CAG acha kuupotosha umma wa Watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CAG acha kuupotosha umma wa Watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MBANINO, Dec 6, 2011.

 1. M

  MBANINO Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwa masikitiko makubwa kile kilichoandikwa katika gazeti la habari leo la jana tarehe 5/12/2011 likimnukuu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali akiwalaumu watendaji mbalimbali wanaohusika katika usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa kushindwa kusimamia miradi hiyo na hivyo kupelekea ongezeko kubwa la 'Special Audits' hapa nchini. Alidokeza pia kaguzi hizi zimesababisha ofisi kushindwa kutekeleza wajibu wake kikamilifu.

  Katika gezeti la leo (6/12/2011) la Habari leo Waziri wa Fedha alionyesha kushangazwa kwake na mzigo huo unaosemwa na CAG.

  My take:
  Kwa ujumla CAG anaupotosha umma kwa sababu ukiangalia sheria ya ukaguzi wa umma, Public Audit Act, inampa mamlaka yote ya yeye kuamua nini cha kukagua na kwa wakati gani. Sheria hiyo imeainisha wazi kabisa ya kwamba hakuna chombo au mamlaka yoyote itakayomuamuru nini cha kuchagua. Vyombo au mamlaka nyingine vitamuomba kukagua na kama ataridhia basi kazi hiyo itafanyika.

  Cha kusikitisha huyu mheshimiwa CAG anaupotosha umma na kuonyesha ya kwamba alikuwa anashurutishwa kufanya kaguzi hizo za special. Hili si la kweli nadhani mwenye udhaifu ni yeye pale anaposhindwa kusimamia sheria inayompa mamlaka ya kuamua ni nini akague na nini asikague.

  Pili, ni ukweli uliowazi ya kwamba 'quality' ya kaguzi zinazofanywa na ofisi ya CAG na yenyewe inachangia sana kuwepo na kaguzi hizi za special. Inasikitisha pale unapoona mradi wa maendeleo ambao ni wazi kabisa umetekelezwa kwa uzembe na udhaifu mkubwa lakini ofisi hii inatoa hati safi kwa wahusika. Wananchi wanapotoa malalamiko yao ndipo hapo uamuzi wa kaguzi maalumu unapochukuliwa. Hivyo ofisi hii inaposhindwa kutekeleza wajibu wake inachangia hili.

  Na katika maelezo ya CAG hajalisema hili hata kidogo. Hapo ndipo napooona upotoshaji. Yeye kafanya nini kuboresha utendaji wa ofisi yake katika kaguzi za miradi ya maendeleo? Je, ni kwa nini alikubali kukagua kila aina ya ukaguzi anao-amriwa na serikali na vombo vingine? Je, alikuwa anafanya wajibu wake professionally? Je, katika hizo kaguzi za special alizofanya ameweza kuwaainisha watendaji wanaokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hatua gani zimechukuliwa dhidi ya maofisa hao?

  Ni muhimu aache siasa na kutumia vyombo vya habari kupaka watu watope huku naye akiwa na madhaifu mengi tu.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tangu alipomwogesha JAIRO,
  SINA MZUKA NA UTTOH,
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  CAG yupi huyo.Si ndie yule yule anakula rushwa kwa mashirika ya Umma ili wapte clean reports kumbe yameoza moja kwa moja? Hana Issue.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Naenda kusoma sheria na professional standards za audit ikiwemo INTOSAI, narudi punde.
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  utohsi.
   
 6. Ikwanja

  Ikwanja JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  ameshalewa pesa ya mafisadi huyo mzee.

  Hana jipya aachie ngazi.
   
 7. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 842
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  Kuanzishwe mahakama ya kimataifa ya kushughulika na waraji(wezi na wala rushwa) wa fedha za umma kama ilivyo icc,maana sisi tumeshindwa
   
 8. MJIMPYA

  MJIMPYA JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kila mtu mjuaji sasa, mambo aliyosema CAG ni professional na ndivo ilivo. Kama ungekuwa na taaluma hiyo ungeweza kuelewa anachosema. Tatizo kila kitu tumefanya siasa kama wanasiasa wetu wanavofanya.
  Kupondo ndo fashion ya jf.
  Hakuna anayeweza kujua kila kitu, ungeandika msg yako ukiomba ufafanuzi tungekusaidia maana yake nini badala ya kujifanya unajua mambo usiyoyajua.
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  inaonyesha wewe ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa k.ikwete bado ana lengo zuri na nchi hii
  iili hali ukijua kuwa jamaa anatamani nchi awauzie waarabu kabisa
   
 10. p

  politiki JF-Expert Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kaka huitaji degree kuona wizi unaofanyika nchi hii zaidi ni swala la common sense CAG kapitisha shs. milioni 6 kwa ajili ya mafuta usafiri wa maofisa wanne chini ya jairo. huitaji degree ya account au finance kuliona hilo ni common sense tu. hakuna kuomba ufafanuzi kitu kiko wazi na CAG mwenyewe tayari ameshapoteza intergrity na kama angekuwa mtu mwenye integrity angekuwa ameshajiuzuru kwani hakuna kitu atakachokitoa watu wakkakiamini tena mara baada ya kupindisha ukweli uliokuwa wazi kwy issue ya jairo. sometimes degree zinatumika kufichia maovu nchi hii yai viza unaambiwa inabidi likapimwe na wataalam ili tujue kama kweli ni visa. wake up mtanzania.
   
 11. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Huyu bwana na Luhanjo mimi sina imani nao kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

  Hawa jamaa ndio wanaotuumiza ktk hii nchi,hawana huruma na kodi zetu
  Yaani ningekuwa ndio niliyempa ajira kwa kosa la kumsafisha Jairo ningekuwa nimesha mtema kitambo tuu

  Angekuwa China balaaaaaaaaaaaaaaaa,zamaaaaaaaaaaani wangekuwa wamechukuwa kichwa chao,amshukuru mungu kuzaliwa Tz ya wapore
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu umenena vyema haswa. CAG kazi yake ni external auditor wa wizara na idara za serikali. Mpango kazi wake ni kutoa opinion kwenye hesabu za serikali na jukumu la kuzuia ama kugundua wizi ni la viongozi wa Idara za serikali. Hawa huwa wana watu wanaitwa Internal Auditors ili kuwasaidia kujua kama idara zinaendeshwa vizuri na internal controls ziko in place. Unapompa CAG kazi za special audit (hasa zinapokuwa nyingi) unampotezea muda wa kufanya shughuli zake.

  Hivi Internal Auditors wa Idara za Serikali wapo wapi?
   
 13. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Unajua nyie watanzania mnatakiwa mtambue kitu hiki, CAG hutoa report, nyingi hafanyi yeye anasub contract to audit firms kama pwc, delloite na EandY, nimeziona nyingi na zinaeleza uozo mwingi tu kwenye miradi nk. Sasa tatizo liko wapi,lipo kwenye serikali ambayo inatakiwa kuchukua hatua staiki. Serikali imelala haichukui any action. Inamaana hata CAG akitoa riport milion na serikali ama buinge haifanyi any serious action on them haina maana. Mtalaum CAG lakini najua anafanya vizuri sana tena sana tu.
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu ungerudia kuisoma ripoti ya Kamati Teule ya Bunge ungeelewa vizuri mambo haya. CAG alipewa terms of reference na pale kulikuwa na limitation of scope. Ni vizuri tukajua tofauti kati ya special audit na audit ya kawaida. Special Audit unapewa terms of reference na unaangukia humo kwenye terms of reference. Hata mimi mwanzoni nilidhani CAG kashambulia vichaka ila baada ya kuona terms of reference nikashangaa!
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Mjomba inakuwaje tume ya bunge kumlaumu CAG kwa kuupotosha umma ina maana wale wabunge hawakujua terms of reference alizopewa CAG na Bunge ??
   
 16. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  wawezesheni Internal Auditor, ajira yao isiwe chini ya makatibu wakuu, raisi wala ceo's wa mashirika na mawizara. Iwe taasisi huru,wawe na mfumo wao tofauti wa kureport, wapewe fedha za kutosha na vitendea kazi, hapo mtafanyikiwa kudhibiti.

   
 17. hoffman

  hoffman Senior Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 131
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Kwa hali hii c wanyonge 2tatetewa na nan kama hata maandamano hawatak?
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280

  Nakumbuka walisema KMK asingetumia ile press briefing ya CAG angetumia report aliyokuwa nayo mkononi.
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo kuna maneno. Internal Auditors hawajawezeshwa na reporting structure yao imekaa vibaya. Nadhani ujio wa Internal Auditor General labda utasaidia.

  Nchi hii tunatakiwa tuangalie miundo na mifumo. Kama miundo na mifumo haijakaa sawa basi kila siku kazi ya CAG itakuwa kufanya special audit kwa kuwa kila mahala ni wizi mtupu!
   
 20. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kimbunga uko sahihi. Watu hawaelewi hivi vitu ukisha kuwa na TOR huwezi kwenda zaidi. Halafu CAG ni tofauti na Takukuru. Ukiweza tofautisha hv vitu utajua limitations zao!
   
Loading...