Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Baada ya kutolewa na Al Ahly kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika timu ya Yanga sasa kupambana na Esperanca ya Angola.
Utaratibu wa CAF ulikuwa kama ifuatavyo;
Timu nane (8)zilizofuzu kutoka michuano ya shirikisho ambazo ni Esperance (Tunisia), Stade Gabesien (Tunisia), FUS Rabat (Morocco), Misr Makkassa (Egypt), Esperanca (Angola), CF Mounana (Gabon), Kawkab (Morocco) and Medeama (Ghana).
Na timu nane (8)zilizofuzu kutoka ligi ya mabingwa ambazo ni TP Mazembe (DR Congo), Etoile du Sahel (Tunisia), El Merreikh (Sudan), Stade Malien (Mali), MO Bejaia (Algeria), Ahli Tripoli (Libya), Mamelodi Sundowns (South Africa) and Young Africans (Tanzania)
Mechi hizo kuchezwa 6-8 Mei 2016 kwa mechi za mzunguko wa kwanza na tarehe 17-18 Mei 2016.
Kila la kheri Yanga.