CAF Confederation: Kikosi cha Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wake Pyramids, yafungwa 3 kwa 0

Turnkey

JF-Expert Member
Jul 9, 2013
7,359
5,831
C0E9D4FA-BEC8-487D-A89B-688EC14D8562.png

Leo kuna mtanange wa kukata na shoka kwenye viunga vya Cairo..na hiki ndio kikosi cha Yanga kitakachoanza

======

Waarabu wa Misri Waibana Mbavu Yanga


Kikosi cha Yanga jana kimeshindwa kufurukuta mbele ya wapinzani wake Pyramids kwenye mchezo wa marudio wa Kombe la Shirikisho uliochezwa nchini Misri.

Yanga SC waliingia katika uwanja wa 30 June kurudiana na Pyramids wakiwa nyuma kwa magoli 2-1, magoli ambayo yalifungwa katika mchezo wa kwanza jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, hivyo walitakiwa kuifunga Pyramids FC mabao 2-0 ili kupenya mbele hatua ya makundi

Kufunga magoli mawili bila kuruhusu kufungwa haikuwa kitu rahisi kwa Yanga, hivyo walijikuta wakimaliza mchezo huo kwa kupoteza kwa kufungwa kwa magoli 3-0 .

Magoli ya Pyramids FC yalifungwa na Traory dakika ya 27, Farouk 79 na El Said dakika za nyongeza.

Matokeo hayo yanaitoa Yanga kwenye michuano ya kimataifa ambapo Pyramids inafuzu hatua ya makundi kwa juma ya mabao 5-1.

Kwa maana hiyo Tanzania sasa msimu wa 2019/20 haina mwakilishi yoyote wa kimataifa katika michuano hiyo.
 
Yanga Bariidii Haina Mvuto
Leo Mkajitahidi Nafasi Mmeipata
Tunawaombea Ingawa Kipigo Chake Ni Cha Mbwa Ko Ko
 
Ila Ali Ali huwa anatupandisha presha mashabiki wa Yanga! Yaani hata huelewi siku hiyo ataamkaje. Kimo kinamtesa! Yaani viongozi wa Yanga walishindwa kabisa kumuona Bakary "Nondo" Mwamnyeto wa Coastal Union kweli!
 
Wana Yanga leo tujiandae hapa ni mwendo wa hamsa hamsa,tukijitahidi tunapigwa tatu bila.

Tujiandae tu kiasikolojia,cha msingi kabla ya mechi hakikisha umeoga na umekula baada ya mechi wewe ni moja kwa moja kulala.
 
Naomba link ya online, au Dstv wanarusha ? Maana azam sina!
 
Back
Top Bottom