Cabinet Meeting......a month later and Karume Missing??

Hivi mbona mnakuwa kama walevi?

mnajadili KATIBA ya ZANZIBAR wakati hakuna aliyeuona mkataba wa MUUNGANO sasa kama kweli mko serious leteni mktaba wa MUUNGANO kisha tuta move on kwenye ajenda hizi zinginezo


maana kuna tatizo la legality ya muungano wenyewe

Point mzee. this one is good.
 
sasa GT hapa umenichanganya mimi na chimpumu changu hapa... kama hakuna mtu aliyeuona Mkataba wa Muungano ambao na wewe hauna (vinginevyo usingeomba watu waulete), umejuaje kuna tatizo katika Muungano? Halafu, kwanini uwatake watu wengine waulete, kwanini wewe usijitahidi kuuleta?

6ydo18p.gif
 
Kuna uwezekano mkubwa kuwa hiki kikao kilikuwa cha dharura kwa ajili tu ya kufahamishana kuhusu kupeleka majeshi Comoro otherwise labda kisingekuwapo(angalia article hapo chini).

Kama ni hivyo ina maana hakuna vikao vya mara kwa mara kupanga/kujadili/kufuatilia mikakati ya maendeleo inavyotekelezwa nk. Hii inatia wasiwasi uwezo na ubora wa uongozi wa Mh. JK. Hivi anaendeshaje nchi bila kukutana na timu yake? Hivi anaelewaje yanayoendelea kwenye wizara zake au kila waziri anafanya anavyoona yeye mwenyewe inafaa? Kazi kubwa tunayo, sura nzuri imetuponza.



JWTZ kuongoza ukombozi Comoro

2008-03-15 09:02:14
Na Sammy Polly



Umoja wa Afrika (AU) umeiteua Tanzania kuwa kamanda wa jeshi la AU litakalohusika na operesheni maalumu kukikomboa kisiwa cha Anjouan ambacho kwa sasa kinakaliwa kimabavu na kiongozi aliyejitangazia madaraka mwenyewe,
Kanali Mohamed Bacar.

Akizungumza katika mkutano na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema tayari sehemu ya askari wa Tanzania watakaojiunga na kikosi hicho waliondoka nchini Jumanne wiki hii kwa ajili ya operesheni ambayo inaweza kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

Alisema kwamba wizara yake ilishindwa kutoa taarifa rasmi kwa umma kuhusiana na kushiriki kwa Tanzania katika jukumu hilo kwa kuwa kiutaratibu ilihitaji kwanza Rais Jakaya Kikwete aliarifu Baraza la Mawaziri na uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya kuvitaarifu vyombo vya habari.

Waziri Membe alisema kwamba jeshi hilo limepangwa kuwa na jumla ya askari 1,800, ambapo Tanzania inatarajia kupeleka askari 750, Senegal na Sudan (750) na Comoro yenyewe 300.

Alisema tayari Tanzania ina askari 200 waliopo Comoro kwa ajili ya kulinda amani.

Alisema kwamba jeshi hilo limepewa majukumu makuu matatu ambayo ni kumtia mbaroni Kanali Bacar ili ashtakiwe, kuhakikisha kuwa wanamgambo wanaomuunga mkono Bacar wanaporwa silaha na kulinda amani kisiwani Anjouan hadi kutakapofanyika uchaguzi halali utakaoitishwa na AU.

``Majeshi yetu hayatarudi nyuma hata kidogo kwa kuwa tumedhamiria na operesheni hii imeandaliwa kisayansi ili pasitokee madhara kwa wananchi,`` alisema.

Alieleza kwamba askari hao wamepangwa kuwepo Anjouan hadi Mwezi Mei mwaka huu ambapo hali inatarajiwa kurejea katika hali ya utulivu.

``Siku 9 zilizopita Bacar aliombwa ili ajisalimishe mwenyewe lakini aligoma tena kwa kiburi kikubwa, na ndiyo maana sasa tumeamua kutumia nguvu za kijeshi,`` alieleza Waziri Membe.

Alisema kabla ya kufikia maamuzi ya kutumia nguvu za kijeshi, AU ilitumia vikao 12 kama njia ya kidiplomasia na baadaye kukiwekea vikwazo kisiwa hicho lakini njia zote hazikufanikiwa.

Alieleza kwamba serikali inaandaa utaratibu ambao utawawezesha waandishi wa habari kutoka Tanzania kuungana na jeshi hilo la AU huko Anjoun ili kuwapasha wananchi matukio yote.

Katika mkutano huo huo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alisema serikali imehakikisha usalama na maslahi ya askari wote ambao wamepelekwa kwa operesheni ya Comoro.

Alikuwa akijibu swali la Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi, Saed Kubenea aliyetaka kujua jinsi serikali itakavyowalinda askari watakaojeruhiwa au kufa huko Comoro.

``Tunawahakikishia wananchi kwamba serikali itaendelea kuziangalia familia za askari wote tuliowapeleka Comoro huku tukiwahakikishia usalama wao,`` alisema Waziri Mwinyi.

Kanali Bacar ambaye aliingia madarakani katika maasi mwaka 2001 alijitangazia ushindi wa kuwa Rais wa Anjouan mwezi Juni mwaka jana katika uchaguzi ambao haukuwa halali.

Tangu ajitangazie madaraka hayo, Kanali Bacar amefunga Uwanja wa Ndege, bandari pekee ya Comoro, Anjouan na kumzuia Rais wa Shirikisho la Comoro, Mohamed Abdallah Sambi asiingie kisiwani humo. Sambi ni mzaliwa wa Anjouan na familia yake iko huko.

Shirikisho la Comoro linaundwa na visiwa vya Muheri, Anjouan na Ngazija na mbali na rais wa shirikisho, kila kisiwa kina rais wake.

Kuna kisiwa kingine cha Mayotte ambacho hakijajiunga na shirikisho na hivyo kinatawaliwa na Ufaransa.

SOURCE: Nipashe
 
[ Kama ni hivyo ina maana hakuna vikao vya mara kwa mara kupanga/kujadili/kufuatilia mikakati ya maendeleo inavyotekelezwa nk. Hii inatia wasiwasi uwezo na ubora wa uongozi wa Mh. JK. Hivi anaendeshaje nchi bila kukutana na timu yake? Hivi anaelewaje yanayoendelea kwenye wizara zake au kila waziri anafanya anavyoona yeye mwenyewe inafaa? Kazi kubwa tunayo, sura nzuri imetuponza.

Tungejuwa tungemchagua Mbowe awe Rais wetu
 
[ Kama ni hivyo ina maana hakuna vikao vya mara kwa mara kupanga/kujadili/kufuatilia mikakati ya maendeleo inavyotekelezwa nk. Hii inatia wasiwasi uwezo na ubora wa uongozi wa Mh. JK. Hivi anaendeshaje nchi bila kukutana na timu yake? Hivi anaelewaje yanayoendelea kwenye wizara zake au kila waziri anafanya anavyoona yeye mwenyewe inafaa? Kazi kubwa tunayo, sura nzuri imetuponza.

Tungejuwa tungemchagua Mbowe awe Rais wetu

Not necessarily. CCM walikuwa na wagombea wazuri sana wawili kati ya finalist watatu. Lakini kwa mikwara iliyopo ndani ya CCM, akachaguliwa mbovu kati yao, kwa vile tu mwenyekiti, Mkapa, alitaka mtu wa kumlinda, mission town badala ya uchaguzi halali. Matokeo ndio haya tumeibua Vasco da Gama, wakati nchi ilikuwa inahitaji mchapa kazi mwenye kuona mbele.
 
Yani nimegundua humu ndani kuna watu wengine wanabwabwaja, eti cabinet haina kazi yakufanya. that is such non-sense.. Maamuzi yote ya uendeshaji wa nchi wa day to day unafanyika Cabinet... unashuhulikiwa na Cabinet secretariat. Mawaziri wanachangia mada mbali mbali kuhusu the many issues that arise. It is held once every thursday... Most of the Time Ikulu DSM, Dodoma Chamwino when the House is in session. This is the way in most countries especially in the commonwealth. UK in every tuesday number 10.

Mjinga mmoja ameongelea mavazi, eti hayako serious!!! HA!!?? Yani vapour vapour... siamini wanaJF wengine wanachangia mvuke badala ya MADA... About the issue of Karume, it is true kwamba jamaa bado hajaa apishwa na anaona uzushi kuapishwa na Rais... From the point of view of Zanzibar's autonomy..or semi-autonomy.. He is right... Inaishusha hadhi SMZ, and these are amongst the issues being raised kwenye Mambo ya Muungano..

MARAIS WALIOFUATIA ZANZIBAR BAADA YA IDRIS ...WAMEKUWA WAKOROFI KIDOGO KUHUSU KUAPA...LAKINI HISTORIA INAONESHA NA REKODI PALE IKULU ZIPO KUA BABA YAO ..YAANI..ABEID AMANI KARUME..ALIAPA KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ..NA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI..MBELE YA MWALIMU..NA MARA ZOTE KARUME SR ALIONA FAHARI KUWA MAKAMU WA RAIS WA NCHI KUBWA TANZANIA.....

NADHANI TURUDISHE MAMLAKA YA RAIS WA ZANZIBAR KAMA MAKAMU WA RAIS ..WAZIRI MKUU ARUDI KUWA MAKAMU WA KWANZA AU WA PILI WA RAIS ....HII ITAMFANYA RAIS WA ZANZIBAR ASIWE INFERIOR ANAPOKUJA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI ...MAANA SASA SIMPLY ANAKUWA MSIKILIZAJI TU....NA KWA ZANZIBAR ILIVO NDOGO KUNA WAKATI RAIS WA ZANZIBAR SIMPLY ANAAMKA ANAKUWA HAJUI AFANYEJE..ZAIDI YA KUKAGUA MASHINA YA WAKEREKETWA KAMA ALIVYOKUWA SALMIN AU KUSHINDA NDANI ANAKUNYWA WHISKY NA KULALA KAMA AMANI.....

MTAGUNDUA KARUME SR NA ABOUD JUMBE NA HATA WAKIL..WALIKUWA WAKIZUNGUKA SANA MIKOANI TANZANIA YOTE ...NA KUWAKILISHA RAIS NJE ...KWA KUWA WALIKUWA NA KOFIA YA UMAKAMU WA RAIS....NAFIKIRI TURUDI KULE KAMA TUNATAKA MUUNGANO IMARA!!!
 

MARAIS WALIOFUATIA ZANZIBAR BAADA YA IDRIS ...WAMEKUWA WAKOROFI KIDOGO KUHUSU KUAPA...LAKINI HISTORIA INAONESHA NA REKODI PALE IKULU ZIPO KUA BABA YAO ..YAANI..ABEID AMANI KARUME..ALIAPA KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ..NA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI..MBELE YA MWALIMU..NA MARA ZOTE KARUME SR ALIONA FAHARI KUWA MAKAMU WA RAIS WA NCHI KUBWA TANZANIA.....

NA KWA ZANZIBAR ILIVO NDOGO KUNA WAKATI RAIS WA ZANZIBAR SIMPLY ANAAMKA ANAKUWA HAJUI AFANYEJE..ZAIDI YA KUKAGUA MASHINA YA WAKEREKETWA KAMA ALIVYOKUWA SALMIN AU KUSHINDA NDANI ANAKUNYWA WHISKY NA KULALA KAMA AMANI.....

MTAGUNDUA KARUME SR NA ABOUD JUMBE NA HATA WAKIL..WALIKUWA WAKIZUNGUKA SANA MIKOANI TANZANIA YOTE ...NA KUWAKILISHA RAIS NJE ...KWA KUWA WALIKUWA NA KOFIA YA UMAKAMU WA RAIS....NAFIKIRI TURUDI KULE KAMA TUNATAKA MUUNGANO IMARA!!!
Kamanda taratibu hapo...!
 
Unajua topic zingine hata pa kuanzia huelewi, Karume anaweza kugoma kwenda kwenye mkutano wa serikali na CCM? Aliyempora urais Bilali na kumpa yeye ni nani? Hiyo jeuri Karume ataitoa wapi?

Ukweli ni kwamba sio lazima Karume, ahudhurie kila mkutano wa cabinet au CCM, Karume ni rais wa visiwani, kwa hivyo anazo schedule zake za kirais ambazo haziwezi kuvunjwa ki-protocal kwa sababu ya mikutano ya dharura ya CCM au cabinet, sidhani kama mtu anahitaji shule kuelewa hili!
 
Unajua topic zingine hata pa kuanzia huelewi, Karume anaweza kugoma kwenda kwenye mkutano wa serikali na CCM? Aliyempora urais Bilali na kumpa yeye ni nani? Hiyo jeuri Karume ataitoa wapi?

Ukweli ni kwamba sio lazima Karume, ahudhurie kila mkutano wa cabinet au CCM, Karume ni rais wa visiwani, kwa hivyo anazo schedule zake za kirais ambazo haziwezi kuvunjwa ki-protocal kwa sababu ya mikutano ya dharura ya CCM au cabinet, sidhani kama mtu anahitaji shule kuelewa hili!

Hii ni kumdhalilisha Karume kusema kuwa alipewa uraisi na sio kuwa ana-qualify. Muhimu ni kufahamu kuwa kama kikao kiliandaliwa siku kadhaa na sio cha kushtukizia, kwanini karume hayupo hasa ikitiliwa maanani kuwa raisi alitaka pia kuwaeleza kuwa vijana tayari wako Anjuan, Comoro?
 
Mkuu kuwepo au kutokuwepo kwa demokrasia ndani ya CCM, will never help any of your misery ambayo unaionyesha hapa kila siku na very angry comments, CCM ina katiba na mipangilio yake,

Halafu unaonekana kuwa mgeni sana na bongo, maana haya yalipotokea yalitangazwa kila kona ya bongo, sasa nina mashaka kama kweli wewe ni mbongo maana haiweezekani kila kitu huelewi, na huenda ikawa a waste of time hata kujadili ishus na wewe maana mengi sana huelewi yanayotokea bongo kila siku mkuu, nafikiri ninahitaji kuiangalia hilo kwa makini.

Ahsante Mkuu.
 
Back
Top Bottom