CAG Ludovick Utouh Live on TBC April 21, 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG Ludovick Utouh Live on TBC April 21, 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 21, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  Baada ya kutoa ile ripoti ya ukaguzi hapo jana. Asubuhi hii, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG, Ludovick Utouh, anahojiwa live na Mtangazaji Marini Hassan Marini wa TBC.

  Endelea nami....

  Mdhibiti amesema japo ripoti yake inaonyesha serikali bado haifanyi vizuri katika kudhibiti matumizi mabaya, CAG ameisifu serikali kwa kujitahidi kudhibiti, ameisifu serikali kwa kuwa transparent kukubali kukaguliwa, na kuchukua hatua mbalimbali kutekeleza maoni ya mdhibiti.

  CAG amesema bilioni 8 zilizolipwa kwa watumishi waliofariki miaka mingi nyuma, hizo zimekwenda na maji, kisheria fedha zikishaingia account ya marehemu, haziwezi tena kutolewa, ni mali ya marehemu, hivyo ni haki ya warithi kihalali.

  Marini akambana Mdhibiti kosa ni la nani, na kwanini hakuna hatua zozote zinachukuliwa dhidi ya wahusika, hapa Mdhibiti alianza kuumauma maneno, kuwa hakuna sheria iliyovunjwa wala jinai yoyote, bali ni uzembe tuu katika kufuata taratibu na kanuni.

  CAG Utouh, amezungumzia Ripoti Chafu (Adverse Opinion) ya Kilosa kuwa haihusiani na mafuriko, kwani ukaguzi unafanywa kwenye vitabu, hakuna ofisi yoyote ya serikali iliyokubwa na mafuriko, bali watendaji wameamua kuficha vitabu vya mahesabu kwa makusudi, hivyo kumbe taarifa hiyo chafu, sio ya ukaguzi, bali ni kutokaguliwa. Hivyo kumbe Utouh amewalipua tuu.

  Utouh amewaahidi Watanzania, kuwa baada ya taarifa hiyo kutinga Bingeni, serikali inatakiwa kuandaa majibu kwa hoja zote alizoziibua na kuyapeleka majibu hayo Bungeni na yeye Mdhibiti kupatiwa copy ili taarifa yake ya ukaguzi ya mwaka unaofuata, ataambatanisha nini kilichotekelezwa na nini bado, na sababu za kile ambacho hakikutekelezwa.

  Kipindi, kimemalizika.

  Mimi binafsi, namkubali sana huyu Mtangazaji, Marini Hassan Marini, anajiamini, ikitokea mahali pa kupigilia misumari, anakomalia kisawasawa, bila kumuogopa anayemhoji ni nani, na hivyo ndivyo interview zinavyopaswa ziwe, sio kubembeleza, ama kuenga enga, kazi ya mtangazaji wa mahojiano, ni ku shoot tuu maswali.

  Asanteni.
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu Pasco,

  Shukrani kwa update hizi lakini hapa naona ni kuuma na kupuliza, wasiwasi wa nini hasa?
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,605
  Trophy Points: 280
  CAG naye ana play PR na serikali, ameuma kwa ripoti kali na kupulizia kuwa serikali ni sikivu, ukweli JK anatake a very good care huyu CAG, hivyo lazima Utouh amsifu JK is doing the best ila watendaji wake ndio wanaomwangusha, kama ilivyo kwa CCM kama chama, ni chama kisafi kabisa ila baadhi ya viongozi wake ndio wanakichafua.
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu nilipo-bold hapo...

  Kuna chama bila hao wanachama? Na kama chama ni watu, watu wakiwa wachafu chama hicho utakiitaje kisafi? Let's call a spade just a spade!
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nilitarajia kuwa ataifagilia Serikali.Serikali ni lazima ikaguliwe tupo katika mfumo wa vyama vingi.Hawana ujanja mazingira yanawalazimisha kukubali kukaguliwa otherwise wasingekubali..
   
 6. Sauti za Wananchi

  Sauti za Wananchi Member

  #6
  Dec 15, 2017
  Joined: Sep 2, 2014
  Messages: 88
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 25
Loading...