CAG aibua ufisadi TPA ya Deus Kakoko, Ni mbaya kuliko wa Kigwangalla

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
10,335
17,850
Kwa wiki zima mitandao ya jamii imemshupalia Dr Hamis Kigwangalla kwa ufisadi wa kutumia Tsh bilioni 2.58 bila idhini ya Bunge. Pengine Kigwangalla yuko kwenye "spotlight" kwa vile siku zote ni mtu wa majibizano kwenye mtandao ya jamii.

Sasa kuna manunuzi ya Tsh bilioni 22.69 yaliyifanywa na TPA ya Deus Kakoko. Katika DHAMBI au makosa makubwa ya manunuzi yanayo mhusisha mnunuzi moja kwa moja na RUSHWA ni kununua kwa SINGLE SOURCE.

Tumpunzishe Dr Kigwangala, tujikite na huyu Deus Kakoko anayejinasibu kuwa ni "home port" na JPM na huwa ana nguvu kuliko mawaziri wa wizara ya mawasiliano. Kumbuka alishindana na Waziri Mbarawa, na Mbarawa akang'oka.
20200409_064703.jpg
 
Ni kama waliambiana huu ndiyo mwaka wa mwisho huwezi jua kama utarudi mara baada ya uchaguzi kwa hiyo chukua chako mapema kwa hiyo lazima pawe na ukwapuaji kila mahali.

Wote waliobainika kuwa na shida kwenye hesabu zao jambo linaloonyesha matumizi mabaya ya fedha za umma hatua stahiki zichukuliwe.
 
Mwaka wa mwisho huu kila mmoja huangalia jinsi ya kupiga Kodi zetu.
Ukiona watu wanataka upinzani ufe huku mlinda Kodi zetu kama Assad akifurushwa uhitaji kujua jibu la nia.

Tofauti na awamu iliyopita tulinufaika wote na ufisadi awamu hii wanufaika wa chache na upiga haswaa.
 
kwa hiyo jamani huyu CAG si mlisema amewekwa kumlinda mkuu, inakuwaje amemgeuka na kuanza kuibua madudu,
? siwaelewi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwangalieni huyu! Sasa huyo Mkuu ndie Mkurugenzi wa Bandari?!

Jibu ni kwamba NDIYO, aliwekwa kumlinda Mkuu na mihamala yake inayopitishwa Ikulu bila hata kujadiliwa Bungeni!!

Jibu ni kwamba NDIYO, aliwekwa kumlinda Mkuu ili aendelee kuficha manunuzi mabovu kama yale ya ndege za ATCL ambazo CAG aliyepita alianza kunusanusa na kusema wazi kwamba ameshindwa kupata data!!

Jibu ni NDIYO, amewekwa kumlinda Mkuu ili tenda za kujuana kama zile za ujenzi wa Chato International Airport aliyopewa swahibu wake Mkuu watu wasifahamu mengi!!
 
zero brain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CAG anapofanya ukaguzi usidhani yale yote aliyoyaibua kwenye ukaguzi ni ya kweli. Unapokaguliwa kunatakiwa pia mrejesho/majibu kutoka kwa mkaguliwa na hivyo majibu yakiishatolewa yanaweza kumridhisha CAG. Kumhukumu Meneja Mkuu wa TPA bado ni mapema sana. Bwana Kakoko ni mfanyakazi bora na wa kuigwa.
 
Back
Top Bottom