PROSPER 05
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 226
- 217
Draw iliyofanyika Misri Leo inaonyesha Kuwa AZAM FC wana Lambalamba ni moja kati ya timu 12 Zitakazoanzia Round ya Kwanza ya Michuano ya CAF Confedaration Cup 2017. Timu zingine 40 zitaanzia na stage ya Mtoano (preliminary stage)
Azam itacheza Mechi ya Kwanza Tarehe 10–12 March 2017 na mshindi wa Mechi ya awali namba 12 kati ya Orapa United(Botswana) VS Mbabane Swallows(Swaziland)
CAF kuelekea michuano ya mwakani imebadilisha mfumo wa mashindano hayo, ambapo imepanua wigo kwa timu zitakazoingia hatua ya makundi kutoka nane hadi 16, kila michuano itahusisha makundi manne yenye timu nne kila moja.
Mfumo huo unamaanisha kuwa timu 32 zitakazocheza raundi ya kwanza inayofuata baada ya ile ya awali kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, zile 16 bora zitakazoshinda zitaingia moja kwa moja katika hatua ya mwisho ya mtoano (play off).
Katika hatua hiyo zitakutanishwa na timu nyingine 16 zilizotolewa katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na wale 16 bora watakaopenya hapo watafuzu moja kwa moja kwenye hatua ya makundi, itakayoanza kuchezwa Mei mwakani.