mmoja hivi amenyooka Kama rula, akipiga kila palipostahiki pasi na kusita mradi tu maslahi ya imma yasipindishwe.

Akihojiwa na Chief Odemba wa Star TV, Jana usiku alupoulizwa Kama, ni sawa kwa Viongozi kusema raisi ametoa hela za kutekeleza mradi fulani?

Lutoh anajibu, hapana, si sawa, anasema hela ni za wananchi, za imma, bunge huidhinisha matumizi yake kwa niaba ya wananchi.

Serikali Ni wakala tu, anasimamia yakiyopitishwa/ yakiyoidhinishwa na bunge. Si sawa kubinafsisha jukumu la utoaji hela za serikali (za watu) kwa Rais, sio zake.

Kwa maana hiyo,baada ufafanuzi huo wa Mh. LUDOVICK Utoh tunategemea kuona viongozi wakianza kutumia neno, SERIKALI IMETOA HELA YA MRADI X, badala ya kutumia neno RAIS ametoa, wenye akili hutafsiri kuwa hiyo ni lugha ya kujikomba kwa Rais na kumpa Ukuu wa Uwezo kifedha ambao kimsingi sio wake yeye bali ni wa wananchi.

Jumapili njema!
Awamu hii watu Wana nongwa Sana aisee,sijui ni kwa vile legacy inafunikwa au?

Haya serikali ya awamu ya 6 chini ya Mama wa shika mh.Rais Samia inawapa kiwewe wengi Sana aisee.Vijiba vya roho..
 
Mwenda zake ameharibu hii nchi.
Watu wamekwisha lemazwa, kutoa sifa kupitiliza kwa raisi tena kwa mambo ambayo sio kweli.

Utukufu huu uliasisiwa na mwenda zake na aliupokea sana akiwa madarakani. Akawa Mungu wao wachumia tumbo.

Watu hawa wanafikiri hiyo ndo style ya kupendwa na raisi ili upewe cheo au fedha za walala hoi kiulaini.

Tuipige vita tabia hii. Ila ilipofikia nivigumu kwa wananchi wa kawaida kuitokomeza tabia hii isipo tokomezwa na raisi mwenyewe mana wenye vyeo ndo wanao isambaza kwa gharama zetu.
 
Haya yote ni matunda ya serikali ya mama ya awamu ya sita, kutowajaza wananchi hofu na woga.

Magufuli tutamkumbuka kama mtu katili, aliyejaza watu hofu na woga na kuwaambukiza mazuzu wake kina Profesa Kabudi roho mbaya, na vitisho na kujipendekeza kulikovuka viwango.

Tuliambiwa na Kabudi kwenye awamu ya tano kama ukubaliani nao uwasaidie tu kwa kukaa kimya kabisa.

Nadhani mama afanye afanyavyo huyu Kabudi hastahili kuwemo kwenye cabinet ya awamu ya sita hata kama sifa anazo haijarishi, bado wananchi tukimuona pale nyogo zetu zinaongezeka, hawa ni malaika wa kuzimu wa mungu wa chato.
Aisee hivi Prof Palamagamba Mwaluko Sijui nani nani Kabudi yupo wapi? Kuna watu hawapati usingizi wa pono aisee

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom