JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,458
“Hali mbaya zaidi ilibainika katika magereza ya kilimo ambapo wafungwa walikuwa wakilala katika vyumba zilivyojengwa kwa mabati. Hali hii ilibainika katika Magereza ya Kilimo ya Ushora na Kingurungundwa,” - CAG.
Bweni la wafungwa la Kilimo ya Ushora lilipigwa picha na kuonekana likiwa limezungushiwa mabati yanatoonekana kuchoka.
Ameongeza kuwa: “Nyumba nyingi za wafanyakazi wa magereza zilizotembelewa zilikuwa katika hali mbaya kwa sababu ya ukosefu wa matengenezo na ukarabati. Nyumba za watumishi wa magereza zilikosa maji safi na ya kutosha.
“Mifumo ya majitaka ilikuwa chakavu na mingi ilikuwa ikivuja. Hali hii ilibainika katika magereza sita ambayo ni magereza makuu ya Keko na Butimba; Magereza ya Wilaya za Kilwa, Manyoni, na Ukerewe; na Magereza ya kilimo ya Kingurungundwa na Kwa Mngumi.
“Jeshi la Magereza halikuwa na mipango ya matengenezo ili kusaidia shughuli zake za ukarabati wa majengo na hakukuwa na bajeti iliyotengwa kwa madhumuni ya ukarabati na matengenezo.
“Kutokana na ukarabati na matengenezo hayo ya miundombinu ya magereza kukosa bajeti, shughuli hizo ziliachwa kwa magereza husika ambapo ukarabati ulifanyika kwa kutumia vyanzo vya fedha vya ndani ya magereza husika.
“Pia, kutokana na ufinyu wa fedha, ukaguzi ulibaini kuwa kwa magereza yote 15 yaliyotembelewa, kiasi cha shilingi milioni 38 kilipelekwa kwa magereza husika kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za askari isipokuwa Wilaya ya Ukerewe iliyopokea shilingi milioni 76 kutokana na hali ya nyumba za maofisa wa magereza kuwa mbaya zaidi.
“Imeelezwa kuwa, fedha zilizotolewa zilitoka katika vyanzo mbalimbali kama vile faida iliyotokana na miradi ya uwekezaji inayotekelezwa na Jeshi la Magereza nchi nzima.”