figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nchini Tanzania, Profesa Mussa Assad amesema siyo jambo jipya ofisi yake kufanyiwa ukaguzi, akisema hatua hiyo hufanyika kila mwaka na taarifa kuwasilishwa Kamati ya Bunge la Hesabu za Serikali (PAC).
Profesa Assad alisema hayo jana Jumanne Juni 13, 2019 wakati akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam.
Alisema baada ya kukamilika kwa ripoti hiyo ya ukaguzi, huwasilishwa kwa kamati hiyo kabla ya kusomwa bungeni.
“Tunakaguliwa kila mwaka na mkaguzi wetu kama kawaida atateuliwa na PAC ya Bunge atafanya kazi yake, akimaliza atatoa ripoti na kuitazama sisi na kusainiwa na audit committee halafu hesabu hizo zitapelekwa kwa mwenyekiti wa PAC ili kusoma bungeni.”
“Hayo ni mambo ya kawaida kabisa katika utendaji wa taasisi yetu na siyo jambo jipya, ni matakwa ya kisheria,” alisema Profesa Assad.
Mei 16, 2019, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alitoa taarifa bungeni kwamba kwa mujibu wa sheria ya ukaguzi wa umma, hesabu za ofisi ya CAG zinakaguliwa na Bunge kupitia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).