CAG aonyesha jinsi watanzania tunavyopigwa ada ya ukaguzi wa magari

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,185
103,702
Kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Masharti Maalum ya
Makubaliano ya Uhakikisho wa Kukidhi Vigezo Kabla ya
Kusafirisha Bidhaa (PVoC) kati ya TBS na watoa
huduma wanne (4) kwa magari yaliyotumika kwa
kipindi cha mwezi Machi 2018 hadi mwezi Februari
2021, ada ya ukaguzi inayotakiwa kutozwa ni Dola za
Kimarekani 150 kwa gari (Machi 2015 hadi Februari
2018 ilikuwa Dola za Kimarekani 140) ambapo Shirika
la Viwango linapata asilimia 30% ya kiasi hicho.
Katika mapitio ya biashara ya magari
yaliyotumika kwa makampuni matano (5) yajulikanayo
kama SBT Japanese Vehicle, Beforward, Auto
Japan, Tradecarview na Real Motors Japan nilibaini
kuwa kwa kipindi cha kati ya tarehe 5 Novemba 2018
na 15 Desemba 2018, wateja walioomba Ankara kifani
walitozwa kati ya Dola za Kimarekani 300 mpaka 380
ambazo zimeleta wastani wa Dola za Kimarekani 316
kwa gari moja kiasi ambacho ni zaidi ya kiwango
kilichoidhinishwa cha Dola za Kimarekani 150 kwa
wastani wa Dola za Kimarekani 166.

Kwa mujibu wa ripoti ya TBS ya Uhakikisho wa Kukidhi Vigezo Kabla ya Kusafirisha Bidhaa, kutoka kwa mawakala wa PVoC, jumla ya magari 57,031 yalikaguliwa nchini Japan kwa ajili ya kuingizwa nchini
Tanzania kati ya tarehe 1 Januari 2017 na 30 Septemba 2018, jumla ya ada ya ukaguzi ya ziada ya Dola za Kimarekani milioni 9.47 (sawa na Sh. bilioni 20.92)
zilitozwa kwa Watanzania na taasisi mbalimbali.
Wauzaji wa magari kwa sasa hawaratibiwi na hawajaandikishwa na TBS hivyo kuondoa dhana nzima
ya kulinda maslahi ya mteja. Ninapendekeza kuwa TBS
ianzishe kampeni ya ufahamu kuelimisha jamii juu ya
kiasi wanachostahili kutozwa na wauzaji wa magari ya mtumba.
 
Back
Top Bottom