CAG aahidi kutoa mlungula kwa watakaompamba kwenye vyombo vya habari

Mkeshaji

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
4,262
1,416
Salaam wanajamvi,
Najua leo jamvi liko bize sana na ishu za utajiri wa mtoto wa mfalme.
Pamoja na hayo ningependa pia kuwakumbusha habari hii ambayo pia ni muhimu katika mustakhabari wa taifa letu.

Jana CAG alikutana na wahariri na waandishi wa vyombo vya habari jijini Dar. Pamoja naye aliambatana na Mkurugenzi wa Shrika la Umeme nchini (Tanesco) Bw. William Mhando.
Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni "kupangua kashfa za ufisadi" zilizoikumba Tanesco hivi karibuni ambazo inasemekana zilifichuliwa na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh.

Kilichonishangaza zaidi katika mkutano huo ni pale CAG alipowaahidi waandishi wa habari kuwa kuanzia mwakani ataanzisha shindano ambapo mwandishi atakayeandika ripoti ya CAG kwa namna anavyotaka yeye (CAG), yaani kuipamba na kuisifia basi mwandishi huyo atazawadiwa kitita cha mamilioni ya pesa pamoja na cheti, ingawa kiwango kamili amedai kitatajwa wakati wa uzinduzi wa shindano hilo.

Binafsi nilitatizika sana na kauli ya CAG kutaka kurubuni waandishi wetu ambao kiukweli hawana kipato kikubwa hivyo unapotangaza donge nono namna hiyo hakuna atakaye-challenge na mwisho wa siku waandishi wote watajikuta wanafanya vile ambavyo CAG anataka na hivyo kujikuta wameingia mtegoni.
Huu ni ukiukwaji wa haki za uandishi na waandishi na pia ni uingiliaji wa uhuru wa vyombo vya habari.

Natoa wito kwa waandishi wote kufanya kazi zao bila kushurutishwa na mtu ama watu, bila kujali uwezo wao wa kipesa ama cheo chao ama nafasi yao katika jamii; kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamekiuka misingi ya kazi zao, watakuwa wameuza utu wao vilevile watakuwa hawajatutendea haki watanzania.

Ama kweli "Penye udhia penyeza rupia"

"Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanganyika"

utouh.JPG
 
mkeshaji umetoka kukesha lazima utakuwa umechoka ni vema ukalale upumzike
 
mkeshaji umetoka kukesha lazima utakuwa umechoka ni vema ukalale upumzike

Kwa nini mkuu..? Mbona wewe umelewa heineken watu hawasemi kitu..!
Back to topic:embarassed2:
 
Hakuna mwandishi wa habari hata mmoja mwenye taaluma ya UHASIBU. Ni kweli anataka wampambe tu. Atawashindanisha kwa lipi?
 
kweli Tanzania imejaa wajinga. Juzi nilimsifia huyu CAG hapa, leo kaja na hili? Ivi kweli tumelaaniwa au ni nini?
Mbona wapumbavu wengi?
 
TANESCO pamoja na wizi, madeni hewa na vurugu zote zilizomo mle CAG anasema amewapa hati safi kwa miaka mitatu mfululizo!!
 
TANESCO pamoja na wizi, madeni hewa na vurugu zote zilizomo mle CAG anasema amewapa hati safi kwa miaka mitatu mfululizo!!

Kwa kweli mkuu hii nchi tumeliwa. Kila kukicha watu wanatafuta namna ya kukingiana kifua. Ili kuthibitisha kuwa hakuna mtumishi wa umma atakayemnyooshea kidole mwenziye, CAG alimbeba mkurugenz wa tanesco ili kupangua kashfa hizo. Hawa wote ni mafisadi tu.
 
Back
Top Bottom