Cabinet mpya: JK kakosea wizara 5 nyeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cabinet mpya: JK kakosea wizara 5 nyeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Nov 24, 2010.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kikwete amejitahidi kiasi kuepukana na mawaziri ambao wana tuhuma/kashfa za ufisadi kwenye cabinet yake mpya. Lakini nimegundua kuwa wanasiasa vilaza wenye uwezo mdogo wa akili, ubunifu na kuchapa kazi ndiyo wamepewa kuongoza wizara nyeti.

  Kwa maoni yangu, kwa kutumia mawaziri walewale wa Cabinet, Kikwete angekuwa na baraza la mawaziri lenye ufanisi mkubwa kama angefanya uteuzi huu:


  1. Waziri wa Fedha, Prof. Anna Tibaijuka

  Huyu ana uzoefu wa UN, UNCTAD, ana PhD ya agro-economics na alikuwa economics professor UDSM. Anakubalika sana kimataifa. Donors hawana imani na uwezo wa Mustafa Mkulo. Angesaidia kurudisha imani ya donors kwa Tanzania ambao walipunguza misaada kwenye bajeti iliyopita kwa kama $250m.

  2. Waziri wa Maliasili na Utalii, John Magufuli

  Utalii inaongoza kwa kuingiza pato serikalini lakini bado Tanzania imelala sana. Afrika Kusini inapata watalii milioni 8 kwa mwaka sisi bado hata hatujafikisha 1 million. Pia angekomesha biashara haramu ya vitalu, magogo na meno ya tembo.

  3. Waziri wa Nishati na Madini, Harisson Mwakyembe

  Huyu ni mchapa kazi mahiri. Anaijua sheria vizuri na angesimamia mikataba mibovu ya madini ibadilishwe. Makampuni makubwa ya madini yanamdharau waziri wa sasa William Ngeleja kuwa hajui kinacho endelea. Ngeleja aliwahi kupongeza De Beers kuuza mgodi wa Mwadui Williamson diamonds kwa Petra kimakosa badala ya kuuza hisa hizo kwa serikali ya Tanzania.

  4. Waziri wa Kilimo, Samuel Sitta

  Angesaidia kuleta msukumo mpya kwenye sekta ya kilimo ambayo bado inalegalega sana. Angeboresha kilimo kwa standards and speed. Kilimo cha kisasa kingefana. Tanzania ingekuwa nchi ya milk and honey.

  5. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Mark Mwandosya


  Ni mfuatiliaji mzuri. Angesaidia kuboresha utendaji kazi wa halmashauri zote nchini. George Mkuchika, ambaye ni swahiba mkubwa wa Kikwete alishindwa kuongoza wizara ndogo kama ya habari. Kumpa Mkuchika wizara hii nyeti ni jambo la ajabu sana na la kutotegemewa.
   
 2. jyfranca

  jyfranca JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sina la kupinga hapo, kijana kazi nzuri. Huyu Kikwete anatakiwa akutafute umshauri. Hao washauri wake akili hakuna, wanakula pesa za bure
   
 3. A

  Agao Kichore Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 26, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Adui mwombee njaa. Kwani unataka utawaliwe na ccm kwa karne ngapi? Tumezoea shida zetu na furaha, vifijo na nderema za makabwela vitasikika siku ccm itakapo kuwa chama cha upinzani. Tatizo watanzania tunatendence ya kubadilika badilika. Mlitaka mwanze kumwaga sifa wakati juzi tu mlidai kachakachua matokeo maana mlishapoteza imani na kura zenu ndo zilizochakachuliwa sasa mazuri kwake utayatoa wapi.
   
 4. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HONGERA KIKWETE KWA KTEUA SURA AMBAZO NI NADRA KWA LAWAMA(wasio na lawama) NA UCHAFU (iwe wa kusingiziwa ama dhahiri)
   
 5. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  hongera JK, Baraza lako la Vipofu tumelipata, sisi mambumbumbu tuko nyuma yako mutukandamize!
   
 6. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Umejaribu kufikiria bro, ila sijaona mpangilio wako kama ungeleta ufanisi wa ajabu zaidi ya ule wa jeikei. Kazi nzuri lakini.
   
 7. D

  DocGoddy Member

  #7
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I didn't espect anything new kutoka kwa Jk!!so am nt suprised na baraza lake,mambumbu wengi ndio wameunda serikali!
   
 8. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  hizi red hususan namba 5, yaelekea huwajui vizuri records zao za utendeaji. TAMISEMI anafaa sana mtu kama wasira
   
 9. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kama kuna watu sikutaka kuwaona ni wanne kwanza ni yeye mwenyewe kama rais (ila hili nimelivumilia) wizarani sikupenda kuwaona Ngeleja yule msela, Mkulo yule mkulaji na Kawa Mbwa alojenga matundu manne ya choo kwa mil mia saba!
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Haya unda hilo Baraza lako unalolipenda!
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  am fed up
   
 12. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  kaka mtizamo mzuri!
   
 13. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Inawezekana Ridhi1 ndio alikuwa mshauri mkubwa na Mama Salma katika uteuzi wa Mawaziri kwani kikwete ni wakushikiwa, Tanzania haina rais makini tangu 2005 nchi inayumba na kikwete ubishi wa kutawala kumbe analiangamiza taifa letu. Mungu Tuepushe na ufisadi mpaka 2015 tuvuke salama katika kipindi hichi cha ufisadi:embarrassed:
   
 14. M

  Mwera JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  fareed nakupa heko,kwahakika wewe ni mchambuzi makinisana,umenifurahisha sana jinsi ulivozipanga wizara na mawazir wake umenena kwelitupu,elf mabrouk, ila jk ndo kashatangaza hakuna namna,tuombe serkali mpya ifanyekazi kwauadilifu naumakinimkubwa huenda tz ikawa nchi ya maziwa na asali,ngoja tuone.
   
 15. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280

  Hahaahah mimi SIMO.
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Duh, hata Sophia Simba?? Kwa uteuzi mwingine wote sina kipingamizi nao, lakini Sophia Simba, not at all. Simuungi mkono hata kidogo. Kwa ujumla baraza ni zuri. Hata hivyo mapendekezo ya Fareed yapo makini, though nafikiri Magufuli amepelekwa mahali sahihi. Tuna miradi mingi sana ya barabara kipindi hiki, lazima waziri wa ujenzi awe ni mtu makini na mchapa kazi. Kumbukeni kuna kujenga fly over Dar es salaam, kuna kuanzisha ule mradi wa Dart etc.
   
 17. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Un habitat unajua maana yake huyu mama anafaa makazi ila ngoja tuone. ngeleja madini hawezi tunazidi kuibiwa
   
 18. Simba Mangu

  Simba Mangu JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  mwanetu polisi pole kwani wasira angewezaje wizara ya tamisemi? au kwa kuwa aliweza mpiga muhidin ndolanga? na akapata utaison.
   
 19. B

  Bull JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkulo anafaa abaki pale pale kwenye fedha kwa sababu zifuatazo;

  1-Kwa mara ya kwanza chini ya utawala wa Mkulo, bajeti tegemezi imeshuka toka 48% mpaka 28%

  2-Ukusanyaki wa kodi umepanda toka 240billion mpaka kufikia 1025billion 2010

  3- Uchumi wetu unaendelea kupata sasa umefikia 7.8%

  4- TZ inakuwa kiuchumi kuliko nchi yoyote ya East afric na kushind nchi nyingi africa

  4- credit facilities/mikopo inapatikana kila sehemu

  5- Bank ya wanawake na kuwawezesha kimaendeleo

  6- Inflation imeshuka sasa ni 4.5% toka 15%

  7- Thamani ya shillingi haijaporomoka kwa muda mrefu

  8- Bail out plane, tz imehimili mtikisiko wa uchumi duniani chini ya JK na Mkulo kama waziri wa fedha

  9- Bajeti ya kila wizara ameongeza hasa wizara zilizo kuwa zimesahaliwa na mawaziri waliopita

  10 Bajeti ya elimu, afya na kilimo imeongezwa maradufu

  11- nk

  Wakuu tuwe fair tunapo wajaji watu tusiwe always negative toward other, naamini Mkulo kajatahidi, chini ya uongozi wake tanzania itafika mbali, kama wanauchumi walivyo tabiri na kusema' TZ kama itaendelea na speed hii ya uchumi kati ya 7 to 10% itakuwemo kati ye emerging market countries' Nawakilis
  ha
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani tunazidi tu kuchanganya madude. Mwingine naye anaweza kuja na muono wake pia. Ukweli JK amewaprove watu kwamba yeye si mtu wa visasi kama walivyokuwa wanalazimisha. Na speculations nyingi zimekuwa wrong. Mwaka 2005, watu walipatia lakini this time ameweza.
  Sasa kwenye hilo pendekezo la ndg Fareed hao woote wapo ndani ya cabinet kwahiyo hamna kilichoharibika wataedelea kushauriana humo.
   
Loading...