CAG: DPP amekusanya zaidi ya Sh. Bilioni 60 na hazijatumika kwa sababu hakuna Sheria ya Matumizi yake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,902
141,845
CAG Kichere amesema Mkurugenzi wa Mashtaka nchini amekusanya zaidi ya sh bilioni 60 kutokana na kesi mbalimbali na fedha hizo hazijatumika kutokana na kukosekana kwa sheria na mwongozo wa namna ya kuzitumia.

CAG amelishauri Bunge kutunga sheria ya matumizi ya fedha hizi.

Ukinizingua Nitakuzingua!
 
Hii taarifa simply inamaanisha DPP alikuwa anafanya kazi isiyomhusu na isiyotambulika kisheria, kwa ufupi DPP alikuwa mnyan'ganyi.

Nichukue fursa hii kuwashauri wale wote waliotapeliwa pesa zao na DPP waende mahakamani kudai haki yao, nina hakika kabisa watashinda hizo kesi, watafute mawakili wanaoeleweka tu.

Kama mwendazake angekuwa hai hizo pesa zingeshapata matumizi.
 
CAG Kichere amesema Mkurugenzi wa mashtaka nchini amekusanya zaidi ya sh bilioni 60 kutokana na kesi mbalimbali na fedha hizo hazijatumika kutokana na kukosekana kwa sheria na mwongozo wa namna ya kuzitumia.

CAG amelishauri bunge kutunga sheria ya matumizi ya fedha hizi.

Ukinizingua Nitakuzingua!

Hizo si ndio zilienda kufichwa CHINA kwa Kairuki?
 
Hazijatumika siyo kwa sababu ya sheria ni kwa sababu aliyezitaka kaondoka angekuwepo wala asingehitaji sheria yangekuwa maelekezo tu, Nampongeza sana tena kwa dhati ya moyo wangu DPP, amefanya kazi nzuri sana (wasikilizaji wanapiga makofi, DPP ananyanyuka na kuinama) kaa tu DPP, amekusanya ndani ya miezi 4, 60B hizi ni fedha za watanzani maskini zilichukuliwa na wachache ila kwa sheria tuliyoipitisha bungeni na kwa hili nimpongeze Spika mtani wangu kwa kuhakikisha sheria inakamilika na tumeifanyizia kazi na haya leo ndiyo matunda yake

Sasa naelekeza hizo bilioni 60 zipelekwe Tanroads zikajenge mabarabara na madaraja na miundombinu mingine watu wa hazina mlisimamie hili kikamilifu(makofi), au nimefanya vibaya ndugu zangu, Asanteni sana
 
Hii taarifa simply inamaanisha DPP alikuwa anafanya kazi isiyomhusu na isiyotambulika kisheria, kwa ufupi DPP alikuwa mnyan'ganyi.

Nichukue fursa hii kuwashauri wale wote waliotapeliwa pesa zao na DPP waende mahakamani kudai haki yao, nina hakika kabisa watashinda hizo kesi, watafute mawakili wanaoeleweka tu.
Hawatatoboa abadani.
 
Hazijatumika siyo kwa sababu ya sheria ni kwa sababu aliyezitaka kaondoka angekuwepo wala asingehitaji sheria yangekuwa maelekezo tu, Nampongeza sana tena kwa dhati ya moyo wangu DPP, amefanya kazi nzuri sana (wasikilizaji wanapiga makofi, DPP ananyanyuka na kuinama) kaa tu DPP, amekusanya ndani ya miezi 4, 60B hizi ni fedha za watanzani maskini zilichukuliwa na wachache ila kwa sheria tuliyoipitisha bungeni na kwa hili nimpongeze Spika mtani wangu kwa kuhakikisha sheria inakamilika na tumeifanyizia kazi na haya leo ndiyo matunda yake

Sasa naelekeza hizo bilioni 60 zipelekwe Tanroads zikajenge mabarabara na madaraja na miundombinu mingine watu wa hazina mlisimamie hili kikamilifu(makofi), au nimefanya vibaya ndugu zangu, Asanteni sana
Watajitahidi sana hawatashinda. Tusubiri miezi mitatu ijayo muelewko utapatikana
 
CAG Kichere amesema Mkurugenzi wa mashtaka nchini amekusanya zaidi ya sh bilioni 60 kutokana na kesi mbalimbali na fedha hizo hazijatumika kutokana na kukosekana kwa sheria na mwongozo wa namna ya kuzitumia.

CAG amelishauri bunge kutunga sheria ya matumizi ya fedha hizi.

Ukinizingua Nitakuzingua!
Kule Uingereza mtu akifa bila kuacha wosia na hana next of kin hela zake huchukuliwa na crown yaani zinakuwa za umma. Pamoja na ushamba wangu siwezi kuona ni jinsi gani faini inayolipwa mahakamani ikose matumizi. Zineanza leo? Tutayajua mengi, lete butamu.
 
DPP hakusanyi faini za mahakama bwashee

DPP ananegotiate na wahujumu uchumi kwa mujibu wa sheria ili warudishe fedha walizofisadu kisha waachiwe huru!
Hapa unazungumzia mabilioni siyo huto tufaini twa mahakamani.
 
Back
Top Bottom