CAG Kichere hongera sana, tena sana!

the glassroof

JF-Expert Member
Apr 25, 2017
259
500
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana na ripoti za idara hii muhimu serikalini ya CAG.

Kwa kweli ukipata watu wanaofanya kazi zao kwa weledi na wenye hofu ya Mungu utajifunza mengi sana hususani kwenye hizi nchi za dunia ya tatu.

Nafikiri kwa uwazi huu huu, ndio uliomfanya CAG kabla ya huyu tuliyenaye sasa kupokonywa tonge mdomoni, hayo mambo ya ukweli na uwazi bwana!

Ukweli ni kwamba, ili nchi iende mbele tunahitaji mambo haya sana, lakini najaribu kuwaza kwa akili zangu ndogo tu na kubaki na maswali yafuatayo: Hawa CAG team, wanafanyaje kazi yao? Je?

Wanakagua mahesabu ya serikali baada tu ya shughuli zote za serikali kukamilika au wanahusishwa pia kwenye michakato ya manunuzi ya serikali?

Kama ndivyo, je mapendekezo yao huwa yana nguvu gani kabla ya hasara kama hizi kujitokeza?

Na kama wana fursa ya kupendekeza jambo lolote kabla ya hatari, mapendekezo yao husikilizwa na nani haswa?

Je, Mtawanyiko wao katika idara za serikali ukoje, au wapo wapo tu kama idara ya nyeti ya TISS, kwamba hawafahamiki sana miongoni mwetu wananchi wa kawaida?

Kama wapo hadi ngazi za chini kwa maana ya kijiji au kitongoji, nini jitihada zao katika kupambana na kuzuia matumizi mabaya ya fedha za serikali kabla ya hatari?

Kama ni wachache, kwanini serikali isiwekeze nguvu zaidi katika idara hii muhimu sana kwa ustawi wa nchi zetu changa kwa kusomesha, kuwajengea uwezo na kuwaajili kila kona ya nchi hii ili tuokoe pesa nyingi badala ya kusubiri kuja kufichua uovu wakati pesa ilishateketea?

Naamini pesa za kuwaajili hawa watu kila kona zitakuwa ndogo tu kulinganisha na upotevu wa mabilioni ya pesa yanayopotea kila mwaka.

Na hapa ndio sehemu pekee na nzuri ya ajira kwa vijana, tena ya kizalendo kabisa kuliko kila mwaka tunalia hatuna uwezo wa kuajili wakati mabilioni yanapigwa na wajanja na wanaendelea kupeta tu mtaani. Inauma sana ndugu zangu

Inaonekana chombo hiki kinakagua vizuri sana serikali pamoja na idara zake. Wao kama zilivyo taasisi nyingine za serikali tunaamini pia wanatumia pesa za serikali kuendesha shughuli zao.

Je, wanakaguliwa na nani ili nasisi wananchi wa kawaida tujiridhishe na usafi wao ili tusije hisi kuwa ni kakitengo fulani tu kanakofanya kazi kwa ajili ya maslahi ya kundi fulani tu la watu wachache kwa maslahi binafsi ama kufurahisha uongozi ulioshika hatamu

Kama idara hii nyeti itakuwa nyuma ya wanasiasa ndugu zangu tumekwisha kabisa, ni vyema nao tujue wazi wanatumiaje raslimali zetu kwa uwazi kabisa na wawe kwanza kutueleza bajeti yao na matumizi yao kabla hata hawajaanza kueleza madudu ya idara za serikali, lakini pia wawepo wengine nyuma yao kuhakiki hicho wanachokisema kama ni kweli au la.

Najua inaweza kuwa ngumu lakini hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Kwa maana hakuna malaika hapa duniani na kamwe hatotokea, hivyo tunaweza jikuta tunayumbishwa sana kama taifa na vyombo vyetu hivi ili tukose pa kusimamia kwa sababu tu ya mifumo yetu mibovu iliyojikita zaidi kuibua changamoto kuliko kuzizuia ama kuzikabili.

Kwa wakubwa wenzangu mtakumbuka kuwa hata kwa marehemu Mkapa tulisikitika sana, kwa Mzee Kikwete tulisikitika pia, Hayati Magufuli vivyo hivyo pengine zaidi, naamini pia na mama yetu Samia hatotoka salama katika hili, kwa kuwataja wachache

Wazo langu, kitengo hiki kiwe kama TAKUKURU, yaani wajikite zaidi katika Kuzuia na Kupambana na matumizi mabaya ya fedha za serikali katika idara zote ili kuokoa pesa zinazopotea kila mwaka, kuliko mtindo wanaoenda nao sasa.

Angalizo, tukiwaajili kila ngazi na wakafahamika huenda nao wakaingia kwenye mkumbo wa rushwa tukashindwa kupata clear data, sema labda waundiwe sheria ngumu zaidi ili nao wakibainika kukiuka maadili ya kazi yao ikiwemo basi wapewe adhabu kali zaidi kuliko mtu mwingine yeyote yule ikiwemo hata kunyongwa kabisa endapo itathibitika hivyo. Vinginevyo hizi hadithi hazitakuwa na mwisho kabisa, na itakuwa mtaji wa kisiasa tu kila uchwao

Naamini wanachofanya wao kwa sasa, Ufujaji ufanyike kwanza ndio wao wapite kukagua, hapa kila mwaka wataibua tu maovu mengi tena sana. Niko radhi kwa ufahamu wangu mdogo nikosolewe katika hili.

Kingine ni kuwa, hata viongozi wetu tulionao kwa nyakati zote pengine wametokana na veting mbovu ama kubebana au kujuana, sasa tusitegemee wakawa na weledi katika matumizi sahihi ya pesa hata siku moja.

Kubwa kuliko yote, wana siasa wetu hawana rangi maalum wanabadilika kulingina na mazingira na matakwa ya viongozi walio juu, hili nalo ni hatari sana na sumu kwa taifa letu lina linalohitaji utashi wa ndani ili tutoke hapa tulipo.

Suluhu ya muda mrefu ninayoiona, ni kukamilisha mchakato wa katiba yetu mpya ili tupate viongozi stahiki tena kwa kuzingatia taaluma zao kwa ngazi zote kuanzia mawaziri na mpaka huku chini na si vinginevyo.

Bila hivyo, sitapiga tena kura kama nilivyofanya mwaka jana, endeleeni tu kunichagulia muwapendao nyie, mie bado naona mazingira hayako sawa kwa sasa ila naamini ipo tutavuka tu upepo huu, kama tulivyowatoa wakoloni, hivyo hata ukoloni wa kifikra utatoweka tu.

Poleni sana kwa kuwachosha na uandishi wangu mbovu, mimi ni msomaji tu, ni mvivu sana wa kuandika. Ahsanteni!
 

dali kimoko

Member
Jan 25, 2021
76
150
Sawa sawa
Kwako Madam Presdent, nadhani ripoti ya CAG umeiona na kila kitu kiko wazi, watu wapo na wametajwa na ushahidi upo yaani DPP hana kazi kbs, chukua hatua sasa tuanzie hapo km kweli una dhamira ya kweli ya kutukomboa ktk hali mbaya ya uchumi, haiwezekani watu wanalipana mabilioni na hawatoi efd receipt,wakt huku mtaani tra wanatunyanyasa na viduka vyetu utadhani tumeua,sioni sababu y akutajwa au kusomewa hii repoti km hakuna ACTION yoyote kila mwaka itakua ni business as usual, ni afadhali mkae kimya tu hakuna sababu.!
 

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,734
2,000
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana na ripoti za idara hii muhimu serikalini ya CAG.


Kwa kweli ukipata watu wanaofanya kazi zao kwa weledi na wenye hofu ya Mungu utajifunza mengi sana hususani kwenye hizi nchi za dunia ya tatu..

Nadhani pongezi za dhati kabisa anatakiwa apewe Mwenyezi Mungu kwa Ufundi wake na kwa Israeli kutekeleza Majukumu yake, kwani naamini bila Wawili hawa Kufanya yao huyu CAG Wetu asingethubutu ( narudia asingethubutu ) kamwe kuja na Ripoti yake ile ya Jana. Asante Mungu.
 

kajembejr

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
1,231
2,000
Hamna kitu ,mbona hatukuona report ya namna hii akiwa chini ya Jiwe?Au ameanza kazi juzi baada ya kifo cha Magu?
 

WAIKORU

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,370
2,000
Nadhani pongezi za dhati kabisa anatakiwa apewe Mwenyezi Mungu kwa Ufundi wake na kwa Israeli kutekeleza Majukumu yake, kwani naamini bila Wawili hawa Kufanya yao huyu CAG Wetu asingethubutu ( narudia asingethubutu ) kamwe kuja na Ripoti yake ile ya Jana. Asante Mungu.
Kwa kweli Mungu anatupenda Watanzania...kwa hili hakika ametupigania..

Sifa na utukufu vimrudie yeye pekee....
 

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
4,631
2,000
Hii ripoti itakuwa imeeditiwa ndani ya hizi wiki 3. Hakuna kijogoo kingeweza kuwika Kwa Magu. Hizi ripoti sio uhalisia Bali matakwa ya Watawala.
 
  • Thanks
Reactions: mmh

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,262
2,000
Hii ripoti itakuwa imeeditiwa ndani ya hizi wiki 3. Hakuna kijogoo kingeweza kuwika Kwa Magu. Hizi ripoti sio uhalisia Bali matakwa ya Watawala.
Ule utamaduni wa kujiuzulu endapo kiongozi umebanwa na huwezi kutimiza majukumu yako kutokana na shinikizo la mkubwa wako ni utamaduni mzuri sana. Mbona hakuna hata mmoja aliyejiuzulu hata baada ya kuona madduddu haya yote?!
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
899
1,000
Kwako Madam Presdent, nadhani ripoti ya CAG umeiona na kila kitu kiko wazi, watu wapo na wametajwa na ushahidi upo yaani DPP hana kazi kbs, chukua hatua sasa tuanzie hapo km kweli una dhamira ya kweli ya kutukomboa ktk hali mbaya ya uchumi, haiwezekani watu wanalipana mabilioni na hawatoi efd receipt,wakt huku mtaani tra wanatunyanyasa na viduka vyetu utadhani tumeua,sioni sababu y akutajwa au kusomewa hii repoti km hakuna ACTION yoyote kila mwaka itakua ni business as usual, ni afadhali mkae kimya tu hakuna sababu.!
Hawezi chukua hatua yoyote..............maana kaanzisha msemo mbaya sana wa kwa "ukizingua tunazinguana.." neno la mwisho linamaanisha hapatakuwa na mshindi akimchukulia hatua huyu na yeye atachukua hatua kupitia kona nyingine.

Uongozi ulikuwa umefuga wanafiki wengi kupita maelezo (mercenaries and traitors) wakijitabanahisha kuwa ni sehemu yao kumbe ni binadamu na fisi kuvizia mkono uanguke autafune.

Kwa hali hii jinsi inavyoendelea na baadhi ya watu hasa wale walioumizwa na utawala wa hayati kwa sababu mbalimbali kwa kumshambulia kupitia ripoti ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali itaipelekea familia na wananchi wanaohisi kutendea ndivyo sivyo kuamini kwamba hao wanaomtuhumu ama kwa kificho au hadharani kwa walimuua.

Hii tahadhari binafsi naitoa maana huenda ndicho kitakachotolewa tamko na familia pamoja na wananchi ambao bado waamini hayati aliyokuwa akitenda ni kwa manufaa ya nchi hivyo kushikwa ghadhabu itakayosababisha mfarakano usiokuwa na tija.

Mwaka jana CAG alipowasilisha ripoti yake aliambia na hayati kwamba kuna mambo mengine hakuyagusa hivyo alitegemea ripoti itakayofuata itagusa ATCL na mashirika mengine kwa uwazi zaidi na ndio kazi hii iliyotokea sasa hivi ijapokuwa bado kuna mengine hayajawekwa kwenye ripoti sijui kwa sababu zipi?
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
23,318
2,000
Who will watch the watchers?

Quis custodiet ipsos custodes?
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
4,943
2,000
Ukimpa Hongera kwa kutoa hii Ripoti (tena kwa kuambiwa lazima iwe wazi zaidi) Je utampa lawama kwa kipindi kile ambapo hakuwa wazi zaidi (sisemi kwamba angelazimisha kusema ya kusema na kuhatarisha ustawi wake) Je alilazimishwa kuchukua kazi (huenda utasema hakujua) ila mwenzake aliyetoka alitokaje ?, Kwahio yeye alijua fika haendi kuchunguza kila anachotaka bali kuonyesha kile wanachotaka...

Kwangu the Jury is Still Out....
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
899
1,000
Ule utamaduni wa kujiuzulu endapo kiongozi umebanwa na huwezi kutimiza majukumu yako kutokana na shinikizo la mkubwa wako ni utamaduni mzuri sana. Mbona hakuna hata mmoja aliyejiuzulu hata baada ya kuona madduddu haya yote?!
Hata sasa walitakiwa wajiuzulu wote kuanzia kichwa hadi miguu halafu Jaji mkuu akaimu kwa muda kipindi cha mpito.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom