CAG ‘anusa’ ufisadi Bandari, DART, Bohari Kuu

Ombudsman

JF-Expert Member
Apr 18, 2012
3,565
3,729
Profesa Mussa Assad ametoa ripoti ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof Mussa Juma Assad akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma jana. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Aeshi Hilaly na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Abdallah Chikota. Picha Emmanuel Herman
Dodoma. Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ametoa ripoti ya ukaguzi wa mashirika 102 ya umma kati ya 186 kwa mwaka wa fedha 2014/15 na kubainisha maeneo yenye harufu ya ufisadi, ubadhirifu na ukiukwaji wa mikataba na sheria.

Miongoni mwa maeneo yaliyobainishwa katika ripoti hiyo ni ufisadi unaodaiwa kufanywa na Bohari Kuu ya Dawa (MSD), Wakala wa Usafiri wa Mwendo Kasi Dar es Salaam (DART), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na mashirika mengine ya umma.

Mbali ya mashirika hayo, CAG alisema Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ni mzigo kwa kutokuwa na ndege za kutosha, gharama za uendeshaji zisizohimilika, uhaba wa mtaji wa kujiendesha, udhaifu wa menejimenti na upungufu wa wafanyakazi katika maeneo ya uendeshaji.

“Ukaguzi umeonyesha kuwa menejimenti ya ATCL haina juhudi na mkakati mahsusi wa kulifufua shirika na hakuna mpango wowote. Bila kuwapo na mpango wa kulifufua shirika, juhudi zinazoendelea za kupata mkopo kwa ajili ya kununua ndege nyingine zinaweza zisiwe na manufaa,” alisema Profesa Assad.

Mradi wa Dart

Profesa Assad alisema katika mwaka wa fedha 2014/15 alibaini kwamba Dart iliingia mkataba ambao ulitaka Uda-RT kutoa huduma ya usafiri ya mpito kuendesha mabasi 76 kulingana na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.
Alisema ukaguzi ulibaini kuwa Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) lilinunua mabasi 140 ikiwa ni 56 zaidi ya yaliyoainishwa kwenye mkataba.

Pia, ukaguzi ulibaini kwamba mabasi hayo yalikuwa na nembo ya Uda-RT badala ya Dart kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba.
Aidha, alishauri Uda irudishwe chini ya usimamizi wa Serikali hadi mgogoro wa kimasilahi uliopo utakapomalizika.

MSD

Ripoti hiyo imebainisha kuwa bidhaa zenye thamani ya Sh2 bilioni zinaonekana zipo njiani kutoka MSD kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) tangu Mei, 2012. Kutoka bohari hiyo hadi Muhimbili ni umbali wa takribani kilomita tano.

Ripoti hiyo pia imeanika jinsi Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) ilivyoingiza nchini bidhaa zenye thamani ya Sh4.6 bilioni bila kuzifanyia ukaguzi na TPA kutotumia mita za kupimia mafuta, kutokuwa na mfumo wa kutambua makontena na meli 85 zilizotia nanga nchini kutoonekana katika mfumo wa mapato ya mamlaka hiyo.

Licha ya kukagua mashirika mengi, CAG alitoa ufafanuzi katika mashirika 13 ambayo ni Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Kiwanda cha Karatasi Mgololo, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Mamlaka ya Udhibiti wa Anga (TCAA), Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

TPA na Ticts

Akizungumzia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Profesa Assad alisema ukaguzi umebaini kuwa haina uwezo wa kufahamu na kusimamia taarifa za makontena yaliyopokewa na Ticts kwa kuwa mamlaka hiyo haina haki ya kuingia katika mfumo wa kompyuta wa Tancis ambao unatumiwa na TRA kuhifadhia taarifa hizo.

“TPA inategemea taarifa kutoka Ticts ambazo zinaweza zisiwe za kweli. Pia, imebainika kasoro kadhaa katika mkataba baina ya Ticts na TPA kwani umiliki wa asilimia 51 ya hisa za Ticts ulihamishiwa kwenye kampuni ya Hutchison International Port Holding kinyume na matakwa ya mkataba,” alisema na kuongeza:

“Ukaguzi umebaini kati ya meli 1,253 zilizotia nanga, 145 hazikuonekana katika mfumo wa mapato wa mamlaka hiyo. Menejimenti ilifanikiwa kupata nyaraka zinazohusu meli 60 tu kati ya 145 huku ikishindwa kutolea ufafanuzi wa kutoonekana kwa meli 85 zilizosalia.”

TTCL

Kuhusu TTCL alisema imekuwa ikipata hasara na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2014, ilikuwa imepata hasara ya Sh361 bilioni kutokana na mtandao wake wa mawasiliano ya simu za mkononi kutopatikana maeneo mengi.

TFDA

Alisema TFDA iliingiza nchini bidhaa zenye thamani ya Sh4.6 bilioni bila kuzifanyia ukaguzi, huku likitoa sababu kuwa jambo hilo lilitokana na upungufu wa wafanyakazi.

MSD

Ukaguzi uliofanyika katiba bohari hiyo mbali na kubaini kutokuwapo kwa maelezo ya Sh2bilioni, pia ulibaini kuwa bidhaa zenye thamani ya Sh18 bilioni zilikaa katika maghala ya bohari hiyo kwa muda mrefu na kuwa katika hatari ya kuharibika.

TIB na TPDC

Kuhusu TIB, Profesa Assad alisema benki hiyo ilibainika kutorejesha mkopo uliotolewa chini ya mpango wa kusafirisha bidhaa nje ya dhamana ya Serikali kiasi cha Sh2.5 bilioni jambo ambalo linadhoofisha utendaji wa benki hiyo.

Alisema ripoti hiyo pia ilibainisha kuwa kiasi cha takribani Sh965milioni hakikulipwa TPDC kama gawio kutoka kampuni ya Songas kutokana na kuhodhi asilimia 29 ya hisa katika kampuni ya Songas.

NDC

Alisema katika NDC, ripoti imebainisha malipo ya asilimia 90 ya fedha za mkataba bila kuwapo kwa dhamana na kutothibitishwa kwa dola za Marekani milioni 600 kama mtaji wa kampuni ya Sichuan Hongda Limited ambayo ilisaini mkataba wa ubia na NDC na Tanzania China International Mineral Hongda iliyoanzishwa ili kutekeleza mradi wa Liganga na Mchuchuma.

cHanzo:Mwananchi
 
Taasisi zote zitumbuliwe tu mana, hazina tija tena ama watu waondelewe tuanze upya
 
Ufisadi ulikuwepo ila hakuna na majipu.

Awamu hii inadili na majipu tu.

Majipu = watumishi wa
umma.

Ufisadi = wanasiasa.

Kwani wizara ya ujenzi iliyoku china ya Magufuli haikuwa na ufisadi wowote?
 
kinacho takiwa sasa ni kukubali kwamba kila wizara ina madudu na watuhumiwa wachukuliwe hatua kwakufuata sheria bora tuanze Upya kwa kukusanya vilivyo mikononi mwa viwavi na wafanyakazi wasifanye kazi kwa muda mrefu eneomoja mpaka wanapanga mipango ya wizi hii ni hatari mtumishi ukisha ingia serikalini lazima ukubari kutumikia mahala popote nchini
 
Back
Top Bottom