OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,180
- 103,672
Namnukuu CAG Kichere
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari iliingia mkataba na “Mkandarasi Mkuu” wa shilingi bilioni 172.36 tarehe 3 Agosti 2019 wa muda wa mwaka mmoja hadi kufikia mwezi Agosti 2020 kwa ajili ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika bandari ya Tanga, kufanya tathmini ya athari za kimazingira, na kununua vifaa kwa ajili ya shughuli za bandari. Kwa kulingana na mkataba, gharama ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia meli katika Bandari ya Tanga ilikuwa ni shilingi bilioni 104.92 (asilimia 60 ya bei yote ya mkataba).
Hata hivyo, mnamo tarehe 1 Agosti 2019, “Mkandarasi Mkuu” iliingia makubaliano na “Mkandarasi Mbia” kwa ajili ya kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli kwa bei ya mkataba dola
za marekani milioni 18.15 sawa na shilingi bilioni 40.46 kwa kipindi cha miezi 11 bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari. Pia “Mkandarasi Mkuu” aliingia mkataba na “Mkandarasi Mbia” hata kabla ya kusaini mkataba wake na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Kuingia mkataba bila kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari ilikuwa ni kinyume na Kifungu Kidogo cha 4.4 cha Masharti ya Jumla ya Mkataba kati ya Mamlaka ya Bandari na Mkandarasi Mkuu ambacho
kinaizuia Mkandarasi Mkuu kutoa sehemu ya kazi kwa Mkandarasi mwingine, na ikiwa kunauhitaji wa kutoa kazi kwa Kampuni nyingine kutekeleza kazi zilizoko kwenye mkataba, Mkandarasi Mkuu anapaswa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Bandari siku 28 kabla ya kutoa kazi hiyo.
Aidha, nilibaini jumla ya malipo yaliyolipwa kwa kazi ya kuongeza kina cha lango na sehemu ya kugeuzia Meli yalikuwa dola za
marekeni milioni 18.22 sawa na shilingi bilioni 40.62, kiasi hiki, pia, kinajumuisha malipo ya dola za marekani 73,824 sawa na shilingi milioni 164.55 kwa huduma za wakala wa meli kwa “Mkandarasi mbia”. Ulinganifu wa kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu shillingi bilioni 104.92 na kiasi alicholipwa na “Mkandarasi mbia”
shilingi bilioni 40.62 inaonesha Kiasi kilichotozwa na Mkandarasi Mkuu kimezidi kiasi halisi kilichotumika kufanya malipo ya kazi hiyo kwa shilingi bilioni 64.30.
My Take
Msimamo wangu ni uleule,kwa mwendo huu ni bora nchi ikauzwa kila mtu achukue chake ajue anafanya nini. Inatia uchungu sana