CAF yakumbushia comeback kubwa kuwahi kutokea ya Simba SC, Ligi ya Mabingwa Afrika

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), leo April 6, 2020 kupitia ukurasa wake wa Instagram @Caf_Online, limepost kumbukumbu ya Comeback kubwa zaidi kuwahi kutokea katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Maajabu hayo ya kipekee ya 'Comeback' kubwa zaidi kuwahi kutokea ya kupindua matokeo kwa idadi ya mabao mengi katika historia ya ligi hiyo, yalifanywa na Mabingwa wa Nchi, Mnyama Simba Sports Club, Wekundu wa Msimbazi.

Simba SC, walianza kwa kupoteza mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 4-0 nyumbani dhidi ya Mufulira Wanderers FC ya Zambia kabla ya kwenda kushinda mabao 5-0 ugenini katika mechi ya mkondo wa pili wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mnamo mwaka 1979.

Kuna anayeweza kwa sasa hii?

FB_IMG_1586202114606.jpeg
 
Wanatamani sana wangekuwa wao, lakini hawana namna..Ndo maana tunawaambia Simba ni Taifa Kubwa, NguvuMoja
Siku zote Yanga wanatamani kumchinja Mnyama tu. Zingine ni porojo tu. Amini nakuambia. Kama unataka reference jikumbushe na mambo yaliyotokea tarehe 08 Machi, 2020.
 
Vyura fc watapinga
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), leo April 6, 2020 kupitia ukurasa wake wa Instagram @Caf_Online, limepost kumbukumbu ya Comeback kubwa zaidi kuwahi kutokea katika Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Maajabu hayo ya kipekee ya Comeback kubwa zaidi, yalifanya na Mabingwa wa Nchi, Mnyama Simba Sports Club, Wekundu wa Msimbazi.

Simba SC, walianza kwa kupoteza mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 4-0 nyumbani dhidi ya Mufulira Wanderers FC ya Zambia kabla ya kwenda kushinda mabao 5-0 ugenini katika mechi ya mkondo wa pili wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika mnamo mwaka 1979.View attachment 1410963

Jr
 
Back
Top Bottom