CAF Team of the Week: Simba Sc waingiza watano

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,169
103,628
20210523_151210198975.jpg

Yumo Bocco, Chama, Miqsone, Kapombe na Tshabalala. Simba ni timu kubwa sana Afrika hii
 
Sijui mikakati ya Timu ya Taifa ikoje, hawa vijana wangatufikisha mbal
Sio vibaya TFF wakaenda kujifunza kwa Simba namna nzuri ya kuhamisha morali ya Simba kuipeleka kwenye timu ya Taifa. Ukiangalia timu ya taifa ikicheza huioni ile hamasa ya wachezaji kutafuta kiu ya matokeo kama ambavyo Simba wanafanya kwenye mechi zao. Na "case study" iwe ni zile mechi Simba alizowakalisha vigogo wa Afrika Al Haly, As Vita n.k. Hamasa ianzie hapo iwapo Simba kampiga Al haly hapa kwa Mkapa basi na timu ya taifa ya Misri haitoki salama kwa Mkapa. Kwa Mkapa iwe machinjio ya timu zote za nje zinazokuja kucheza hapa nchini na timu yoyote ile ya Tanzania.
 
Simba imetoka, mashindano yamekosa mvuto

Best team of the week zitazowekwa kwanzia sasa, zitawekwa kwasababu timu tu ilishiriki na sio uwezo

Just imagine kwenye list kaizer chief kaingia kipa tu unategemea nini mbeleni?
 
Ni kweli hamasa zinatia sana confidence na kujituma.

Naona tatizo lingine na TFF ni kuwa wao hawako kibiashara kama Simba ndio maana hata wakipata matokeo mabaya hawaoni tatizo.

TFF wakitekeleza majukumu yao kama kibiashara mbona mbinu zitatafutwa na timu itajengwa na hatimaye kuimarika
 
Simba imetoka, mashindano yamekosa mvuto

Best team of the week zitazowekwa kwanzia sasa, zitawekwa kwasababu timu tu ilishiriki na sio uwezo

Just imagine kwenye list kaizer chief kaingia kipa tu unategemea nini mbeleni?
Umeumia eeeeeee?
 
Mbona kama kuna nembo mbili za Yanga hapo zimefata nini kudadazeki zake?
Kwenye M.Affonso na M.Lebusa.
 
CAF wanatarajia kuiomba timu ya Simba SC ya Tanzania kutembelea makao makuu yao pale Cairo Misri, wakawaeleze haya mafanikio makubwa hivi kwa muda mfupi wametumia akili gani kiyafikia, ili iwe funzo kwa timu nyingine za wapiga kelele Afrika kama utopolo FC inayopatikana Tz mitaa ya twiga na jangwani, utopolo FC wanasisitizwa kutuma wawakilishi wao wakapewe darsa.
 
Chama amepewa points nyingi kuliko wote 9.9

Halafu huyo kipa wa Kaiza katunguliwa goli 3 inakuwaje awe bora. Au wameangalia n sevu alizo ziokoa?.
Hongereni Simba na mashabiki wote wa kibongo maana tulikuwa tunakinukisha hadi kwenye mitandao ya nje hadi wametumiss.

Mashabiki wa Kaizer nao nimeona wamekubali mziki wa Simba.
 
Timu ya Simba ifanyie Kazi ya kuongeza kipa 1,mabeki 2,,washambuliaji 2, na kiungo 1.

Mabeki wa pembeni wasajiliwe wazuri wawe wanapanda kama akina Miskoni na Morisoni.

Washambuliaji wawe wakali kwa ajili ya ku score tuu.

Na pia kocha afanyie Kazi utengenezaji wa space wakiwa na mpira badala ya kuchezea mpira nyuma ya wapinzani hata kama Wana mpira.

Mwisho ,Simba iwe na mind set kwamba wao ni timu kubwa kwa hiyo waache mind set ya kutegemea uwanja wa nyumbani tuu,wakiwa ugenini wacheze defensive game but wajitahidi kupata japo goli moja au basi sare ama wasiruhusu kufungwa magoli mengi.

Timu ikifungwa wafunguke kutafuta goli Ili kupunguza mzigo mechi ya nyumbani.
 
Asante sana.
Wewe ni mdau wa mpira wa miguu.

Umeshauri vizuri sana
 
Chama amepewa points nyingi kuliko wote 9.9

Halafu huyo kipa wa Kaiza katunguliwa goli 3 inakuwaje awe bora. Au wameangalia n sevu alizo ziokoa?.
Hongereni Simba na mashabiki wote wa kibongo maana tulikuwa tunakinukisha hadi kwenye mitandao ya nje hadi wametumiss.

Mashabiki wa Kaizer nao nimeona wamekubali mziki wa Simba.
Wale Kaizer nimewaona wanapanda ndege huku wanatetemeka, bado hawaamini kama wamefuzu mbele ya Simba SC baba lao Afrika masharaki, kati na kusini mwa bara la Afrika.
 
Back
Top Bottom