CAG asikague mahesabu tu, bali adhibiti mapato na matumizi ya fedha za serikali pia

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,656
18,310
CAG ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serilali lakini mara nyingi inaonekane GAC anakagua mahesabu ya serikali, lakini hafanyi udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali.

Kazi ya CAG inapaswa pia kudhibiti jinsi fedha za serikali zinavyotumika, la sivyo naona hatutaondokana na haya madduddu ya kila mwaka.

Au mnijulishe ni nani anayefanya udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa?
 
Ni mkaguzi na mdhibiti wa Hesabu za Serikali SI mdhibiti wa matumizi ya fedha hizo. Kila idara ina watu ambao hufanya kazi hiyo ya kudhibiti matumizi hayo. CAG hufanya ukaguzi kwa hao waliopewa jukumu la kudhibiti na kuona kama kweli wametekeleza hayo. Wanaoshindwa kufanya hivyo CAG anawaripoti . Hii ndo kazi yake.
 
Unataka manunuzi na matumizi mengine kabla hayajafanyika yapitie kwake? eg Quotations, Pos, invoices etc?
 
Assad alijaribu kidogo tu kukemea yakamkuta ya kumkuta kwamba angepelekwa Bungeni kwa pingu awe hai ama hahemi.
Hii nchi ina vituko kibao!!

Huyu CAG wa sasa kaanika kila kitu, sasa CCM chatoh inalalamika eti wamebumba riport kumuharibia marehemu legacy aliyoiacha!!
 
Kaka unafahamu udhibiti?

Matumiz ya fedha za serikal huwa znakwenda sehemy husika kukiwa na bajet yake.

Sasa pale ambapo hizo sehemu znakwenda kutumika nje ya bajet ama utaratibu. Ndipo CAG anapokuja kutoa ripot kwa serikal ili iweze kukemea na kuchua hatua stahiki.

Ifahamike kuwa ...

1. CAG hana mamlaka ya kufukuza mtu ndan ya serikal
2. CAG ni mkaguzi tu, hana mamlaka yoyote ile
3. CAG hayo mnayoyaona kuwa ni makosa, ukizama kwa undani kabisa utaona hayo ni nusu tu. Unaweza kuta TPA inanunua laptop kwa ajili ya kazi zao, bei ya laptop moja ukakuta ni 5ml. Antivirus ya 20k mpka 30k ukakuta ni laki 5. Na unakuta kabisa kuna risit za hayo mambo, kwahiyo CAG hapo hana ujanja, anapitisha tu.

Kwahiyo ni partial tu wala sio mambo kamili.
 
Lakini CAG ni mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali, ilipaswa kuwepo ofisi huru yenye kudhibiti matumizi ya fedha za serikali, haiwezekani serikali ikajidhibiti yenyewe, ndio madudu yanapoanzia.
 
Ile MDHIBITI ndiyo ambayo serikali haitaki kuisikia kabisa !! yeye ni kukagua na kutoa recommendations zake basi.
 
CAG ni mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serilali lakini mara nyingi inaonekane GAC anakagua mahesabu ya serikali, lakini hafanyi udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali.

Kazi ya CAG inapaswa pia kudhibiti jinsi fedha za serikali zinavyotumika, la sivyo naona hatutaondokana na haya madduddu ya kila mwaka.

Au mnijulishe ni nani anayefanya udhibiti wa matumizi ya fedha za serikali kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa?
Hili linapaswa kuingia moja kwa moja kwenye katiba mpya
 
Lakini CAG ni mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali, ilipaswa kuwepo ofisi huru yenye kudhibiti matumizi ya fedha za serikali, haiwezekani serikali ikajidhibiti yenyewe, ndio madudu yanapoanzia.
Nadhan mkuu huna uelewa mpana wa mambo haya, kila ofisi ya serikal ina mkaguz. Anafahamika kama internal auditor, ama mkaguz wa ndani.

Huyu ndie mwenye majukumu hayo. Bado tuna mifumo mibovu hapa afrika juu ya matumiz ya fedha za umma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom