CAG: Kama tunataka kuongeza kodi tuachane na malipo kwa pesa taslimu, tutumie kadi

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968

Mkaguzi wa mapato na mahesabu ya serikali amesema matumizi ya kadi za kielekroniki kwenye mihamala itazuia ukwepaji kodi na kuongeza mapato kwa kuwa rekodi zinakuwa rahisi kupatikana na kufuatilia.
Amesema ununuzi kwa kutumia pesa taslimu unahamasisha wizi kwa kuwa mtu anaweza kununua nyumba lakini wakakabidhiana pesa bila kulipa kodi
 
Ana maanisha tuwe na credit kadi au
 
Mawazo ya aina hiyo ndiyo yatakayoivusha nchi kutoka hapa tulipo. Lakini hizi mbinu za kipolisi eti usipodai risiti utapelekwa jela miaka mitatu ni uzembe wa akili tu. Unakusanya kodi kwa kutisha watu!!!???
 
Mkaguzi wa mapato na mahesabu ya serikali amesema matumizi ya kadi za kielekroniki kwenye mihamala itazuia ukwepaji kodi na kuongeza mapato kwa kuwa rekodi zinakuwa rahisi kupatikana na kufuatilia.
Amesema ununuzi kwa kutumia pesa taslimu unahamasisha wizi kwa kuwa mtu anaweza kununua nyumba lakini wakakabidhiana pesa bila kulipa kodi

anachosema ni sahihi kabisa, nisuala la maxmalipo kuongeza wigo wa matumizi ya card za udart, zitumike kama debit card,
 
Inashangaza mno kuona kwamba kila mwenye akaunti benki anapatiwa kadi lakini asilimia kubwa ya hizi kadi hazimpi mmiliki uwezo wa kufanya malipo. Hii cash culture tuliyonayo inaonekana hakuna mwenye uharaka wa kuiondoa; karne ya 21 hatupaswi kushindilia hela kwenye soksi au kubeba mfuko wa hela kwenda kununua gari.
 
Wazo zuri sana aisee, nasi tufanane na nchi zilizoendelea. Ni ajabu sana mtu unanunua gari milioni 50 mpaka mia na mtu analipa cash ama kiwanja. Vilevile wahuhishe na TIN,

Hivi data base ya vitambulisho vya NIDA kwanini isitumike kukusanyia taarifa za watu ama zile za NEC.?
 
teknolojia yetu tatizo ipo chini sana mkuu
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Mkaguzi wa mapato na mahesabu ya serikali amesema matumizi ya kadi za kielekroniki kwenye mihamala itazuia ukwepaji kodi na kuongeza mapato kwa kuwa rekodi zinakuwa rahisi kupatikana na kufuatilia.
Amesema ununuzi kwa kutumia pesa taslimu unahamasisha wizi kwa kuwa mtu anaweza kununua nyumba lakini wakakabidhiana pesa bila kulipa kodi

Hivi ni wananchi wangapi wanatumia benk kuweka na kutoa pesa
 
Ni wazo lililoenda shule sana, ila shida inabaki kuwa utatumiaje kadi wakati watu asilimia 90 hawana akaunti benki na pia nchi haina hata vitambulisho vya utaifa? Safari bado ni ndefu

Mkuu ni kweli kwetu hiyo kitu kuja kufanikiwa , inhitataji walau 0.24% ya bajeti yetu kwa maana masuper maketi yote ,vituo vya mabasi vyote lazma ziwe na hio miundo mbinu ,sasa kama mambo madogo tu kama ya nida yametushinda wanaomiliki atm ni wangapi na kwa nin tukimbilie mambo makubwa kiasi hicho ili hali mambo madogo kama electronic ticket kwenye vianja vyetu yametushinda ,

E payment ni muhim sana anzia kwenye mabasi yetu ,na kwenye huduma nyingine lakin kwangu mim naona bado tukomae kwanza na EFD
 
Wazo zuri sana aisee, nasi tufanane na nchi zilizoendelea. Ni ajabu sana mtu unanunua gari milioni 50 mpaka mia na mtu analipa cash ama kiwanja. Vilevile wahuhishe na TIN,

Hivi data base ya vitambulisho vya NIDA kwanini isitumike kukusanyia taarifa za watu ama zile za NEC.?
Hiyo labda tukimaliza kujenga lile jengo ambalo mkulu ametupatia 12bil tukajenge pale idodomya kwa ajili ya makao makuu yetu,

Ila swalk lako ni zuri nami nimekujibu kwa maelekezo
 
Am sore. Hata Marekani, wanaoweza kulipua dunia mara kadha na silaha zao za nyuklia, hawawezi kutegemea kukusanya kodi yao kwa mfumo wa kadi.

Kwanza ni maduka makubwa mangapi yenye mfumo wa kulipa kwa kadi? Achia mbali maduka madogo ambayo ndiyo mengi.

Kadi ni njia mojawapo tu. Tusitegemee kwamba tunaweza kuondokana na hela taslimu kwa sasa.
 
Back
Top Bottom